Hivi Tanzania tuna muziki?

bayonet

Member
Jan 7, 2011
43
0
Hivi karibuni japokuwa sikumbuki ni mwaka gani lilifanyika shindano kubwa tu nchini na likiwashindanisha wabunifu wote wa mavazi,LENGO likiwa ni kupata vazi la kitaifa...hilo halijawezekana mpaka sasa na sijui litawezekana lini.....likaja kichwani mwangu swali ambalo si tu huwa najiuliza mie bali watanzania wote,hivi jamani tukiichukua taarabu,bongoflava,takeu,dansi n.k..je,miziki ya namna hii ni YETU??tunapojadilim hebu tuzingatie vigezo hivi,asili,style za uchezaji,mavazi,lugha,mipigo(beats) na pengine zaidi ya yote,utengenezaji wake...........je,hizi na aina zingine ambazo sijataja ni aina za muziki ambao ukipigwa ugenini mtu atajua ni wa kitanzania???
 
Tanzania/Tanganyika hatuna identity ya muziki wetu kiasili,
 
asili ipo, mipigo kama ya ottu jazi, okestra makwiz, nyimbo flan walizokuwa wanaimba wazee wetu kama mtaa wa saba..midundo flan hivi unajua tu hii tanganyika,,,zanzibar, asili taarabu hiyo haina ubishi...
 
Mkuu hiyo kitu ipo sana tu, unajua hata wazaire magitaa na vinanda waliletewa na wakoloni tu, kinacho matter ni midundo au waweza sema ile ladha ya muziki ndio inayoweza kuutambulisha muziki.
 
Mziki wa kututambulisha kama Watanzania/ Watanganyika hamna, binafsi mm wa kunitambulisha kama Mkurya ninao. Naamini vivyo hivyo kwa Wasandawe, Chagga, Ngoni, Zaramo etc......
 
kwa makabila sina shida kabisa ndugu zangu,kila kabila lina muziki wake..lakini kama kongo inatambulishwa na bolingo,rhumba licha ya kuwa wana miziki ya kikabila,south africa wana kwaito,botswana nao wanao mfano culture spears na makhirikhiri,sisi kwanini jamani hatuna?eh?
 
Ndiyo, Tanzania tuna muziki. Tangu enzi za Salim Abdallah, Morogoro Jazz, Juma Kilaza, Mbarak Mwinshehe, Kiko Kids,
Tabora Jazz, Atomic Jazz, Simba wa Nyika, Juwata, etc. etc. tumekuwa na muziki ambao tunaweza kuuita Tanzania's modern dance music.
 
Ndiyo, Tanzania tuna muziki. Tangu enzi za Salim Abdallah, Morogoro Jazz, Juma Kilaza, Mbarak Mwinshehe, Kiko Kids,
Tabora Jazz, Atomic Jazz, Simba wa Nyika, Juwata, etc. etc. tumekuwa na muziki ambao tunaweza kuuita Tanzania's modern dance music.

ile mipigo haikuwa ya kizairwaa kweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom