Hivi ni sawa mbunge wa Tabora kupigania maslahi ya Simba SC kuliko wanatabora?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,182
3,547
Kwakweli kwa tunaotoka mkoa Tabora,hali ya kimaisha huku imekuwa ngumuu sana.Mbunge wetu wa Tabora Mjini mheshimiwa Rage.

Kila nikiaangaliaa taarifa ya habari bungeni na magazeti,kila nikimwona naona anaongelea maswala ya Simba na akitetea maslahi ya Simba mara mpira pesa,yaani simuelewii kwa kweli muda mwingi yupo Dar.

Mbona jamani anasahau shida za wana Tabora mpaka hii leo barabara ya kwenda Tabora Mjini mpaka Urambo ni mbovu,shida ya maji,umeme hapa Tabora anasahau uwanja wa ndege wa Tabora mjini umeshakufa hata siku hizi hazitui.

Uwanja wa ndege hadi kule Uramba pia umekufa, barabara ya Changarawe huku mpaka lini.

Hivi kuna umuhimu 2015 huyu jamaa tumrudishe tena bungeni.
 
ndiyo maana UKAWA wanataka katiba ijayo viongozi wabovu kama hawa wavuliwe nyadhifa zao hata kabla ya kumalizia kipindi chao cha miaka mitano ya uwakilishi bungeni!!!


Rage anafanya haya kwa sababu katiba mbovu iliyopo inampa huo mwanya, hakuna wa kumuwajibisha.
 
kwa kweli kwa tunaotoka mkoa tabora....hali ya kimaisha huku imekuwa ngumuu sana...mbunge wetu wa tabora mjini muheshimiwa rage....kila nikiaangaliaa taarifa ya habali,bungeni na magazeti....kila nikimwonaa naona anaongelea maswala ya simba....akitetea masialai ya simba mara mpira pesa...yaani simuelewii kwa kweli muda mwingi yupo dar......

Mbona jamani anasahau shida za wana tabora....mpaka hii leo barabara ya kwenda tabora mjini mpaka urambo ni mbovu...,shida ya maji,umeme hapa tabora anasahau uwanja wa ndege wa tabora mjini umeshakufa hata siku hizi hazitui, uwanja wa ndege hadi kule uramba pia umekufa, barabara ya changarawe huku mpaka lini...

Hivi kuna umuhimu 2015....huyu jamaa tumrudishe tena bungeni.......



yani wewe ni zuzu kweli, unauliza kumrudisha tena bungeni wakati hata hiyo kumchaguwa kipindi kimoja wote mliomchaguwa wapuuzi watupu.
 
Kwani wakati mnachagua hamkufahamu kwamba ni M/Kiti wa Simba SC? Kama ameshindwa hata kuisaidia Rhino Rangers isishuke daraja ni kwa vipi uote hayo mambo makubwa ya barabara, maji, elimu . Mchawi wa Wana Tabora sio Rage ni Wana Tabora wenyewe. JITAMBUENI
 
Back
Top Bottom