Naomba mwenye taarifa za ndani zaidi anifahamishe kwani sielewi mwenendo wa Kampuni Komgwe ya mawasiliano nchini (TTCL), nimesitushwa na kuona kwamba maeneo mengi yanayopata huduma ya simu za mezani kama Magomeni, Wageni, Osterdbay nk kwa hivi sasa hayana huduma hii. Mimi naishi Magomeni nilipofuatilia niliambiwa kuwa TeS sijui kitu gani haifanyi kazi,na nilipouliza itapona lini niliambiwa haijulikani na wala hakiponi ila wanabadilisha kwenda kwenye TeS nyingine na kwa sisi wateja wadogo simu zetu hazitaweza kupona, je suala hili ina maana walikuwa hawalijui? au TTCL wamefilisika kiungozi na Ufundi? Na kibaya zaidi tetesi nilizozipata nimeambiwa wafanyakazi walikuwa wanategemea kulipwa mshahara wa mwezi february leo 27/02/2012 lakini hata Salary Slip bado hazijatolewa. Mweye taarifa atufahamishe la sivyo je Hivi TTCL wamefilisika ??????