Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 701
Nimekuwa na kazi ya kusoma ripoti mbali mbali zilizoandikwa katika lugha ya Kiingereza. Kuna mambo mawili ambayo nimeyaona katika ripoti nyingi. La kwanza ni kutotumia alama za vituo kama coma, colons, semi-colons,nk. Mtu anaandika paragraph yenye mistari zaidi ya kumi lakini hakuna kituo hata kimoja. Baadhi hata full stop za mwisho wa sentensi hawaweki.
La pili ni kutojua kutumia umoja na wingi (singular and plural). Unakutana na vitu kama many house, 500 student, monies, we are implementing eight project, nk. Baadhi ya hizi ripoti zimeandikwa na watu wazito kwenye wizara za serikali na taasisi zingine.
Swali langu ni je, mambo ya punctuation na umoja na wingi siku hizi havifundishwi shuleni?