LINCOLINMTZA
JF-Expert Member
- Mar 15, 2011
- 1,639
- 516
Dungu wanaJF,
Nimekuwa nikiwaza jinsi haya mataifa makubwa ya ulaya na Marekani yanavyoendesha siasa zake katika dunia hii.
Mataifa haya yanatumia njia mbalimbali ili kuweza kujipatia rasimali na nguvu za kiutawala kutoka mataifa mengine kwa njia mbalimbali kama za kijasusi au za kawaida. Na ninavyojua mimi, taifa kama Marekani limekuwa na nguvu na ujuzi mzuri sana wa kufanya kazi hiyo tangia karne ya 19 hadi sasa.
Baba wa Taifa, Mwl. J.K. Nyerere alikabiliana nao katika uongozi wake wote bila kuyumba na hasa ikizigantiwa kwamba kipindi chake hakukuwa na maendeleo ya mawasiliano kama sasa ambapo kwa sasa unaweza pata hata siri za Marekani kupitia WikiLeaks,na kwingineko
Swali, Je ni njia gani mwalimu alitumia, kwanza kuwaelewa hawa watu na pili kukabiliana nao kwa wakati huo wote?
Hii itasaidia vijana wetu wanojiandaa kuwa viongozi kuweza kuona mbinu hizo mapema kwani waliowengi hawana expose ya mambo kama hayo.
Naomba kuwakilisha wanaJF kwa heshima na utiifu.