Hivi ubakaji umekua fashion au?

s.fm

JF-Expert Member
Jul 8, 2009
663
117
Nimesikitishwa na story ya kwenye gazeti la habar leo "mwanafunzi mgonjwa abakwa, afa" huku taarifa zaidi zinasema alikua mgonjwa wa moyo na alifariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa wa Rukwa. huyu mwanafunzi alibakwa na genge la watu wasiofahamika huku wakifanya hivyo kwa zamu.

ukiachilia mbali habari hii, zipo nyingine nyingi sana ambazo tunazisikia kila kukicha yani mpaka nahisi ubakaji ni kitu cha kawaida vile....!

We must be very careful na ndugu zetu jamani..kaka,dada, na watoto tena ikiwezekana usiruhusu hata kama kuna mgeni (ndugu/rafiki) eti kaja nyumbani unamwacha alale na watoto/mtoto wako...yani kubaka these days is very easy mtu anachukua tu anavua ch*pi anaanza..

Yani mpaka leo hii watu wanashindwa kutongoza? wanawake wenyewe kibao tunapigana vikumbo tu mitaani huko...na wale wanaobaka watoto je? ni kiu, hamu ya kuona uchi wa mtoto, ushirikina, domo zege, au basi ti visa..! halafu eti tunaishi kwa amani, amani gani?

sijui hawa watu wanahitaji elimu ya namna gani...msaada hapa! and just remember this thing has been part of us, it is everywhere in this world
 
Sex maniacs find pleasure in rapping....

You know what, shida hatuwapimi akili wabakaji, some of them are maniacs....
 
Tatizo ni jamii kufumbia macho na kulea unyanyaswaji wa kijinsia. Ila kikubwa zaidi ni nchi kuendeshwa kishaghabaghala. Hatuko makini katika kufuata sheria. Hatuko wakali katika utekelezaje wake.

Manyanyaso tunayaona ni mambo ya kawaida. Mara zingine tunaelekeza lawama kwa wahanga na tunawaacha wakosefu wakipeta. Unadhania mkosefu akisikia watu wanamlaumu mhanga atafanya nini? Uwezekano ni atajisikia kupata hamasa na kuona pengine tendo lake si baya na kulirudia tena na tena bila hofu ya kupata adhabu.

Tunapenda sana kujidai sijui tuna maadili lakini ukweli wa mambo maadili hatuna kivile. Tuna mfano wa maadili tu. Maadili ya kweli sidhani kama tunayo. Tungekuwa tunayo tungekuwa wakali dhidi ya vitendo viovu kama hivi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom