Hivi ni shukrani ya spika kwa mbunge kuchangia hoja?

TOWNSEND

JF-Expert Member
May 8, 2011
2,598
460
Nipeni mawazo yenu kwani kIla ninapoangalia bunge nakerwa na mambo mengi hasa hili la mbunge hasa wa ccm wanapopewa nafasi ya kuchangia huanza na neno nakushukuru spika kwa kuniona au kuniruhusu na mimi nichangie hivi ni kweli mpaka huruma ya spika? au ni wajibu wake kihalali?
...au naomba waziri anisaidie kijijini kwangu hakuna umeme je ni haki kusema unamuomba waziri au ni wajibu wa waziri kutekeleza bila sharti lakuombwa?
 
Tumefundishwa kuomba kila kitu hata ukiwa na pesa ukienda dukani unaomba wakati hapo ni pesa yako. Sisi hatujui kudai haki zetu ila tunajua kuomba na hatuzipati kwa sababu ombi laweza kataliwa.
 
I hope na mimi leo ntapata majibu juu ya hili

Nyongeza; Kuwashukuru wake na watoto wao humo bungeni pia ningependa kupata muongozo
 
Si hilo tu,wabunge wetu huwa wanashukuru hata maswali yao yanapojibiwa na mawaziri!
 
Napenda kumshukuru mtoa mada, nawashukuru wale wote waliochangia, na nakushukuruni kwa kunishukuru
 
Ndio maana hata haki zetu tunaomba badala ya kuitaka.

Kuomba kuna NDIYO na HAPANA

Kutaka ni HAKI yako na lazima upewe
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom