hivi nyie mumewaomba watoto wetu waje kwenye haraiki au waje muwagawie kofia na t-shirt za ccm??

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
wakuu kama mnavyojua sasa hivi ni maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya uhuru.hivyo wamechagua watoto wa shule za msingi mbao hivi sasa wanafanya mazoezi ya halaiki ili waje waonyeshe mgeni rasmi siku ya uhuru.

Lakini cha ajabu hawa watoto wamewagawia kofia na t-shirt za ccm rangi ya njano wawe wanavaa. Nimemwambia aivirudishe alipovitoa na ndo mwisho wa kwenda huko.

Watoto wetu wameenda kusoma si kufanya shughuli za chama.

wahusika msiwadhalilishe watoto wetu wao sio bango la ccm.

ujumbe umefika.

mia
 
eeeehhh ni kweli lakini. Tafadhali na wengine wenye watoto wanaokwenda huko fanyeni hivo.
 
Kweli mkuu ninakutana nao mara kwa mara hasa maeneo ya kurasini wamevalishwa t'shirt na kofia za chama cha jembe na nyundo! Hawawatendei haki hawa watoto
 
wakuu kama mnavyojua sasa hivi ni maandalizi ya sherehe za miaka 50 ya uhuru.hivyo wamechagua watoto wa shule za msingi mbao hivi sasa wanafanya mazoezi ya haraiki ili waje waonyeshe mgeni rasmi siku ya uhuru.lakini cha ajabu hawa watoto wamewagawia kofia na t-shirt za ccm rangi ya njano wawe wanavaa.mi nmemwambia aivirudishe alipovitoa na ndo mwisho wa kwenda huko.watoto wetu wameenda kusoma si kufanya shughuli za chama.wahusika msiwadhalilishe watoto wetu wao sio bango la ccm.ujumbe umefika.mia

Heeh kumbe wanasoma eeeh?! Au shule gani unaziongelea maana "kwa miaka hamsini hakuna lolote lililofanyika"
Mtoto wako "anaenda shule", naashum wewe ulienda pia. Nikukumbushe tu, bendera ya TAIFA ina rangi nne na siyo kama urembo zote zina maana.
Kama uliona manjano ukaona na kijani basi hiyo ni alama ya UTAIFA wala siyo CCM. Au una mzio na CCM?!
Najua ungependa kuona rangi nyekundu, bahati mbaya sana historia ya nchii haina mahusiano mazuri na maana inayobebwa na rangi hii.
Angalizo:
Usimpotoshe mtoto kwa makusudi halafu akijapata sifuri iwe "madudu ya Ccm".
Muache mwanao afaidi matunda ya uhuru hata kama wewe hukuitumia vizuri fursa hiyo...
 
bora ingekua alama ya taifa.je Tanzania inawakilishwa na jembe na nyundo na tshirt za chagua kikwete zinazofika miguuni?kwanini wasingewatafutia tshirt zenye kaulimbiu ya miaka 50 ya uhuru?hii nchi ya vyama vingi si vizuri mambo ya kitaifa kuyashirikisha mambo ya vyama.ndo maana viongozi wa siasa hawahudhulii sherehe za kitaifa kwa sababu zinageuzwa kua za chama.hii haifai hata kidogo.mia
 
halafu kinachosikitisha wanafanyia mazoezi kwenye viwanja vya polisi ndani ya polisi.na wale polisi wanaruhusu watu waingie na gari lao lenye makorokoro ya ccm.nashindwa kuwaelewa.mia
 
Back
Top Bottom