Hivi nyie kina dada mna nini?

sio wote wanaishi kwa kufuata bible , wengi tunaishi kwa kuiga western culture kwa hiyo mimi nadhani unachimba kwenye wrong source.
JE HUKO TULIKO HIGA HIZO PETE WANAMAANA GANI?

lakini pia kumbuka kwamba bible ina heshimu tamaduni zetu.

sina uhakika kwamba unakielewa unachokiongea!! Ndio maana sijibu lolote!!!
 
Mnazungumzia Biblia pekee, kwani kwenye Quran suala la pete ya ndoa halizungumziwi?

mimi nimeongelea Biblia kwa kuwa ndiyo kitabu changu cha imani nikijuacho, hivyo kama ww unajua kuhusu quran si useme? kwani umekatazwa??
 
kwanini uendelee kuishi maisha ya kudanganya watu. Ukumbuke unaweza danganya binadamu wenzio lakini Mungu hadanganywi. Ama kweli dhambi huzaa dhambi nyingine. Kusema uongo-uzinzi.
 
Duh wajameni! kama kuna wadada wanavaa pete za ndoa bila kuolewa sijajua bado. ni kutokujiamini maybe sababu kama anakwepa kuulizwa au mitongozo anaweza simamia msimamo wake na kuwajibu wanaomtongoza bila kuwa na pete, and by the way, mbona wake za watu wanatongozwa tu na pete zao?
 
Ngoja na mimi nianzishe yangu....HIVI KINA KAKA /BABA MNA NINI KUVUA PETE ZENU ZA NDOA????
 
Unaposema anajipotezea bahati ya kuolewa kwani anakua amekwambia anataka kuolewa??Unajuaje kama havai kwasababu hiyo hiyo kwamba hataki ndoa hivyo anavaa ili wamtambue kama mke /mchumba wa mtu??Au unajuaje kama havai ili awavutie wale wanaopenda wake za watu??Hapo anapata mahusiano yasiyo na ulikua wapi au kwanini simu unazima usiku!!Kabla hujajua kwanini mtu anafanya kitu ambacho sio uasi wa aina yoyote ile chunguza sababu kabla ya kumhukumu!
Shemej unaukataa ukweli?
 
Ngoja na mimi nianzishe yangu....HIVI KINA KAKA /BABA MNA NINI KUVUA PETE ZENU ZA NDOA????
Kweli kabisa anzisha lizzy nakuhakikishia page zaidi ya mia nne lol wanavua wanafikiri mademu ndio hawapendi waume za watu lol
 
Mi kwa mtazamo wangu sion kama ni vibaya kwan mwingine anaivaa akiwa na malengo yake lbd hataki kuwa na mwanaume hadi malengo yake yatakapotimia so sion ajabu
 
Mi kwa mtazamo wangu sion kama ni vibaya kwan mwingine anaivaa akiwa na malengo yake lbd hataki kuwa na mwanaume hadi malengo yake yatakapotimia so sion ajabu
Malengo gani ya kuvaa pete za ndoa? kwa nini asijiamini na kuwajibu wote wanaomsumbua kwamba hataki usumbufu, na nani kasema mwenye pete asumbuliwi? watu wamepinda balaa
 
Jamani inanishangaza, hii si mara ya kwanza kuliona na leo nimeamua kulivalia njuga. Jamani hebu liangalieni hili, utakuta mwanamke, mdada bado hakubahatika kuolewa na ukimfuatilia kwa undani utagundua ana kazi yake nzuuuuuuri tuu,ila hana cha boyfriend wala fiancee. Cha ajabu kila cku anajivalia pete ya ndoa tena ya gharama kubwa,tena wakati akitembea anaurusha ule mkono wenye pete kwa maringo makubwa ili kila apishanaye aione. Hivi hamuoni kama hii ni kutaka kujipotezea bahati ya kuolewa au? Au wana jf mnalizungumziaje hili?

Hujajua! Hao ni malaya ni kwamba huvaa pete za ndoa ili watongozwe kwa gia kubwa ufikiri umempata mke wa mtu.
Na wengi mkifika kunako chumba anakuambia nimeamua tu kukuheshimu wewe peke yako maana namheshimu sana mume wangu aliyeko masomoni au kikazi nje ya nchi au mkoa.
Ukiwa naye huwa hawataki mpira! Wanasema wana wleji nayo! Yamewakutawengi sana hayo. Take care
 
Kuepuka usumbufu. Unajua kuna baadhi ya wanaume wakiona mdada ana pete ya ndoa wanamwogopa na kumpa heshima kama mke wa mtu.
Kuna dada mmoja nilimuuliza akasema alikuwa anapata usumbufu mwingi kutoka kwa kinakaka na toka aamue kuvaa kapumzika usumbufu,nikamuuliza kwanini ? akadai hana muda wa mahusiano kwa sasa kamaliza masomo na kuanza kazi karibuni na anaweka maisha yake sawa na pia nyumbani kwao kuna shida inabidi asaidie kwa hiyo akili yake yote iko huko na baadae akijiweka sawa na familia pia ataivua.
 
Jamani inanishangaza, hii si mara ya kwanza kuliona na leo nimeamua kulivalia njuga. Jamani hebu liangalieni hili, utakuta mwanamke, mdada bado hakubahatika kuolewa na ukimfuatilia kwa undani utagundua ana kazi yake nzuuuuuuri tuu,ila hana cha boyfriend wala fiancee. Cha ajabu kila cku anajivalia pete ya ndoa tena ya gharama kubwa,tena wakati akitembea anaurusha ule mkono wenye pete kwa maringo makubwa ili kila apishanaye aione. Hivi hamuoni kama hii ni kutaka kujipotezea bahati ya kuolewa au? Au wana jf mnalizungumziaje hili?

Haikuhusu hii,we endelea na maisha yako
 
Ukiona kavaa pete ya ndoa na hajaolewa I think hivyo ni kukujulisha kuwa she's not interested in men/relationship
 
Wewe tafuta wengine kwani huyo tu ndio liyepo?Acha ushamba sio kila mtu wa kuoa.
 
Back
Top Bottom