fredmlay
JF-Expert Member
- Apr 30, 2008
- 1,849
- 388
Wana jamvi habarini za leo.
Nilikuwa napitia financial report za kampuni ya TanzaniteOne (ambazo hazijakaguliwa bado) inayofanya shughuli za uchimbaji madini ya Tanzanite Mererani Simanjiro. Kuna mambo mengi hayajakaa vizuri ila nataka kuzungumzia moja tu.
Nimesahangazwa na kiasi kidogo cha mrahaba kilicholipwa serikalini huku kampuni ikionyesha kuzalisha kwa mwaka 2010 carats 2,200,000 sina hakika kama hii ni polished au rough maana hawajasema, lakini ndugu zangu kwa soko lilivyokuwa mwaka jana hapa Arusha, carat 1 ya polished Tanzanite ilikuwa ikiuzwa kati ya US $180 US $200
Kwa carats walizopata kwa mwaka huo, mathalani tuchukulie ni rough zikiwa polished wangepata carats 1,100,000 ambazo kwa bei ilivyokuwa hapa Arusha thamani yake ingekuwa US $198 mil US $220 mil
Kwa taratibu za serikali kupitia idara yao ya madini serikali ilipaswa kukusanya kiasi kisichopungua US $5.94mil badala ya US $0.4mil zilizokusanywa kulingana na hesabu zao (hii ni kama carat 2,200,000 zilikuwa rough na si polished) kwa mwaka kama kiasi walichokiri kuzalisha kitakuwa exported, hata hivyo kuna uhakika kwamba Tanzanite wanayozalisha huwa haibaki hapa nchini bali hupelekwa Africa Kusini kwa maandalizi ya kuiingiza katika soko la dunia, huko penye bei nzuri zaidi kuliko hizi hapa kwetu. Na pia ikumbukwe mrahaba kwa wafanyabiashara ya madini hulipwa hata kabla ya mauzo kufanyika ilimradi madini yametoka nchini.
Pia ieleweke kwamba mkataba wao wa kuwepo hapa nchini kiuwekezaji unakamilika mwaka 2012 na inaonekana wanajiandaa ku-lobby ili mkataba uongezwe ikiwa ni pamoja na kubadili jina la kampuni yao na kuwa Richland Resources Ltd
Kazi kwetu wadanganyika, tukomae na serikali ikiwezekana hao wanyonyaji waondoke watuachie madini yetu
Ukitaka kupitia hizo account waweza download