Hivi ukitaka kushiriki kipindi cha malumbano ya hoja itv...wanangalia sifa gani

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Wadau napenda kujua hivi mtu mpaka unashiriki kipindi cha malumbano ya hoja kipindi cha itv....wanangalia sifa gani....maana kuna kipindi kimerushwa leo na mada ambayo imenigusa ya polisi kuua raia lakini nashangaa wachangiaji wote wana mawazo sawa hivi waliangalia sifa gani

kuchukua watu kwenye kipindi
 
inabidi usiwe na akili ya kufikiri mwenyewe, ukifika pale uwasikilize wanataka useme nini kisha ufanye hivyo, jana wamenitesa sana sababu nililazimika ku-mute tv kila baada ya muda mfupi maana wachangiaji walikuwa hawana point za maana, na nilikuwa na hasira kuwasikia wakiongea hovyo
 
Wadau napenda kujua hivi mtu mpaka unashiriki kipindi cha malumbano ya hoja kipindi cha itv....wanangalia sifa gani....maana kuna kipindi kimerushwa leo na mada ambayo imenigusa ya polisi kuua raia lakini nashangaa wachangiaji wote wana mawazo sawa hivi waliangalia sifa gani

kuchukua watu kwenye kipindi

Katika kipindi hicho wachangiaji wengi walikuwa askari polisi waliojifanya ni raia wa kawaida. Hizo ni mbinu za kitoto kwani askari polisi anatambulika kwa mwonekano, maneno na matendo yake hata asipokuwa katika mavazi rasmi (sare). Walikuwa amejipanga kuwashambulia wanaharakati na wanasheria wanaotetea haki za binadamu dhidi ya vitendo vya askari polisi kuwaua raia wasio na hatia wanapoandamana kuwasilisha ujumbe wa madai/malalamiko yao. Sikuamini kauli zao kama watu hao ni Watanzania wenzetu au wamekodiwa kutoka nje. Wakati wanzungumzia utii wa sheria bila shuruti kwa raia, lakini hawazungumzii haki ya kuishi, haki ya maandamano kama moja ya njia ya kuwasilisha ujumbe baada ya hatua za mazungumzo kushindikana. Hawatoi majibu juu ya wajibu wa serikali kuwapa maisha bora raia wanaoteseka katika nchi yao yenye utajiri wa ajabu duniani. Ni vipi amani na utulivu vipatikane bila haki?
 
Ndugu yangu lazima uwe mjingamjinga na mwehu ndo ushiriki hicho kipindi. Hawataki mtu timamu pale.....Hongera sana ITV
 
Wala usiumize kichwa mkuu yale yalikua maigizo.. it was a staged thing, nchi hii sijui tunaelekea wapi
 
Back
Top Bottom