Hivi tunahitaji IMF kutukumbusha na hili???

kamanzi

Senior Member
Oct 28, 2007
100
23
IMF YAIKALIA KOO SERIKALI

Yaitaka iangalie upya misamaha ya kodi
*yasisitiza ongezeko la kodi katika madini
Na Mnaku Mbani

MAOFISA wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) wameitaka serikali kuangalia upya suala la misamaha ya kodi, kuongeza wigo wa malipo ya Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT), pamoja na kuongeza wigo wa kodi katika madini ili kuongeza mapato ambayo nyanazidi kudorora.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema wiki hii na IMF, baada ya kumalizika mazungumzo baina ya maofisa wake na wale wa serikali, ushauri huo unalenga katika kuiwezesha serikali ya Tanzania kuongeza wigo wa ukusanyaji wa kodi.

“Wakurugenzi wamependekeza umuhimu wa kuongeza wigo wa kodi, kupunguza misamaha na kuongeza udhibiti wa fedha za umma. Wamependekeza kuongeza wigo wa ulipaji wa VAT na kuongeza wigo wa kodi katika madini,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo pia imekemea suala la Tanzania kuendelea kutegemea wafadhiri wa nje katika kuendesha bajeti yake kwani utegemezi unatarajia kukua hadi kufikia asilimia 10 ya pato la ndani la taifa (GDP) kwa mwaka huu.

Hali hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuwepo na taarifa kwamba serikali ya Tanzania inakumbwa na ukata mkubwa ambao umesababisha baadhi wa watumishi kuchelewezewa mishahara yao, huku ikiwa imebakia mwezi mmoja tu kumalizika kwa mwaka wa fedha 2010/2011.

Hata hivyo, waziri wa fedha, uchumi na mipango Mustafa Mkulo alikanusha vikali habari hizo juzi na kusema kuwa serikali ina hali nzuri ya kifedha na yote yanayosemwa ni siasa za kujitafutia umaarufu.

“Hali ya upatikanaji wa mapato na matumizi bado ina changamoto zaidi kipindi hiki: makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2010/2011 hayataweza kutimiza malengo ya bajeti kutokana na hali mbaya ha hewa, ukata wa fedha za matumizi ya serikali pamoja na riba za madeni ya nyuma. Kumekuwepo na upunguzaji wa matumizi lakini tunatarajia uthibiti zaidi wa matumizi,” imesema taarifa ya IMF.

“Wakurugenzi wamekubali kwamba mwaka 2011/2012 utakuwa ni hatua moja au nyingine ya serikali ya Tanzania kuboresha uthibiti wa fedha za umma. Tunatambua kwamba bei kubwa ya mafuta, hali ya hewa na upungufu wa misaada utasababisha matatizo katika kugharamia mipango ya bajeti, wameitaka serikali kuendelea kubana matumizi ili yalingane na hali halisi ya mapato.”

Maafisa hao wameiomba serikali kuongeza matumizi katika huduma za kijamii na miundombinu ambayo ina mrejesho mkubwa.

“Wakurugenzi wamesisitiza maofisa wa serikali kukamilisha mkakati wa kuratibu madeni ili kuhakikisha kwamba mikopo yote itakayokopwa inazingatia kupunguza riba,” inasema taarifa hiyo.

Hata hivyo, wakurugenzi hao wa IMF wamesisitiza umuhimu wa serikali kuangalia maendeleo ya mfumuko wa bei kwa kubana masharti ya masoko ya fedha ikiwa ni pamoja na kuangalia tatizo ya kushindwa kurudisha mikopo katika benki kwa baadhi ya wakopaji hasa watu binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo yenye kumbukumbu namba No. 11/53 iliyotolewa Mei 9, 2011, maafisa hao walisema kwamba ukuaji wa uchumi wa nchi kwa mwaka 2011 utashuka hadi kufikia asilimia 6 ikiwa hali ya bei za mafuta, umeme zinaendelea kwa muda mrefu.

“Kwa makadirio yetu ya kipindi cha kati, tunaona kwamba hali ya kiuchumi sio mbaya sana lakini kutakuwepo na changamoto za kisera. Kuongezeka kwa idadi ya watu kutaongeza changamoto katika utoaji wa huduma za kijamii achilia mbali kushuka kwa kodi na misaada,” ilisema taarifa hiyo.

SOURCE: MAJIRA

Hizi zingine aibu kubwa jamani. By the way, big up to Zitto kwa kurudi kundini. Sasa tunaweza kukaa meza moja na kuongea kama watoto wa kiume. Keep it up young man. Wavuruge hao mafisadi wakiongozwa na Kikwete mwenyewe!!!
 
Back
Top Bottom