Hivi ni nani mshauri wa Rais Kikwete?

Jamani, rais wetu hana washauri, ana washika ofisi na waganga wa kienyeji... period!!!!
 
nchi yetu hatuwezi kusema rais ana washauri kwa jinsi inavyoendeshwa, yaani ipo kama maamuzi yote yanatoka kwa rais moja kwa moja bila kpitia kwa washauri

Urais wa nchi ni taasisi, hivyo maamuzi ya Rais husika huwa ni matokeo ya mchakato mrefu unaochambuliwa kimfumo na washauri wake ndani na nje ya Ikulu. Hivyo, kwa mazingira haya ambayo mpendwa wetu kaandika kwa ustadi na umakini kabisa, ni alama/ishara ya kuanguka kwa utendaji wa taasisi hii muhimu ndani ya nchi yetu.

Najua Ikulu kuna wataalamu wa kila fani, kwa lengo tu la kurahisisha maamuzi ya mkuu huyu wa nchi kuhusiana na jambo fulani hasa lenye maslahi ya nchi. Sasa kama wataalamu hawa wanaweza kutoa ushauri kwa mtu asiyejari ushauri au mbishi na mbabe; basi mwotisha wa wao kumshauri hukoma na kubaki na fikra za kudumaa tu. Matokeo yake ni kuporomoka kwa kila kitu ambacho Rais anawajibika moja kwa moja au si moja kwa moja maana yote atakuwa anayafanya yeye pekee labda kwa kushauriwa na mke wake na mtu kama Makamba (tumeona mfano Makamba alivyosema kuwa yuko tayari kufa kwa kumtetea mkuu wake na siyo kuwa tayari kumtetea mkuu kwa masuala tu yanayohusu masilahi ya umma bali ni chama CCM tena kundi fulani)!

Naogopa zaidi sasa hivi maana kwa mazingira haya ndani ya nchi yetu, hata huko kuirudisha nyuma hali ya kutoaminiana ili mambo yaende vizuri tena kwenye Taasisi hii itakuwa ngumu. Sababu ni kwamba, katika makundi yote yaliyotaja (ambayo ni ukweli tupu) hakuna hata moja ambalo mkuu wa nchi yetu analiamini kwa asilimia 100. Wasiwasi umekua kwa kiasi cha hali ya juu sana na chanzo ni makundi mbalimbali yenye mtazamo tofauti kulingana na maslahi (wengine maslahi binafsi na wengine maslahi ya umma). Kundi lenye nguvu liko upande wa maslahi ya binafsi na ndilo linaloyumbisha nchi hii. Limefanya wataalamu wakawa tena siyo washauri maana ushauri wao kama hauna maslahi na kundi hilo basi mkuu wa nchi hawezi kuwasikiliza maana hayuko tayari kupingana nalo hata kidogo.

Ndiyo maana washauri wengine siku chache zilizopita walishauri mkuu huyu wa nchi awe mbogo (afanye ushauri wa wendawazimu kwa maslahi ya umma) ili kuinusuru nchi na huko inakozama ndani ya shimo refu kiasi cha kuja kushindwa kuipoa itakapofika chini ya kina.

Rais wetu, yaone haya mapema kabla hatujachelewa sana na kuamka ili kuinusuru nchi na watu wake kutoka kwenye hatari hii ya hiari!!
 
Kutokana na maandishi huyu msomaji mzuri wa Raia mwema, Rais ayasome na ajipime mwenyewe!
 
Ni nadra ukikutana na Mmarekani, Mwingereza au Mjapani utamsikia akimlaani na kumlaumu kiongozi wake. Nchi yoyote iliyo huru kiongozi Mkuu wa nchi ni kioo cha utaifa wao na uhuru wao. Rais wetu ni kioo chetu cha uhuru wetu na utaifa wetu.

Imejengeka tabia ya kulaumu viongozi wetu bila kuuelewa mfumo mzima wa kikatiba na sheria uliopo hapa Tanzania. Lalamika lalamika ni moja ya mapungufu yetu sisi watanzania. Tunawachagua viongozi ili tuwalaumu. Sasa wasomi au watanzania wenye uelewa wanapolalamika bila ya kuchukua muda kidogo tu na kuisoma Katiba na mfumo wa kimaamuzi basi inakuwa ni hatari kubwa kwa demokrasia yetu. Ni hatari kwa sababu wananchi wa kawaida wanaweza kudanganyika na lawama zisizo na msingi wowote ule.

Mfumo wa kimaamuzi uliopo hapa Tanzania umegawa maamuzi mengi sana kwa vyombo, taasisi na viongozi mbali mbali. Tunazo wizara, idara zinazojitegemea (DPP, TAKUKURU), mawaziri na makatibu wakuu ambao wamepewa uhuru mkubwa wa kisheria wa kufikia maamuzi bila ya kuingiliwa na Rais. Tunazo EWURA, SUMATRA, TFDA, DAWASCO, TANESCO na kadhalika ambao wana uwezo na uhuru wa kisheria kufikia maamuzi makubwa sana bila ya kuingiliwa na Rais.
 
Pumba nyingine huwa zinatia kichefuchefu.
 
Ni nadra ukikutana na Mmarekani, Mwingereza au Mjapani utamsikia akimlaani na kumlaumu kiongozi wake. Nchi yoyote iliyo huru kiongozi Mkuu wa nchi ni kioo cha utaifa wao na uhuru wao. Rais wetu ni kioo chetu cha uhuru wetu na utaifa wetu.
You MUST be kidding!

Hebu kuwa serious kidogo tu mkuu... Kidogo tu mkuu wangu. Mataifa yote uloandika hapo juu wenzio ndipo aidha tunaishi, au tunafanya kazi au wenzio tumeshaamua kuchukua uraia wake na kuukana uraia wa Tz kabisa. Tunachokijua ni tofauti na ulichoandika!
 
Ni nadra ukikutana na Mmarekani, Mwingereza au Mjapani utamsikia akimlaani na kumlaumu kiongozi wake.

katika dunia hiii hii au?....mbona viongozi wao wanapigwa "mawe" kila kukicha.......wee unaishi Mars nini?

Nchi yoyote iliyo huru kiongozi Mkuu wa nchi ni kioo cha utaifa wao na uhuru wao. Rais wetu ni kioo chetu cha uhuru wetu na utaifa wetu.

Kwa hiyo tuendelee kuwa mabendera kufuata upepo eehh?

Imejengeka tabia ya kulaumu viongozi wetu bila kuuelewa mfumo mzima wa kikatiba na sheria uliopo hapa Tanzania. Lalamika lalamika ni moja ya mapungufu yetu sisi watanzania. Tunawachagua viongozi ili tuwalaumu. Sasa wasomi au watanzania wenye uelewa wanapolalamika bila ya kuchukua muda kidogo tu na kuisoma Katiba na mfumo wa kimaamuzi basi inakuwa ni hatari kubwa kwa demokrasia yetu. Ni hatari kwa sababu wananchi wa kawaida wanaweza kudanganyika na lawama zisizo na msingi wowote ule.

Kwa hiyo wakituibia, wakitudanganya na wakitufisadi kwenye mikataba ya hovyohovyo sisi tuwachekee tuu.....

Mfumo wa kimaamuzi uliopo hapa Tanzania umegawa maamuzi mengi sana kwa vyombo, taasisi na viongozi mbali mbali. Tunazo wizara, idara zinazojitegemea (DPP, TAKUKURU), mawaziri na makatibu wakuu ambao wamepewa uhuru mkubwa wa kisheria wa kufikia maamuzi bila ya kuingiliwa na Rais. Tunazo EWURA, SUMATRA, TFDA, DAWASCO, TANESCO na kadhalika ambao wana uwezo na uhuru wa kisheria kufikia maamuzi makubwa sana bila ya kuingiliwa na Rais.

unaishi wapi mwenzetu.....dunia hii hii au?.....hivi Richmond, Buzwagi, Kagoda, EPA....na wizi wa Mafuta unaoendelea....si viko chini ya watu hao hao!!........

usifikiri tulio hapa tunaojadili mustakabali wa Taifa letu ni kama wewe bendera fuata upepo
 
Hali inatisha! Swali ni je tufanye nini sasa? Umefika wakati tutoe ushauri kufahamu na kukakaa kimya hakutatusaidia chochote. Ni kwa kutumia akili na utashi wetu tutafakari jinsi ya kutoka huku shimoni. Haiwezekani watu na akili zetu tukae tu chomboni wakati tunaona kwamba kinazama.
 
Ni nadra ukikutana na Mmarekani, Mwingereza au Mjapani utamsikia akimlaani na kumlaumu kiongozi wake. ...

haya yanasemwa na mtu mwenye access na internet sasa kule kwetu ambako bado tunatumia karabai watasema nini! nachoka kabisa
 
https://www.jamiiforums.com/members/teroburu.html
Ni nadra ukikutana na Mmarekani, Mwingereza au Mjapani utamsikia akimlaani na kumlaumu kiongozi wake. Nchi yoyote iliyo huru kiongozi Mkuu wa nchi ni kioo cha utaifa wao na uhuru wao. Rais wetu ni kioo chetu cha uhuru wetu na utaifa wetu.

Imejengeka tabia ya kulaumu viongozi wetu bila kuuelewa mfumo mzima wa kikatiba na sheria uliopo hapa Tanzania. Lalamika lalamika ni moja ya mapungufu yetu sisi watanzania. Tunawachagua viongozi ili tuwalaumu. Sasa wasomi au watanzania wenye uelewa wanapolalamika bila ya kuchukua muda kidogo tu na kuisoma Katiba na mfumo wa kimaamuzi basi inakuwa ni hatari kubwa kwa demokrasia yetu. Ni hatari kwa sababu wananchi wa kawaida wanaweza kudanganyika na lawama zisizo na msingi wowote ule.

Mfumo wa kimaamuzi uliopo hapa Tanzania umegawa maamuzi mengi sana kwa vyombo, taasisi na viongozi mbali mbali. Tunazo wizara, idara zinazojitegemea (DPP, TAKUKURU), mawaziri na makatibu wakuu ambao wamepewa uhuru mkubwa wa kisheria wa kufikia maamuzi bila ya kuingiliwa na Rais. Tunazo EWURA, SUMATRA, TFDA, DAWASCO, TANESCO na kadhalika ambao wana uwezo na uhuru wa kisheria kufikia maamuzi makubwa sana bila ya kuingiliwa na Rais.

Duh! Tumuombee huyu jamaa. Au ni walewale?

Obama analaumiwa na kukosolewa vikali ndani ya Marekani.
UK Gordon Brown yuko maji ya shingo kwa lawama na shutuma.
Japan na Italia ndio usiseme. Serikali karibu kila mwaka Serikali inaanguka na kuundwa nyingine.

Hao wote wanalaumiwa kwa POLICIES zao na DECISIONS zao. Ni kazi yao kujitetea na kuzipangua.

Hili la JK kuongea Too much ni kweli kabisa,jamaa ni Mr.know much kiaina.yani kila kitua anataka kuonekana yeye ndie mjuaji.hata kama hana mamlaka na ujuzi wa kuvisemea vitu hivyo.

Aliniacha hoi alipoenda kufungua mkonga,badala ya yeye kusikiliza wataalam wa Mawasiliano wamuelezee yeye pamoja na wananchi wake faida za Mkonga,jamaa akachukua Center Stage kuelezea kwa wananchi kazi za mkonga,jinsi ulivyoletwa Tanzania,na matumizi yake as if the JK ni mfanyakazi wa kampuni ya Mkonga,kumbe ni President wa Nchi.too low sometimes.

Mh.Rais needs to lay low sometimes,and listen!
 
Rais alichofanya kila mtu anakiona, kama hukioni basi pengine hutaki kuona.

Kusafiri sana, + shopping spree, kutokusolve matatizo ya ndani kwa dhati etc. kwa mtindo huo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom