Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 9,482
- 14,352
wanajamvi naomba tujadiliane hili jambo, kwa muda mrefu nimekuwa nikijiuliza: hivi inakuaje sehemu ambapo maji ya mvua hutulia na baada ya muda hukauka kabisa na sehemu ile huwa kavu kabisa mpaka huwa panakua na mipasuko lakini baadaye mvua ikianza kunyesha mahali pale Samaki huwa wanatokea tena wakubwa kama Kambale na perege mpaka wakati mwingine raia huwa wanavua na kupata kitoweo..
maswali yangu...
1. hivi inakuaje sehemu ambayo ni kavu baada ya mvua kunyesha samaki huanza kutokea?
2. inawezekana hawa samaki huwa washuka wakati mvua inaponyesha?
3. au kuna mbegu ambazo huwa zinashushwa kutoka juu ambazo zikitua ardhini hurutubishwa halafu samaki hutokea?
vilevile: sio samaki hata vyura pia huwa wanatokea baada ya mvua kunyesha na maji kujaa kwenye madimbwi nao hutokea wapi?
naomba kujuzwa naamini kuna wataalamu waliobobea katika haya mambo.