Hivi vazi la taifa limekwenda wapi?

Kuuliza si ujinga anayeuliza anataka kujua..
Ndugu wanajamvi, hoja na mchakato wa vazi la taifa umefikia wapi? What is the status...?

kesho jioni wanakuja nyumbani kwako kuchukua maoni ya familia yako,
kabla hawajaja unatakiwa kuwagharimia

1) usafiri,

2) posho ya kibunge,

3) malazi (tahadhari kama my wife wako ana viwango ingawa hata kama una binti anaweza kufanyiwa sensa bila dodoso)

4) vitafunwa na juice ya hadhi ya ikulu,

5) posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi,

6) posho ya kufanya kazi kwenye mazingira magumu,

7) posho ya kuongea,

8) posho ya vishawishi.
 
wana JF ebu leo tujadili kuhusu vazi la taifa!Litapatikana lini?

Kamati/Tume ya vazi la Taifa inafanya warsha,makongamano,semeni elekezi ya vazi la taifa lakini mpaka leo hawajafikia muafaka wa vazi la taifa!!

My take! Napendekeza Gwanda la CHADEMA liwe vazi la taifa.
 
Wewe hauna vazi lako? Hilo ndilo la Taifa. Unategemea Joseph Kusaga anayefuga maelfu ya mashorobalo wanaovaa Kimarekani kwenye redio yake ya Clouds na TV akupe vazi la Taifa? Lipi? Alipoteuliwa tu kuongoza kamati ya vazi la Taifa basi nilipata jibu moja tu UFISADI
 
Nafikiri kuamuru vazi fulani la taifa ni wazo ambalo ni la kidikteta. kwa maoni yangu hapana haja yoyote ya kuamuru vazi la taifa au chakula cha taifa au mnyoo wa taifa au kiatu cha taifa.
 
Kama kweli kuna kamati imeundwa kwa ajili ya vazi la taifa, basi huo ni usanii kama sio ufisadi!!!
Enzi zile vazi la taifa LILIPOJITOKEZA kuwa suti ya chuenlai (hususan kwa wanaume) ambapo iliendelea ku-evolve na hatimaye kuwa suti ya Kaunda, Hayati JKN ndiye aliiva kwanza na watu wengine wakawa wanajiona fahari kuvaa kama yeye. Kwa hivyo, leo hii haishangazi kuona wanaume wanajiona fahari au kujifanya hivyo kwa kuvaa suti anayovaa Mhe Rais Dkt JK. Kwa maneno mengine, vazi la taifa ni hilo hilo wanalovaa Baba na Mama M.w.a.n.a.a.s.h.a.
 
Wameshakula chao.Ila msijali kuna vazi jipya la taifa ileshaanza kusambaa mitaani ambalo ni nguo zenye viraka kutokana na ugumu wa maisha.
 
Teh, teh, teh, kwih, kwih, kwih! Hivi Mkuu kumbe mgeni na hii nchi! Ule ulikuwa mpango wa wahuni kupiga hela, si unajua usanii ni kuigiza? Basi Msanii aliwapa dili wasanii wenzie wamepiga hela wametulia! Besides ahsante kwa kutukumbusha maana Tanzania tunashika nafasi ya 3 Duniani kwa kusahau mambo.
 
Kusaga amepewa hela ameenda kumleta kwenye fiesta Rickroos kutoka marekani, hapo hakuna jpya
 
wana JF ebu leo tujadili kuhusu vazi la taifa!Litapatikana lini?

Kamati/Tume ya vazi la Taifa inafanya warsha,makongamano,semeni elekezi ya vazi la taifa lakini mpaka leo hawajafikia muafaka wa vazi la taifa!!

My take! Napendekeza Gwanda la CHADEMA liwe vazi la taifa.

Vazi la taifa la kazi gani, ndio upuuzi wa serikali ya CCM. watu wana matatizo lukuki, ccm wanafikiria vazi!
 
wana JF ebu leo tujadili kuhusu vazi la taifa!Litapatikana lini?

Kamati/Tume ya vazi la Taifa inafanya warsha,makongamano,semeni elekezi ya vazi la taifa lakini mpaka leo hawajafikia muafaka wa vazi la taifa!!

My take! Napendekeza Gwanda la CHADEMA liwe vazi la taifa.
Mwandishi mmoja TZ DAIMA ALIJITOA MAPEMA,NA KAMA UNAVYOJUA BILA YA CDM HAMNA KINACHOFANYKIA!
 
kina kibonde wakajipendekeza weee masaa tote ya jahazi na uchafu tele. aaargh another ufisadi in the making by magamba.
 
kina kibonde wakajipendekeza weee masaa tote ya jahazi na uchafu tele. aaargh another ufisadi in the making by magamba.
 
ukitaka kuona umuhimu wa vazi la taifa,subiri siku ya afrika,kwa tanzania ni aibu,huwezi hata kuelewa uvae vazi lipi,na hii ni kwa wale waliopo nje ya tanzania ndio utayaona haya,ila ukiwa tanzania ni kawaida tu na huoni umuhimu wake,muda mwingine huwa tunavaa jezi ya taifa ya mpira
 
Sasa hivi wako busy na kupigia kura vivutio vya tanzania iwe kwenye maajabu ya dunia.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Vazi la taifa litakusaidia nini??
Watu (wajumbe) washagawana hela za kamati, we endelea kusubiria hilo vazi.

Mi najigongea zangu "model" na shemeji yako na mashori wengine wa kitaa + ofisini wananikubali, so ndilo vazi langu la taifa.
 
Back
Top Bottom