Wazanzibar hatuutaki Muungano na Tanganyika

Kwa Wazanzibar walio wengi leo hii ni kuona kwamba Zanzibar kama Nchi inajitawala wenyewe huku ikiongoza tawala zake kama vile historia ya kweli unavyotufahamisha, jinsi ya utawala halali wa kIzanzibar kabla ya kuja mapinduzi ambayo yamepelekea athari kubwa miongoni mwa Jamii ya Wazanzibar hadi leo hii.

Huu sio wakati wa malumbano kwa Wazanzibar kwani siku zote mwenye macho haambiwii tazama wala mwenye masikio yake hahitaji kuhimizwa kusikia.Hii ndio nafasi pekee kwa Wazanzibar kushikamana na kuondoa tofauti zao kwani kinyume chake ni kuipoteza Zanzibar na vizazi vyake ambavyo hadi hivi leo vinahangaika bila kujua hatma yao.

Wakati umefika kwa Wazanzibar kuchukua hatua zinazohitajika ili kuionesha dunia kwamba na sisi Wazanzibar sio wanyama ni binaadam ambao haki zetu za msingi lazima ziheshimiwe. Mifano mingi tumeiona leo hii imetokea Duniani na mpaka sasa Wanaukombozi bado hawajarudi nyuma, wapo na wanaendelea kudai haki zao, licha ya damu inayoendelea kumwagika, lakini leo lao ni ukombozi kwa kile wanachokiamini.

Hatuna budi kuvishukuru vyama vya upinzani Zanzibar kwa kutoa muamsho na taswiira inayoonesha kwamba Wazanzibar wameporwa kile ambacho kilikuwa chao, wametoa msaada mkubwa hili hatuwezi kulikataa.

Wakati umefika kwa Wazanzibar kuachana na mawazo mapotofu kwa kusema kwamba tunategemea chama fulani ili kituletee maendeleo na ukombozi, au fulani ndie pekee atatuokoa, tuelewe kwamba na huyu fulani ni binaadam na yeye pia anahitaji tumsaidie kufikia lengo lake, tusilaumu tu kwani ukombozi wa Nchi si wake peke yake bali ni jukumu la kila Mzanzibar awe ndani au nje ya nchi mchango wake unahitajika na taifa.

Huu sio wakati tena wa kufikiria hayo, kwani kila kitu kina wakati wake, la msingi hivi ni kukaa chini kama Wazanzibar bila kujali huyu ni chama gani na anatoka wapi, bali uzanzibar uwe ndio mwega wa kulalia ukombozi wa mhimili wa nchi yetu kijikomboa kwa Madhalim na maadui zetu.

Ikiwa Wazanzibar tutakaa kimya kwa kufikiria kusubiri rasimu ya katiba au vyenginevyo, hilo nikusema kwamba Zanzibar imeshapotea na haitorudi tena kwenye mikono ya Wazanzibar abadan.

Njama za kuihujumu Zanzibar haikuanza jana wala leo, kwa wale wenye kujua na kufuatilia historia wataungana na mimi , kwamba tokea enzi za Mababu na Mabibi zetu mbinu na hila zilitumika kuiangamiza visiwa hivi mashughuri vya Zanzibar. Kwa vile Wazanzibar waliongozwa na dini yao pamoja na ukarimu wao hayo ndio yakawa chachu kwa Wazanzibar kutawaliwa hadi leo hii. Sasa basi mwiba unapoingia ndio unapotolewa wakati umefika kwa Wazanzibar kutumia dini yao kuikomboa nchi yetu.

Mimi nahisi kwamba kwa sisi vijana wa Kizanzibar ingelikuwa ni vyema kama tungekuwa tunapigania Nchi yetu na kuuwawa kwa hilo kuliko kufa kwa madawa ya kulevya, kwani pindipo Zanzibar ikijikomboa basi ni kusema matunda yake yatakuwa kwa umma wote wa Kizanzibar.

Nataka niweke wazi kwamba na iwe iwavyo na tufanye kila linalowezekena, Zanzibar haiwezi kupatikana kwa njia ya kidemokrasia abadani. Sina haja ya kulizungumzia hili kwani kila Mzanzibar anajua ni kitu gani kinachoendelea Zanzibar tokea kuasisiwa kwa vyama vingi.

Watanganyika wako tayari kupigana vita ikibidi iwe hivyo ili kuhakikisha kwamba Zanzibar siku zote inakuwa katika miliki yake na hilo ndilo lengo la Watanganyika. Mbinu nyingi zinatumika ili kuwaziba macho Wazanzibar bila wao wenyewe kujitambua kwamba hizo ni mbinu za Watanganyika kuendelea kuwatawala Wazanzibar. Watanganyika huwachukua mamluki wachache pale Zanzibar na kuwapa vyeo ili Wazanzibar waone hawa ni wenzetu, kumbe hatujui kwamba kile ni chambo tu kwani viongozi wale hawazimi wala hawawashi kule Tanganyika, wapo pale kutumiliwa kuingamiza Dola ya Kizanzibar tu.

Watanganyika wanatumia mbinu za kitoto kabisa kuidhibiti Zanzibar, kiasi ambacho ni aibu kwa Wazanzibar kutozitambua mbinu hizi. Iweje kila maamuzi makubwa ya Wazanzibar yafanywe na Watanganyika ? Hivi sisi Wazanzibar vichwa vyetu ni maji au ? Nasema wakati umefika kwa Vijana Wakizanzibar kuacha kupiga kelele ovyo bali tukae pamoja tuandae mbinu na mikakati ya kuikomboa Zanzibar yetu, kinyume chake itakuwa tunajidanganya wenyewe Watanganyika hawawezi kuitoa Zanzibar kwa bei yeyote isipokuwa kwa vita na mikakati maalum.

NB: Ni maoni yangu tu.
 

GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,432
3,006
Assalaam Alaaykum, Waungwana

Kwanza ninashirikiana na ndugu zetu katika kuombea duwa nafsi zetu na ndugu zetu waliomo kwenye mitihani ya siha, Sheikh Ali Baucha, Bi Salma, japo naye kwa sasa Alhamdulillah. Mwenyezi Mungu Mtukufu atujaalie sisi, wao na jamii ya Waumini siha na furaha na uwezo wa kutenda mema na kuepuka maovu, Aamyn. Jana tulijaaliwa kwenda kumzuri Sheikh Ali, Alhamdulillah anaendelea vyema; salamu zake ni kwa ndugu zetu wote katika ukumbi wetu huu. Tuzidi dua.

Pili, napenda nilete machache kukhusu yale niliojaaliwa kuyaona na kuyasikia katika vikao vya Mhishimiwa Samuel Sita, mjumbe wa Mhishimiwa Rais wa JMT kwa Wazanzibari.

Ujumbe wa Wazanzibari kwa Rais Jakaya Kikwete

Muungano Hatuukati! Muungano Hatuutaki!! Muungano Hatuutaki!!! Ni ujumbe aliopewa Mhishimiwa Sameul Sita kuufikisha kwa Mhishimiwa Rais wa JMT kutoka kwa Wazanzibari.

Ni Imani ya Wazanzibari juu ya Mhishimiwa Sita
Mhishimiwa Samuel Sita, alifika Zanzibar akiwa ni mgeni rasmi na wa hishima kwa Wazanzibari na kwa Zanzibar. Mhishimiwa Sita na tume yake walifika Zanzibar kumuwakilisha Rais Kikwete katika kutafuta maoni ya Wazanzibari kukhusu pendekezo la uwendeshaji mpango wa urekibishaji katiba ya Tanzania.

Mhishimiwa Sita alifanya vikao viwili, Bwawani na Haleisalasi. Wazanzibari wengi, wa vyama vya siasa, jumuia za dini, Waislamu na hata Wakiristo walihudhuria vikao hivi muhimu na kutoa maoni yao kwa uwazi na uhuru kaamili. Humalizi kuwataja wahishimiwa waliohudhuria vikao hivi na kutoa maoni yao. Maoni yote kwa jumla yalikuwa na ujumbe mmoja kwa Rais Kikwete.

Wazanzibari muungano (huu) hatuutakiâ. Tukitaja wachache waliohudhuria na kutoa maoni yao haya ni, mzee wetu Mhishimiwa Hassan Nassor Moyo, Profesa Abdulshariff, Mhishimiwa Hamza, Mhishimiwa Salim Bimani, Mhishimiwa Jamila Abeid, Mhishimiwa Edy Riami, Mhishimiwa Farid, na wengi wengineo.

Kwa jumla wote hawa na waliohudhuria walidhihirisha kutoridhia kwao kwa huu muungano, hivyo wakamuomba Mhishimiwa Sita afikishe ujumbe huu kwa Mhishimiwa Rais wa JMT. Mhishimiwa Sita aliahidi mbele ya umma uliohudhuria, kwamba ataufikisha ujumbe huu wa Wazanzibar kama anavyo upokea, bila ya kupunguza wala kuzidisha. Ni imani yetu kubwa juu ya uwaminifu wa ndugu yetu, Mhishimiwa Sita kwamba ameufikisha ujumbe kama alivyoahidi.

Kura ya Maoni Juu ya Muungano

Wazanzibari tangu sikumosi ya mavamizi na kumezwa nchi yao, Zanzibar; wamo katika kuwania kurejea Dola yao kama ilivyokuwa pale ilipopata uhuru wake na kujiunga na Umoja wa Mataifa, Disemba 10, 1963. Wazanzibari muda wote huu wakiwa katika juhudi hizi za ukombozi wa Dola yao, Zanzibar; kwa sauti kuu wakikanya, na wanakanya; mpango wowote ule wa 'kura ya maoni'.

Kama walivyo bainisha ndugu zetu, Virus 99 na Alkindy, kwamba kura ya maoni ndio turufu kuu na ya mwisho wanayoitayarisha watawala Tanganyika kwa kuhalalisha haya mavamizi yao ya 1964 na umezwaji wa Dola ya Zanzibar waliofanya April, 1964. Hadhari wanayoitoa ndugu zetu kuepuka âkura ya maoniâ ni muhimu sana. Wajibu wetu Wazanzibari tusimame qauli moja na hata kwa vitendo (vya amani) kukataa kata-kata mpango wowote ule wa kura ya maoni kukhusu suala la muungano. Nnanukulu hapa yaliobainishwa kwenye tamko la Chama Cha Jahazi Asilia kukhusu suala la kurejea Dola ya Zanzibar bila ya shuruti yoyote ile na kuepukana na kura ya maoni kukhusu suala hili.

"Chama Cha Jahazi Asilia kinadai kurejea Dola ya Zanzibar bila ya shuruti lolote. Chama Cha Jahazi Asilia, kinakataa kabisa mpango wowote ule wa kuleta kura ya maoni kuhusiana na suala la kurejea Dola ya Zanzibar; kwa sababu, kurejea Dola ya Zanzibar ni haki ya kimsingi ya Dola ya Zanzibar sawa na Dola yoyote ile ulimwenguni".

Maneno haya ya Chama Cha Jahazi Asilia ni maneno ya msingi na muhimu kabisa, juu yetu sisi Wazanzibari kuzidi kuyazingatia kila wakati na kuchukuwa kila hadhari.

Kura ya Maoni Ipigwe Kutokana na Daftari la Wapiga Kura

Hii kura ya maoni inayopangwa na watawala ni upotofu juu ya upotofu. Upotofu.

Kwanza, ilipovamiwa Zanzibar na kumezwa Dola ya Zanzibar, jee Wazanzibari waliulizwa na kupatikana ridhaa yao? Hawakuulizwa. Natusome maandishi ya Mzee wetu, Al Haj Aboud Jumbe, maandishi ya Mhishimiwa Dorado, na wengi wengineo; wote hawa walieleza wazi kabisa kwamba Wazanzibari hawakuulizwa juu ya huu wenyekuitwa muungano, kama wanautaka.

Pili, kura ya maoni kwa kutumia daftari la kudumu la wapiga kura!! Nani asiejuwa upungufu uliojaa katika daftari hili? Nani asiejuwa kuwa Wazanzibari wangapi wamenyimwa haqi zao na daftari hili? Nani asiejuwa wangapi waliokuwa si Wazanzibari wamepewa haqi na kuandikishwa kwenye daftari hii?

Tatu, kuleta kura ya maoni kumuuliza Mzanzibari kama anataka au hataki kurejea Dola yake ni dharau, bali ni tusi kwa Mzanzibari. Kufanya hivyo ni kuuliza uwezo wake wa kiakili. Nani mwenye akili timamu atakubali suala hili?

Muungano Hatuutaki!

Maoni ya Wazanzibari ni yale waliompa Mhishimiwa Samuel Sita, nayo ni âMuungano hatuutakiâ! Haya ndio yaliodhihirishwa na Wazanzibari na kufika kwa sauti moja kusisitiza hivyo.

Wa Billahi Tawfiiq
Farouk
Mei 26, 2011
 
Wazanzibari mnaiba tu mali za Tanganyika, hasa mliovuka maji kuja Bara.
Hamna ubavu hata siku moja ya kuvunja Muungano, ingekuwa furaha kama mngeweza tuonandokane na kundi la wahujumu uchumi wa Tanganyika, hebu tazama katika idara au wizara inayoshikiliwa na Mzanzibari Tanganyika ni unyama mtupu.
Mnadeka mpaka mwisho wa Dunia
 
Wazanzibari mnaiba tu mali za Tanganyika, hasa mliovuka maji kuja Bara.
Hamna ubavu hata siku moja ya kuvunja Muungano, ingekuwa furaha kama mngeweza tuonandokane na kundi la wahujumu uchumi wa Tanganyika, hebu tazama katika idara au wizara inayoshikiliwa na Mzanzibari Tanganyika ni unyama mtupu.
Mnadeka mpaka mwisho wa Dunia


Kama sisi hatuwezi, vunjeni nyinyi msilalamike na kama sisi.

Angalau sisi tunaoathirika tunaukataa lakini nyinyi mnafaidika na tena mnalalamika nini?

Oh Mawaziri, Oh umeme hamna mgao, Oh umeme hawalipi, Oh Wapemba wamejazana.

Mibaba mikubwa lakini mmejawa na woga.

Vunjeni mfe njaa kwa kuendekeza ufisadi.
 
Mtakao athirika ni nyinyi,sisi tumeshatamka muungano hatutaki ondoeni wanajeshi wenu hapa zanzibar,tumechoka kutawaliwa na muungano,Na hao wapemba watarudi tu kwao huku zanzibar na hawajafukuzwa etii,,mutaathirika nyinyi.

Hatutaki muungano tena,tumechoshwa na vikao vya kupeana posho kwa kutatua kero,kwani ni kero ? Ni haki yetu kudai yale ambayo yamo ndani ya muungo na sio kiro,mbona hamuelewi...........
Wazanzibari mnaiba tu mali za Tanganyika, hasa mliovuka maji kuja Bara.
Hamna ubavu hata siku moja ya kuvunja Muungano, ingekuwa furaha kama mngeweza tuonandokane na kundi la wahujumu uchumi wa Tanganyika, hebu tazama katika idara au wizara inayoshikiliwa na Mzanzibari Tanganyika ni unyama mtupu.
Mnadeka mpaka mwisho wa Dunia
 
nani atamfunga paka kengele? tunataka kiongozi wa serikali ya mapinduzi asimame na atamke kwamba hamuutaki muungano...
hapo tutaelewa ila kwa kelele za kwenye mablogu, mnazuga tu!!!
 
Mtakao athirika ni nyinyi,sisi tumeshatamka muungano hatutaki ondoeni wanajeshi wenu hapa zanzibar,tumechoka kutawaliwa na muungano,Na hao wapemba watarudi tu kwao huku zanzibar na hawajafukuzwa etii,,mutaathirika nyinyi.

Hatutaki muungano tena,tumechoshwa na vikao vya kupeana posho kwa kutatua kero,kwani ni kero ? Ni haki yetu kudai yale ambayo yamo ndani ya muungo na sio kiro,mbona hamuelewi...........

Tutaondoaje majeshi kwenye nchi yetu wandugu? Mbona mnakuwa vichwa maji hivyo? Tutaendelea kuweka majeshi ili kulinda nchi dhidi ya wenye kutaka kuisambaratisha nchi yetu, Tanzania! Nyinyi endeleeni kulilia kiti kwenye Umoja wa Mataifa alichokiacha Sultani wa Oman!
 
Mtakao athirika ni nyinyi,sisi tumeshatamka muungano hatutaki ondoeni wanajeshi wenu hapa zanzibar,tumechoka kutawaliwa na muungano,Na hao wapemba watarudi tu kwao huku zanzibar na hawajafukuzwa etii,,mutaathirika nyinyi.

Hatutaki muungano tena,tumechoshwa na vikao vya kupeana posho kwa kutatua kero,kwani ni kero ? Ni haki yetu kudai yale ambayo yamo ndani ya muungo na sio kiro,mbona hamuelewi...........

Mbona unadai eti "Wapemba watarudi kwao Zanzibar!" Kama kweli wanachukia Muungano kwa nini wasifungashe virago sasa hivi kimyakimya? Unafiki wote wa nini? Mbona mkipewa post bara hata isiyo ya Muungano mnaichangamkia kiulaini? Wonder shall never end!
 
Wazanzibari mnaiba tu mali za Tanganyika, hasa mliovuka maji kuja Bara.
Hamna ubavu hata siku moja ya kuvunja Muungano, ingekuwa furaha kama mngeweza tuonandokane na kundi la wahujumu uchumi wa Tanganyika, hebu tazama katika idara au wizara inayoshikiliwa na Mzanzibari Tanganyika ni unyama mtupu.
Mnadeka mpaka mwisho wa Dunia
kweli nyerere alikuwa clever! kwani amewaprogram watanganyika kuwa wajinga! kivipi? hebu jiangalieni mna resourses nyingi lakini hamjijuwi nini mnafanya. malizenu wazungu wanazichukuwa kama zao nyie mmelala na wala hamjui lini mtaamka kwa upofu wenu. watanganyika ni watu pekee barani africa wasio faidika na rasilimali zao. hebu angalia makampuni ya kigeni yanavyo kusanya jasholenu na kuwalisha wananchi wa kwao! hivi unajuwa ni kiasi gani unalipa kwa kumlisha muingereza mmoja akiwemo mzanzibar aishie kule? hivi unajuwa kiasi gani unamplipia mjapani kwao kwa dimond yako? hivi unajuwa hiyo text msg yako unayotuma kwa ule ujuha waliokuleteeni wazungu wa tuma ujumbe utajirike kuwa inawalipia wazungu kiasi gani kwao kwa huduza kilasiki kwao?
watanganyika mko ziro katika africa mmejaa madeni ya ilhali ni matajiri wa rasilimali. watanganyika mpaka leo mnasomeshana kwenye mabanda ya mbuzi ilhali ni matajiri mno wa rasilimali na eti mna wasomi wa ceconomics ! watanganyika hamjui kusoma mikataba na ndiyo maana wazungu wanakupateni hapo kwa u-sifuri wenu
watanganyika mmejaa ujinga ndiyo maana mnauwana kwa imani za ushirikina eti albino ukipata limbs zake utakuwa tajiri! munauwana na kuchunanan ngozi kwa imani mtakuwa matajiri! mara leo vita vya anchari na wanchoki kwa bangi tu! nyinyi watanganyika hadi leo mnajidai mmesoma wakati mmejaa ujinga munauwa vibaka na munawaabudu wezi wa mamilioni ya walipa kodi !
hebu juilize ile gesi ya songosongo nani anafaidika?
watanganyika mhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!
 
hawa wamesahau zile ndinga za washa washa! We waache walete ujinga wakati wanajua fika wao wenyewe ndo wameyataka kwa kujidai wahafidhina eti CCM! Haya mzimu wa ccm huo unawatafuna!
 
hawa wamesahau zile ndinga za washa washa! We waache walete ujinga wakati wanajua fika wao wenyewe ndo wameyataka kwa kujidai wahafidhina eti CCM! Haya mzimu wa ccm huo unawatafuna!


Unafikiri tunashangaa? Ufisadi umo ndani ya damu za watu na hizi harakati za maandamano ni kugombania ulaji tu. Kama kweli lengo la harakati hizi ni kuona kuondowa dhuluma basi mgeliungana na Wazanzibari kwa haki yao. Haki mnaitaka nyie lakini wenzenu wakiitaka mnacharuka. Unajuwa nyie uzandiki unawasumbua lakini ukweli ni ukweli na haki ni haki iko siku mtatambuwa kuwa unapodai haki basi uwe tayari kutowa haki.
 
Hawa wazenj waduanz kweli,wanadhan wakijtoa cc watanganyika 2tatetereka,wao ndo watakao umia as wenyewe ndo wana2tegemea sisi watanganyika 2pge mzigo tuwalishe na wao!wenyewe kutwa kazi kukaa kwenye vijiwe vya kahawa kupga umbea 2!jitoeni hata leo muone ka tanganyika itayumba kwa lolote.
 
Unafikiri tunashangaa? Ufisadi umo ndani ya damu za watu na hizi harakati za maandamano ni kugombania ulaji tu. Kama kweli lengo la harakati hizi ni kuona kuondowa dhuluma basi mgeliungana na Wazanzibari kwa haki yao. Haki mnaitaka nyie lakini wenzenu wakiitaka mnacharuka. Unajuwa nyie uzandiki unawasumbua lakini ukweli ni ukweli na haki ni haki iko siku mtatambuwa kuwa unapodai haki basi uwe tayari kutowa haki.
Hivi Tanganyika iliivamia Zanzibar? Huyo Karume wenu alikuwa amelala usingizi? Mimi nakereka sana na hizi kelele za kuonewa na Watanganyika. Ebu tuambieni faida kubwa tunayoipata kutoka Zanzibar? Huku bara vimejaa vi-Pemba chungu mzima na viduka vyao. Kila kiongozi wa juu wa Zanzibar ana bangalow huku bara. Chakula chenu kwa kiasi kikubwa kinatoka bara. Bila kusahau umeme wa bure. Mtoto akililia embe mpe umkate ....................... Tanganzeni kujitenga hata leo.
 
ni mtanganyika nitafurani sana kusikia muungano unavunjika manake hauna faida yoyote na watanganyika. sisi ndio tunaopoteza in terms of bajeti yetu inakwenda zanzibar na uchumi wetu unamiminikia zanzibar. tuvune muungano kwa faida ya watanganyika kama wazanzibar nao itawafaidisha basi sawa kabisa
 
Mkivunja muungano bara nafuu yetu. Maana tumewabeba kwa miaka zaidi ya arobaini na hambebeki, hamna kumbukumbu wala shukrani marhuni nyie. Mkivunja muungano mtapata wapi pa kuzalia hovyo kama inzi? Vunjeni hata leo mkome. Mkienda Kenya kwa wakola ndiyo mtajua sie waungwana ati. Vunjeni muone cha moto. Mtapinduana hadi jasho liwatoke. Angalieni Comoros pale. Nani anamhitaji mwenzake kati ya bara na zenj kama si zenj kupata pa kupatia japo mlo wa dezo na vyeo lukuki bila stahiki.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom