Ernesto Che
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,114
- 293
Kwa muda mrefu sasa CHADEMA imekuwa inahamasisha washabiki/wapenzi wake kujiunga na M4C, au Movement For Change (kwa kiingereza). Wakati mwingine wanaona kwamba jambo lao fulani limefanikiwa, basi ni kutokana na nguvu ya M4C, na kadhalika, na kadhalika......... Baada ya kuambiwa kuwa huko Uingereza (UK) kuna chama kinachoitwa Movement for Change ambacho pia kinatumia kifupisho cha M4C nikashawishika kuona kama kuna uhusiano wowote na CHADEMA.
Baada ya kusoma tovuti yao (Movement for Change | Home), sioni uhusiano wa moja kwa moja zaidi ya ku-copy jina la chama cha wazungu hao. Swali langu, je CHADEMA wameanzisha M4C yao wakiwa wanajua haya? Kama ndivyo, najua kuwa CHADEMA ina uhusiano fulani na chama cha Conservertive cha Uingereza, lakini M4C hiyo ya Waingereza ina mahusiano na chama cha Labour cha Uingereza! Hapa pana nini? Jina la jinsi hii si sawa na Athmani au Jane ambalo mtu unaweza kujiita pamoja na kujua kuwa wapo wengine wenye jina hilo. CHADEMA watufafanulie hili!
Kwani ukombozi unamilikiwa na waingereza? acha uzushi wewe