Hivi ni sahihi serikali kubadilisha maamuzi ya bunge?

Chatumkali

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,037
458
Katika gazeti la MwanaHalisi la jumatano Desemba 21 imeripotiwa kwamba serikali imebadilisha maamuzi ya bunge lililoidhinisha mapato na matumizi yake juni mwaka huu kwa kuagiza ajira zote serikalini katika mwaka wa fedha 2011/2012 zipunguzwe kwa asilimia 50.Vilevile upandishwaji vyeo upunguzwe kwa kiwango kilekile.Imedaiwa kwamba hii ni kutokana na serikali kutokuwa na uwezo wa kifedha kutekeleza bajeti iliyopitishwa na bunge.
KAMA NI KWELI:
1.Ni sahihi kwa serikali kubadilisha maamuzi ya bunge ambayo kimsingi ni maamuzi ya wananchi?
2.Kama si sahihi,jeuri hiyo serikali imepata wapi?
3.Kama si sahihi,ukuu wa bunge letu uko wapi ikiwa maamuzi yake yanabadilishwa kwa mtindo huo?Na je bunge linahaki ya kuendelea kuwa na imani na serikali?Na je hii haiwezi kuwa dharau kwa bunge?Kama si sahihi,nini hukumu kwa serikali ambayo inabadilisha maamuzi ya bunge?
LAKINI:Kama ni sahihi basi mimi sina neno kwa hilo.
 
Bunge liunde kamati teule ya kuchunguza habari hiyo! Hivi kama bunge lilipitisha budget kwamba serikali ikusanye kwa.mfano bilioni 200 na kutumia kiasi sawa na hicho lkn serikali ikakusanya chini ya hapo (kwa sababu wanazozijua) itakuwaje sasa? Serikali itaendelea kutumia bil. 200 wakati imekusanya bilioni 120?
 
Mkuu tume tena? Hiyo pesa watakayotumia ku probe bora iende kuwapa watu ajira.

Watakapokutana kwenye kamati zao za bunge ndipo wahoji kwanini serikali imepunguza idadi ya ajira zilizoahidiwa?
 
Mkuu tume tena? Hiyo pesa watakayotumia ku probe bora iende kuwapa watu ajira.

Watakapokutana kwenye kamati zao za bunge ndipo wahoji kwanini serikali imepunguza idadi ya ajira zilizoahidiwa?
Mkuu hujui kwamba siku hizi Bunge linaendeshwa kwa kamati teule. Anyway yote heri tu ilimradi tupate majawabu ya nini kinatokea kwenye bajeti iliyopitishwa ambayo inaonekana haitekelezeki! Sasa na haya mafuriko si ndio hatari manake hizo pesa za emergency siamini kama zilikuwepo kwenye bajeti!
 
Hizi fedha za dharula za kuwasaidia waliopatwa na mafuriko zitaliwa na Lukuvi na genge lake; huyu jamaa ndio zake hizo kwani aliishakomba fedha za mabasi ya vijana huko nyuma!! Akisikia kuna maafa anajua wamemtengenezea ulaji.
 
Kamati teule sasahivi hatuhizitaji, labda hadi hapo bunge litakapothibitisha kwamba linao uwezo wa kufuatilia na kusimamia maamuzi yake.

Kuendelea kuunda kamati teule kwa mambo ambayo hayahitaji tume ni ufujaji wa fedha za umma na haikubaliki.
 
Mkuu afadhali umeliona hilo. Tatizo sisi Wtz huwa hatufuatilii mambo, kamati inaundwa inatumia pesa lukuki lakini inaishia kupendekeza mapendekezo ambayo hayafanyiwi kazi. Mkuu nasikia ukiingia kwenye Kamati Teule ya Bunge basi unakuwa umeukemea umasikini sijui kama kuna ukweli ama la. Inabidi Bunge japo lituambie Kamati Teule ya Jairo imetumia kiasi gani. Hiyo ndigo accountability to the public for the public funds spent.
 
Hizi fedha za dharula za kuwasaidia waliopatwa na mafuriko zitaliwa na Lukuvi na genge lake; huyu jamaa ndio zake hizo kwani aliishakomba fedha za mabasi ya vijana huko nyuma!! Akisikia kuna maafa anajua wamemtengenezea ulaji.

Kumbe mh. Lukuvi alikuwepo wakati huo, mimi namkumbuka mtu mmoja anaitwa John John Guninita wakati huo akiwa Mwenyekiti wa UVCCM. Baadaye akatimkia CDM kabla ya kurudi tena CCM na kukwaa uenyekiti wa CCM mkoa wa Dar
 
Kumbe source ya taarifa hii ni gazeti, hii ilifaa kuwa tetesi vinginevyo tuletee ushahidi zaidi wa suala hili.
 
Itabidi serikali ielezee sababu ya kufanya hivyo ndani ya bunge na wabunge wajadili wakikubali maelezo ya serikali basi hamna la ziada ni kujadili ajenda nyingine.
 
Kumbe source ya taarifa hii ni gazeti, hii ilifaa kuwa tetesi vinginevyo tuletee ushahidi zaidi wa suala hili.

Mkuu hili si gazeti la udaku!Bado tunaamini kwamba hili ni gazeti makini.Limenikuu waraka wa ikulu wa tarehe 18 novemba 2011 wenye kumb,Na BC.97/109/014/15.
 
Mi ninavyoelewa Bunge linaisimamia serikali ktk kila jambo na serikali kazi yake kutekeleza maamuzi ya Bunge lkn kwa sababu Bunge kujifanya sehemu ya serikali ndio hcho kinacho tokea ssa.Kwa ssa Bunge na Mahakama wana buruzwa na serikali hakuna cha Mgawanyo wa madaraka wala Utawala wa sheria.
 
Kwa Tanzania sishangai kuona serikali inapindisha maamuzi ya bunge maana hii ndo democracy iliyojengwa na CCM kuhakikisha bunge halina nguvu zaidi ya serikali. Kwa mfano maamuzi yaliyopitishwa na bunge kua kina Jairo na wenzake wajiuzuru yalitakiwa yatekelezwe pale pale na serikali lakini tulichoona ni kinyume chake eti ngoja tumsikilize mkuu wa kaya nae amekaa kimya hadi sasa. Hii inamaana kua tutaongea, tutazijua na kuzikariri sheria na vifungu vyake juu ya nguvu ya bunge juu ya serikali kama chombo kikuu kinachosimamia shughuri za serikali but zitabakia kwenye vitabu na majarada na midomoni mwetu pasipo utendaji kitu ambacho kinaifanya demokrasia yetu kua na mapungufu mengi sana. Mabadiliko ni muhimu nchini mwetu.
 
Kwa hili linaloendelea kujitokeza ni jambo ambalo si zuri, yaani hapa ni mvutano kati ya serikali na bunge, ikiwa hii ni kati mihimili mitatu ya dola, ikiwa ni SERIKALI, BUNGE na MAHAKAMA,
Huu ni mgongano mkubwa sana wa kiutendaji, tulitegemea kuona ushirikiano mzuri katika mihimili hii ya nchi, kinachoamriwa na BUNGE, ni lazima kikubalike na SERIKALI.
Hali kama hii tutegemee nini wananchi ??
 
Inachekesha kwa nchi yenye utendaji kama TZ tukisema tunafuata misingi ya Democracy wakati kiutendaji hilo swala halipo kabisa. Si sahihi hata kidogo Serilali kuingilia maamuzi na kushindwa ketekeleza yale yote ambayo bunge lanaishauri au kuitaka serikali kutekeleza. Cha msingi ni kuutoa huu udharimu unaofanywa kwa kukitoa chama tawala madarakani na kukisimamisha chama kitakachofuata misingi nma kanuni za Democracy kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom