Hivi uheshimiwa kwetu una maana ile iliyokusudiwa?

Kiby

JF-Expert Member
Nov 16, 2009
6,897
4,620
Nimejaribu kutafakari juu ya hii title ya heshima tunayotumia kwa viongozi wetu kwa kuwaita 'waheshimiwa'. Kwa kweli nilichogundua ni kwamba kuna wanaostahili uheshimiwa, na baadhi hawakustahili kabisa uheshimiwa kiasi kwamba kuwaita waheshimiwa ni kama tunajitukana wenyewe kwa kujizihaki. Hivyo basi nimekuja na mapendekezo yafuatayo hapa JF.
(1)Mtu yeyote yule abaki kuwa ndugu/dada, mpaka hapo atakapojithibitisha kwamba kwa jitihada zake binafsi au kwa kushirikisha wengine zimeleta manufaa ya kimaendeleo kwa jamii.
(2) Kuwe na jopo la watu waliotukuka ndani ya jamii kuanzia ngazi ya jimbo hadi taifa watakaopewa mamlaka ya kisheria kumtangaza mtu kuwa ni mheshimiwa kwa minajili ya kazi zake zilizo wazi.
Hii inatokana na wimbi la baazi ya watu kuupata ubunge kwa njia za ajabu ajabu na za aibu, zaidi sana kwa kununua na hivyo kujikuta wakipewa heshima ya mheshimiwa wasioistahili kabisa. Na kibaya zaidi baazi yao wanajikuta wamefikia ngazi ya uwaziri.
Hili mnaliona je wana-JF?
 
Back
Top Bottom