Hivi ukigundua mumeo anaku-cheat na inajulikana public, utafanyaje?

ila kusalitiwa kunauma jamani nyie acheni kusikieni kwa mwenzako kusikufike....kama huna busara na hekima na mungu pia waweza fanya maamuzi ya ajabu sana...mi naona na maombi yanahitajika sana kumuombea mwenz wako mungu awaongoze na kuwaweka mbali na vishaishi...

ndo mana wanasema mwenza wako usimpukunyue pukunyue,haya mambo ya kuchungulia simu ya mmeo,wallet mara baba upekue handbag ya mrs,ya nini yote hayo,unataka ukute nini?
 
bidada mtoa mada naomba nikwambie hivi kucheat kwa mumeo na kujulikana hadharani siyo mwisho wa maisha hata kidogo, wala haisimamishi sekunde moja katka saa. so life goes on. ukishalijua hili akilini mwako na ukijua ya kwamba ni tabia yake ndio maana imeonekana hadharani na pengine yawezekana ikawa inamuumiza au la fanya hivi.

muombe sana mungu akupe amani na furaha japo ni ngumu kuipata lakin hii utaipata kwa kuweka dharau juu kila anacho kifanya na pia usitake kabisa kusikia the rest of the stories. hii itakupa amani sana nafsi ili uweze kutimiza wajibu wako wa ndani kama mke kama ntakavyoongea hapa chini:-

wewe jiangalie upya mamii katika kila eneo lako kisha jipange upya. timiza wajibu wako kama mama ndani ya nyumba in such a way that asikukute na kosa la namna yeyote ile,menu ndani fresh, house cleaned, washings and ironing ziko ok, kids wako ok.

ukishavisimamia hivyo vizuri kaabisa kwa uaminifu, the next thing rudi kwako jipige pamba za nguvu, kila siku uwe kama malkia humo ndani, uamkapo haijulikani wala ulalapo pia haijulikani.Pendeza sana kila siku atleast uvae zile nguo ambazo zinakutoa uwe malkia haswa haswa. Na penyewe hapo usilumbane naye uwe kimya weka na mungu akusaidie usimuulize ila aone matendo yako tu kuwa yamebadilika.

ukiyaweza hayo basi fanya hivi, tafuta njia ya kuongeza kipato chako hata kama utafunga maji na juice uuze ili ukwepe kumuomba omba hela. hii itakupa amani sana na itamfanya aone aibu sana. Siku huna pika kilichopo na akiuliza mwambie wazi kuwa hukuwa na alternative nyingine. na penyewe hapo uwe na amani yako moyoni.

kama waweza basi uwe unapenda kutoka muda mwingi ujichanganye na watu labda harusin kuona wagonjwa na muda mwingine toka na wanao yaani mpaka hapo nakufundisha jinsi ya kumpaunish kwa isolation. ukimudu hapo rafiki nakuambia atarudi tu ndani. Njia hii naiamni sana katika kurudisha mtu wa namna hiyo manake imefanya kazi kwa watu walioitumia. Pia jua kuwa ndoa kama hamjaish miaka zaid ya 7 utapita magumu sana so lazima ujue utavuka vipi and beleive me or not mwanaume bila kufika miaka 40 hawez kuwa na kaili iliyotulia na hapa ntakosolewa sana lkn ndio ukweli hivyo lazima ujue hiyo ni changamoto.

pia sasa jua kabisa kwenye ndoa yeyote matatizo makubwa yanapotokea akina mama wanakuwaga ni wahanga sana na pia kwasababau ya kuhamalika huwa wanashindwa jinsi ya kufanya.

matokeo ya ndoa zinazopata shida as for me na siyo sheria lakini huwaga naona njia 3 ndizo lazima ziwe ni suluhu
1)Reconciliation- na hii waweza ifanya kwa njia niliyokuambia hapo juu siyo laizma watu wakae wajadili maswala ya familia yako while you can work on it.

2)separation - hapa yalazimika kupeana muda kwanza kila mmoja akae mbali na mwenzake halafu hatua hii itapelekea wazazi kuingilia kati kuwaleta pamoja.during separation mtu huweza kubadilika na kuvaa utu mpya so bado yaweza kuwa ni njia ila pia yaweza kusababisha mtandao msipokuwa makini

3)divorce- binafsi huwa hii siipendelei sana ila when needs arises mtu unakaa pembeni kuepusha msongamano. na haii haitahitaji mwanakamati wa kujadili tena manake umesha fikia mwisho wa kila kitu.

naona niishie hapo nisikuchoshe kusoma ma dia. kama hujaelewa uliza.
Dada kuna wengine ni magume gume haswaa nakwambia unavumilia tu ila chamoto unakiona.
 
nikijua nachapa yebo home kwetu

Ss ukiondoka si ndio unampa mwanya huyo kuja kujenga ngome ....labda kama hukumpenda huyo mume wako kwa dhati ama nawe unasehemu yakujishikiza/inakupa kiburi ila kama huna utampigania mpaka mwisho wa pumzi yako chezea kupenda ww:......yani ukiona mtu hakupiganii/haumpiganii jua hujaugusa/hajaugusa bado mtima wake/wako kabisaaa
 
ndo mana wanasema mwenza wako usimpukunyue pukunyue,haya mambo ya kuchungulia simu ya mmeo,wallet mara baba upekue handbag ya mrs,ya nini yote hayo,unataka ukute nini?

Yan ukitaka magonjwa ya moyo na pb huko ndio kwenyewe
 
wengine wanacheat si kwa sababu wametibuliwa na wake zao bali ni hulka zao tu na spirit ya uzinzi, hakuna zaidi ya hapo...kama unampenda mkeo hata akikukosea vp unatakiwa kukaa naye mrekebishe, ili maelewano yatawale, ndio mtasonga mbele vzr...acheni hulka za ajabu ajabu jamani!
ni kweli jamiif wengine ni hulka tu, lakini hata kama ni hulka na ukajua kuwa ni hulka haswa kipindi hiki cha maradhi, basi ni lazima kuongea naye na sala mbele ya aliyewaunganisha, inasaidia amini usiamini kumbadilisha! ila jamani TUMUOGOPE MUNGU, TUSICHEAT! wanandoa hatuna hofu ya MUNGU tena ndio maana tooooo much cheatings.
 
Last edited by a moderator:
Mwanamke mjinga atavunja ndoa yeke kwa mikono yake, ye mwenyeweeee
 
Mwanamke mjinga atavunja ndoa yeke kwa mikono yake, ye mwenyeweeee

Kwahiyo mwanamke ndio kacheat eeh? Na huyo mwanaume aliyecheat havunji ndoa? Au beneficially wa ndoa ni mwanamke peke yake? To hell with ndoa kama ni ya dizaini hiyo!
 
Erotica amekwiva kwa sasa! nina imani naye vibaya mno, hawezi kutuangusha, na mume atampata hapahapa! Kaunga matron nakuaminia, hivi jana summary yake ulimpa?

Nilimpa hny, ila sijui alishindwa kudigest akaDO kwa forbidden style, leo tumbo linamuuma sana haid ikabidi aende kliniki. Dont worry, she should be fine kesho atakuja kwa mafunzo zaidi. Lol
 
hivi maumivu ya kuchitiwa in private na in public ni tofauti?????

Tofauti ni kwa wale ambao wanaishi jinsi watu wanavyotaka na si jinsi wanavyojisikia wao.

So akichit privately, unajua wewe tu na maumivu ni 3/4
Ila ikiwa publically, watu watakuonaje???? Maumivu ni 6/4!

LOL kwangu me, it makes no difirensi kabisa!
 
Back
Top Bottom