Elections 2010 Hivi Ridhwani alitembeza fomu mikoa gani

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Kitendo cha Kikwete kutokabidhi chama chake fomu ya kutafuta wadhamini bado kimekuwa kikihojiwa na baadhi ya wana-CCM walioonekana kuudhiwa na hatua hiyo ya Rais Kikwete kuonesha kukosa imani na wanachama wengine, na kumwamini tu kija wake.

Lakini mbali ya hilo hadi leo hakuna mtu anayejua ni mikoa gani kijana wake aliweza kufika, wadadisi wa mambo wanasema isije ikawa baadhi ya majina yaliandikwa bila ridhaa ya wenyenayo na kuweza kuleta matatizo hapo mbeleni.

Je kuna mtu yeyote anaweza kutuambia ni mikoa ipi Ridhwani alifika.
 
Labda wameamua kutumia uzoefu na majina ya 2005. Mimi nilikuwa nasubiri kumwaga signature yangu hapa, hadi leo sijaziona.
 
Labda wameamua kutumia uzoefu na majina ya 2005. Mimi nilikuwa nasubiri kumwaga signature yangu hapa, hadi leo sijaziona.
Kuna namna hapa imefanyika NEC wanasemaje, mbona hatujaona akitembeza fomu kwa wazi kama wanavyofanya wagombea wengine, kama alijazia nyumbani Bagamoyo tuelezwe basi tujue maana atakuwa rais wa wote, Lissu na Marando wanamaoni gani sheria zinasemaje kwa hili.

Kuna gazeti moja liliandika kuwa wanachama fulani wanawazomea wanaCCM kwa kudhamini picha ya mtu na si mtu mwenyewe wakaenda mbali eti wanaCCM wameuziwa mbuzi kwenye gunia inawezekana kweli maana usiri mkubwa umetawala katika kujaza fomu.
 
Mpaka leo bado sijaelewa kwanini JK alifanya hivyo na Li-CCM likakubali..
Hata hivyo ya Ngoswe...
 
Back
Top Bottom