Hivi unajua juu ya hizi picha

tamimusalim

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
1,822
494
ImageUploadedByJamiiForums1407868887.851406.jpg ImageUploadedByJamiiForums1407868965.092070.jpg Hizi ni picha zinazoonyesha mawindo ya miongoni mwa wanyama katika mbuga , na maeneo yetu hapa tanzania,lakini katika hali ya kushangaza hizi picha zimetia fola au zimekuwa ni picha zilizovutia na kupendwa na watu wengi barani ulaya,kwetu sisi afrika ,hasa hapa tanzania tunaweza kuona picha isiyokuwa na umuhimu mkubwa rakini hali hii ni tofauti na wenzetu uko ulaya na marekani, pia kupatikana na kuonekana picha hizi katika ukurasa wa mbele wa magazeti na majarida mengi kuliamashisha watalii wengi kuja katika mbuga zetu hasa hapa tanzania,pia zimekuwa ni picha bora sana za msituni kupigwa 2013/2014
 
Wahusika bado hawajafanikiwa kushawishi utalii wa ndani. ..Gharama ziko juu kwenda kuona hao wanyama live. ..
Tunaishia kuangalia kwenye TV na mtandaoni. ...
 
Hapa ndipo hatuelewi!!mtalii ni mtu anaekuja kushangaa kitu ambacho kwao hakuna,sisi hatuoni thamani yake kwa kuwa vitu hvyo ni vya kwetu!Nasi tukienda nje ulaya,marekani nk tutashangaa vile ambavyo kwetu havipo!
kweli kama magari ya bei mbaya ,magholofa,na ushoga
 
Naona mleta mada unatulazimisha kushangaa mambo tuliyoyazoea
 
Naona mleta mada unatulazimisha kushangaa mambo tuliyoyazoea
duuu mwana jf mbona mgumu kuelewa thread nilikwambia katika iyo uzi kuwa " kwetu hapa tanzania inawezekana ukaona picha ya kawaida ila hii ni tofauti na wenzetu ulaya na marekani na kwingine ni kitu chenye mshangao mkubwa sana sasa hapo umelazimishwa wapi?
 
Wazungu nao washamba sana, nakumbuka 2010 SA kipindi cha world cup team england yote waliacha mazoezi kisa wanashangaa mbuzi waliokuwa wanapita karibu na training ground, sio bekham, gelard wala bosi wao capello wote walikua wanashangaa mbuzi.

Hahahaa aisee mkuu umeshawahi nje ya Tz hata mara moja? Huenda kuna wanaoona hao mbuzi lakini nikuambie sio kirahisi kuona mbuzi akitembea free huko ulaya. Sio rahisi kuona kuku, mbuzi ama ng'ombe anazurula au hata kafungiwa kwa banda la mtu kama hapa kwetu tz. So we kuwaita washamba unakosea mkuu hayo mambo yapo
 
Kwangu mimi namsifia mzungu aliyekaa mbugani muda mrefu. Yawekana mwaka mzima au zaidi kupata picha ya aina hiyo. Watanzania hatuwezi kushangaa sana wanyama kwa sababu ni sehemu ya maisha yetu. Tukisafiri, maeneo tunapoishi, wanyama ni sehemu yetu. Timu ya Uingereza ilishangaa mbuzi kwa sababu inawezekana huko kwao hawajawahi kuwaona wala hawaamini kama mbuzi anaweza akarandaranda mitaani ovyo. Hata sisi tukienda kwao ulaya tunashangaa jinsi majengo yao yalivyo marefu na treni zao zinavyoenda kwa kasi. Hivyo mshangao siiti ushamba unaweza kumtokea mtu yeyote ambaye ameona jambo geni kabisa kwake. Mwisho wakati namsifia aliyetumia muda wake mwingi kupata picha hizo nawaasa wapiga picha kkuumba vibali na kwenda kukaa mbugani kitafuta picha bora kama hizo kuliko kuishia kupiga picha za harusi tu.
 
ni sawa na wachagga wanatokea kilimanjaro lakini HAWAJAWAHI KUKWEA JUU YA MLIMA HUO
 
View attachment 177121View attachment 177122 Hizi ni picha zinazoonyesha mawindo ya miongoni mwa wanyama katika mbuga , na maeneo yetu hapa tanzania,lakini katika hali ya kushangaza hizi picha zimetia fola au zimekuwa ni picha zilizovutia na kupendwa na watu wengi barani ulaya,kwetu sisi afrika ,hasa hapa tanzania tunaweza kuona picha isiyokuwa na umuhimu mkubwa rakini hali hii ni tofauti na wenzetu uko ulaya na marekani, pia kupatikana na kuonekana picha hizi katika ukurasa wa mbele wa magazeti na majarida mengi kuliamashisha watalii wengi kuja katika mbuga zetu hasa hapa tanzania,pia zimekuwa ni picha bora sana za msituni kupigwa 2013/2014

Kwangu mimi namsifia mzungu aliyekaa mbugani muda mrefu. Yawekana mwaka mzima au zaidi kupata picha ya aina hiyo. Watanzania hatuwezi kushangaa sana wanyama kwa sababu ni sehemu ya maisha yetu. Tukisafiri, maeneo tunapoishi, wanyama ni sehemu yetu. Timu ya Uingereza ilishangaa mbuzi kwa sababu inawezekana huko kwao hawajawahi kuwaona wala hawaamini kama mbuzi anaweza akarandaranda mitaani ovyo. Hata sisi tukienda kwao ulaya tunashangaa jinsi majengo yao yalivyo marefu na treni zao zinavyoenda kwa kasi. Hivyo mshangao siiti ushamba unaweza kumtokea mtu yeyote ambaye ameona jambo geni kabisa kwake. Mwisho wakati namsifia aliyetumia muda wake mwingi kupata picha hizo nawaasa wapiga picha kkuumba vibali na kwenda kukaa mbugani kitafuta picha bora kama hizo kuliko kuishia kupiga picha za harusi tu.

My God! Nimezipendaje, picha kama hizi zilitakiwa kuwepo katika mitaala za shule katika somo husika.

Tanzania tunatatizo kama si matatizo mojawapo idara ya utalii hakuna ubunifu, Cassian Mdami wa Channel ten ndiye mtu pekee ambaye anatuzibua fahamu zetu kuhusu National Parks. Shame on you TANAPA, Ubunifu Zero.
 
Hahahaa aisee mkuu umeshawahi nje ya Tz hata mara moja? Huenda kuna wanaoona hao mbuzi lakini nikuambie sio kirahisi kuona mbuzi akitembea free huko ulaya. Sio rahisi kuona kuku, mbuzi ama ng'ombe anazurula au hata kafungiwa kwa banda la mtu kama hapa kwetu tz. So we kuwaita washamba unakosea mkuu hayo mambo yapo
sawasawa ukiwa umekaa ulaya ni nadra sana kumuona mbuzi kuku hata ng' ombe hovyohovyo kama huku kwetu,yeye uyo ndio mshamba ila hao wa wazungu walikuwa sahihi
 
My God! Nimezipendaje, picha kama hizi zilitakiwa kuwepo katika mitaala za shule katika somo husika.

Tanzania tunatatizo kama si matatizo mojawapo idara ya utalii hakuna ubunifu, Cassian Mdami wa Channel ten ndiye mtu pekee ambaye anatuzibua fahamu zetu kuhusu National Parks. Shame on you TANAPA, Ubunifu Zero.
kweli kabisa cha kushangaza utakuta sijui picha ya nyerere kashika mwenge, yaani mambo ya kishetani tupu
 
Ni kweli kabisa mkuu, ni picha za kushangaza....kwanza kuzipata kwake sio kazi rahisi. Asante wazungu kwa kutupigia picha nzuri kama hizi, maake sisi waswahili hatuna uwezo wa kupiga picha hizo.
 
Ni kweli kabisa mkuu, ni picha za kushangaza....kwanza kuzipata kwake sio kazi rahisi. Asante wazungu kwa kutupigia picha nzuri kama hizi, maake sisi waswahili hatuna uwezo wa kupiga picha hizo.
yaani hata wazungu uko ulaya wamezipenda sana tena walishangaa mpigaji alikuwa wapi, yaani ndio maana kushika picha bora za msituni kwa miaka 2mfululizo safi sana wazungu
 
Hapa ndipo hatuelewi!!mtalii ni mtu anaekuja kushangaa kitu ambacho kwao hakuna,sisi hatuoni thamani yake kwa kuwa vitu hvyo ni vya kwetu!Nasi tukienda nje ulaya,marekani nk tutashangaa vile ambavyo kwetu havipo!

Kwenu kivipi?Maana watanzania si wote wanatokea maeneo yenye vivutio maana vipo nchi nzima.sasa kama hujawahi kutembelea maeneo hayo we ni sawa na mgeni.Au unazungumzia kuwaona wakivuka barabara mkuu.
 
Picha nzuri sana!Huwezi amini kama zimepigwa nchini kwetu.Ni wakati muafaka kwa wapiga picha wetu kujifunza kutafuta picha nzuri kama hizo,kwani wao wameweza wana nini na sisi tushindwe tuna nini?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom