Hivi tuko Mwaka gani?

Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
13,157
10,655
Wanajamii;

nimeamka na kukuta kwenye news headline mambo ya Richmond, Dowans, EPA, BOT wtin tower, kipindupindu, kingunge bado mbuge, manji bado ni mwanachama wa nguvu CCM, rostam hajafungwa, kikwete napanda pipa tena.

zaidi ya hapo eti bado kwenye soka kuna timu mbili tu, yaani yanga na simba!!

huu ni mwaka gani??
 
halafu nimeona hakuna hata noti moja ina sura ya muungwana wakati ndio rais mwenye kupenda kuuza sura

hivi huu ni mwaka gani?
 
tanzania tuna uwezo wa ku carry over assignments, activities na hata shida zetu

tuliza moyo garang
 
Janjaweed,
Huu ni mwaka wa nzige... vuta subira oktoba si mbali sana panapo majaaliwa.

Annina
 
..................mwaka wa 50 wa katika kalenda kitangayika, na mwaka wa 47 katika kalenda ya kitanzania na ya kizanzibari; je utaka kujua tarehe, siku na saa?
 
Kweli tupo kwenye mwaka wa 50 katika kalenda ya kitanganyika na mwaka 45 kwa kalenda ya kitanzania lakini sasa yote hiyo unaminus na mwaka 95 utapata jibu tupo mwaka gani.
 
wanajamii;

nimeamka na kukuta kwenye news headline mambo ya richmond, dowans, epa, bot wtin tower, kipindupindu, kingunge bado mbuge, manji bado ni mwanachama wa nguvu ccm, rostam hajafungwa, kikwete napanda pipa tena.

Zaidi ya hapo eti bado kwenye soka kuna timu mbili tu, yaani yanga na simba!!

Huu ni mwaka gani??

1010 ad
 
Tuko kwenye mwaka wa njaa,Ufisadi,Ujambazi mwingi,Ulaji rushwa,Ukosefu wa maji safi mijini,Ukosefu wa Umeme Mijini,Ukosefu wa Kazi Mijini, Ukame,Maradhi,Kutokuwajibika kwa kazi tunazopewa na Wakubwa wetu wa kazi,Uvivu,na kutegemea Misaada kutoka nje ya nchi na Uongozi mmbaya na ya serikali yetu tukufu huo ndio mwaka tuliokuwepo kwa sasa Mkuu Janjaweed (MIAFRIKA BWANA NDIVYO ILIVYO)
 
Mwaka wa ombwe la uongozi

Mimi nimegundua kwamba tanzania ya awamu ya nne imebarikiwa na muumba kuwa na siku 1400 kwa mwaka mmoja, why?

  • maamuzi yanayohitaji mwezi kufanyiwa kazi yanachukua mwaka
  • kila kilichoanzishwa na huyu mkulu hakijakamilika --- ni kama ana mkosi vile
  • Tulianza na mbwembwe za MGD, AGOA, tukarithi MKURABITA na MKUKUTA sasa hivi naona ndio wanatengezeza framework za kumonitor
  • Kama sikosei, Mh. PInda aliapishwa wiki tatu zilizopita na bado hajahamia kwenye nyumba yake, ndio maana inakua vigumu kwa yeye kufanya maamuzi yoyote, si ajabu hata mali alizotangaza alitumia docments za 2004
  • Basi tukasikia michoro imekamilika na daraja letu pendwa la kigamboni linaanza kujengwa 2006, nina imani huo mwaka ukifika tu, tutaona ujenzi
Kinachonishangaza ni kwamba eti kuna watu humu jamvini bado wanadhani huu ni mwaka wa takrima, kanga, kofia na vilemba....

Janjaweed... Amka fungua macho ujue huu ni mwaka wa tabu!!
 
No... hapana bwana, hata Mkwawa hajazaliwa bado?? historia nzuri ya nchi hii imeanza kipindi cha akina Mkwawa! graph ikapanda mpaka Nyerere ikafika maximum, then baadae ikaanza kushuka kwa kasi; yaani kadiri miaka inayoenda mbele ndiyo tunapata rais bomu zaidi,

Huu ni ule mwaka wa neema kwa wengi (wapiga kura) na maafa kwa wachche (wagombea)

NI mwaka ambao hata John KOmba atapiga magoti kuomba vijana wampe kula
 
wanajamii;

nimeamka na kukuta kwenye news headline mambo ya richmond, dowans, epa, bot wtin tower, kipindupindu, kingunge bado mbuge, manji bado ni mwanachama wa nguvu ccm, rostam hajafungwa, kikwete napanda pipa tena.

Zaidi ya hapo eti bado kwenye soka kuna timu mbili tu, yaani yanga na simba!!

huu ni mwaka gani??
mwaka 2010
 
haiwezekani... nakumbuka JK alituahidi maisha bora na kasi ya ajabu kutatua matatizo, sasa kwanini imekua hivi?

Maisha bora!!! Mwenzetu ulikuwa wapi wakati mamilioni ya Kikwete yakigawiwa??? Hapo ndipo alikuwa anatimiza ahadi ya maisha bora kwa kila MTZ. Ahadi gani ambayo hajaitimiza na haitawezekana ndani ya miezi tisa iliyobaki?? Next question..................???
 
Back
Top Bottom