Hivi uchaga ni kabila kweli? hebu angalia hii.........!

Ukiona jamii inajiita kwa jina moja wakati inaongea lugha tofauti basi ujue jamii hiyo inapenda umoja na mshikamano. Big up Wachaga.
 
yani mapka kero every day wachaga .. minutes topic wachaga jamani mtupe japo nafasi wapo wengi mbona i.e wandingo, wafipa, wazanaki e.tc maana ni kila day wachaga .. please give us space na wewe uliyeandika ni kabila gani kama vipi wape jina lingine ili uridhike lol

ni mjadala tu ndugu wala usikasirike,
 
Mtoa mada unazungumzia utofauti wa lafudhi ama wa lugha? Mfn Wapare wa Same, Usangi na Ugweno wanaongea lugha moja lkn wanatofautiana lafudhi the same kwa wachaga.
 
mbona sisi Waarusha hamtudiscuss na kila iku maneno mapya ya lugha yanaanzia Rchuga..mfano wiki mbili zilizopita tumeanzisha neno jipya ..KWIKWI LAANA..YANI NZURI SANA..MANENO YOTE YAKO ARUSHA

ukiona hivyo ujue hamna maana sana ktk eneo la huko
 
Umekosea nadahani mkuu. Mada ni kutoelewana lugha zao wamachame, wauru, wakibosho, wamarangu nk. HAWAELEWANI KABISA. Sasa hiyo mifano ya Mbeya umedanganywa, Wanyakyusa, Wasafwa, Wandali ni makabila tofauti, wakiongea waweza kudaka neno moja la hapa na pale lakini ni makabila tofauti. Umesema mwenyewe vema, hukusema wanyakyusa wa kisafwa, wanyakyusa wa kindali. Mwenzako kasema "Wachaga wa Uru, Wachaga wa Kibosho...." Unataka kupotosha mada ya kimsingi ambayo wengi wetu tumekuwa tukijiuliza miaka yote ingawa hatukuuliza kwenye jukwaa. Mjibu anachouliza mleta hoja usiwe kama bunge la sasa la dodoma kujadili watu badala ya hoja.

duuu! hapa unastahili 'like' yangu mkuu. nadhani wewe umemaliza issue yote ktk hili. ngoja tumsubiri
 
Mtoa mada unazungumzia utofauti wa lafudhi ama wa lugha? Mfn Wapare wa Same, Usangi na Ugweno wanaongea lugha moja lkn wanatofautiana lafudhi the same kwa wachaga.

Sio kweli mkuu. Lafudhi ni inaendana na matamshi bwana. Mtu akiongea kiingereza unaweza jua huyu ni mzanzibar, mnigeria, mganda, mhindi, muitaliano nk. tofauti ya sauti na matamshi ndiyo tunayoita lafudhi. ktk uchaga ni tofauti. kama ni kuku basi ataitwa kwa jina tofauti kati ya mmarangu na mmachame. tofauti. usitake kutuaminisha kwamba mmakonde anapoita chumvi munyu halafu mnyakyusa aiite isalt then hiyo ni lafudhi, si kweli hayo ni majina mawili tofauti na ndivyo ilivyo kwa wachaga, why?
 
Back
Top Bottom