Hivi tunahisi sifa tunapoambiwa wa Tz aliki zetu ni everage?

Babylon

JF-Expert Member
Feb 5, 2009
1,332
82
Juzi hapa seif khatib alihojiwa na kusema kuwa yeye hajauonapo waraka wa Mungano alichokiona yeye ni picha za wasisi wakikabidhiana waraka huo, cha kujiuliza leo inakuwaje wazi huyo huyo anawambia wabunge waende wakauangalie huo waraka upo kule katika maktaba ya bunge tokea Februari 11, 2002 sasa waziri huyu anashuhulikia Mungano wa aina gani? ambae hajapatapo kwenda kuona au kusoma huo mkataba mungano anaoushuhulikia huku akijuwa upo makta kwa miaka 7 sasa ?na wakati huo huo anawadanganya watanzania kuwa yeye hajauonapo na kwa manaana hiyo jamaa ni USELESS.

Date::10/29/2009 Hati ya Muungano Tanganyika,Zanzibar kuwekwa hadharani
Na Habel Chidawali, Dodoma Â
SERIKALI imesema mkutano ujao wa bunge itagawa kwa wabunge pamoja na kuweka katika maktaba mbalimbali pamoja na makumbusho Hati ya Muungano kwa kuwa ni haki ya kila mtu kuufahamu mkataba huo.

Aidha pamoja na kuweka katika maeneo hayo, bado hati hiyo itawekwa katika mtandao maalumu kumuwezesha kila Mtanzania kuiona na kuisoma kwa urahisi.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohamed Seif Khatibu aliwaambia wabunge jana kwamba hati ya Muungano ni nyaraka ya umma na kila raia ana uhuru na haki ya kuipata na kuitumia.

Khatibu alisema hati hiyo ni sehemu ya sheria za Muungano (The Act  of  Union) ya sheria nambari 22 ya mwaka 1964 na kwamba haki hiyo iliridhiwa na kupatikana na katika maktaba ya bunge pamoja na sheria namba 22 ya mwaka 1964.

Awali Mbunge wa Tumbe Salim Abdallah Khalfan (CUF) alitaka kujua hati ya mkataba wa Muungano “Article of Union” ni waraka muhimu wa historia ya nchi na akahoji ni kwa nini
waraka huo hauonekani wazi.

 Mbunge huyo pia alitaka kujua kujua ni pi nafasi ya kawaida kuweza kuupata na kuutumia waraka huo na kama serikali itakuwa tayari kuusambaza waraka huo kwa baraza la wawakilishi,wabunge pamoja na maeneo ya maktaba za vyuo na makumbusho ya Taifa.

Hata hivyo Waziri aliwataka wabunge kutumia nafasi hiyo kusoma vitu mbalimbali katika maktaba ya bunge kwa kuwa waraka huo upo tangu Februari 11, 2002 hivyo aliwataka wabunge wanaohitaji kujua waende katika maktaba yao kwa ajili ya kuusoma.
 
Edit title basi mkuu, ili wasije wakaanza ku-confirm bure kumbe ni typing error.
 
Back
Top Bottom