Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
Ndio, Junk Food ni jina(lisilo rasmi) kwa vyakula ambavyo havina virutubisho vya muhimu kwa afya ya binadam,au kama vipo basi vinachanganywa na vitu ambavyo vina madhara katika afya ya mlaji. Haya na wewe unajua maana gani zaidi?
...kwa maana hiyo zile Burgers, coleslaw na fries hazina virutubisho muhimu mwilini? Kama unakubali vipo, preservatives gani unazojua wewe zinamadhara kwa binaadamu? acheni propaganda nyie... "Junk food" ni neno tu lilokaliwa kidedea kusisitiza umuhimu wa balanced diet, period!
Burger yenye salad na fries unaweza kulinganisha lishe yake na ubwabwa na maharage ya mama ntilie? acheni hizo bana...BTW, kule vijijini wanakula Organic products, kuanzia mapapai, matembele, mihogo na kisamvu chake nk, wala tusijilinganishe nao kwenye masuala ya mlo bora!
Mkuu, watalii wengi wanakuja kwetu ili waonje vitu tofauti. Ndio mana utawaona wengi wanakwenda sehemu kama Chef's Pride pale mjini n.k. Wewe unafikiri wanalipia ticketi za ndege ili waje kula McDonald's/KFC huku? By the way, wengi wanaofurahia hizo fast food joints huku "ulaya" ni wahamiaji, si wazawa!!!
...ooh, ok...
Kwa ufafanuzi mzuri, watalii wa aina hiyo wamo kwenye kundi la Drifters/Backpackers. Watalii wa aina hiyo wengi wao ni wanafunzi walio kwenye Gap years, nk. Watalii wa namna hiyo kule unguja huitwa 'vishuka'.
Vile vile watalii wa namna hiyo hujichanganya na wenyeji katika usafiri wa mabasi, treni nk. Si ajabu kupigana nao vikumbo kwa mama lishe...
Watalii hao huwezi kuwalinganisha na Business travellers, au waliomo kwenye package holidays, au expatriates...
Binafsi ningehitaji uthibitisho wa kina kuhusu hilo la immigrants kuwa walaji kwa asilimia kubwa kwenye hizo fast food joints