Hivi ukumbi wa Deleuxe Mwanza bado upo?

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Nilipita pale kwa michuzi na nikaona picha ya deleuxe Mwanza,imenikumbusha mbali sana...way back nilipokuwa Mwanza mwaka 2000.Mlioko huko naomba mniambie kama bado upo.

Nilikumbuka ukumbi huu ulikuwa na mlango mmoja tu wa kutokea,Hisia zimenipanda sana baada ya ile ajali iliyotekea Tabora na kuua watoto..Kama bado upo basi tutarajie maafa mengine tu ..

Naomba mtu mwenye habari atuambie...Mwanakijiji unapakumbuka hapo?
 
Still ni mlango mmoja kutokea kama Rumours na kumbi zingine kama The kiss,Villa na kwingine.Naona wao wanajari sana security kuliko madhara ya moto kuwaka kwenye mlango.Harafu mkashidwa kutoka kabisa.
 
Gembe,

Hadi mwaka jana mwezi wa nane huo ukumbi ulikuwepo..nilifika pale ila pamechoka mno...sina hakika kama uta(una) survive dhoruba za kumbi kama villa park,capri cabana etc..
 
Nilipita pale kwa michuzi na nikaona picha ya deleuxe Mwanza,imenikumbusha mbali sana...way back nilipokuwa Mwanza mwaka 2000.Mlioko huko naomba mniambie kama bado upo.

Nilikumbuka ukumbi huu ulikuwa na mlango mmoja tu wa kutokea,Hisia zimenipanda sana baada ya ile ajali iliyotekea Tabora na kuua watoto..Kama bado upo basi tutarajie maafa mengine tu ..

Naomba mtu mwenye habari atuambie...Mwanakijiji unapakumbuka hapo?
...Gembe,
Nilikuwa nahudhuria sana Deluxe miaka ya 1998 -2000 na honestly kitendo cha ule ukumbi kuwa ghorofani na mlango wa kutokea mmoja kuna siku kilinifanya niwaulize wahusika kama kweli hawaoni hatari iliyopo kama kukitokea moto maana hata madirisha yamewekwa grill.

Tatizo la watu wetu ndio hilo wanaangalia pesa kuliko usalama wa hao watu wanaowapatia pesa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom