Hivi ni Mbowe au CHADEMA???

wewe sajenti wa nyumbani kwako...
Tatizo sio Mbowe...Ni sisi em... Tanzania imejaza vichwa BUPU kama wewe.....WakeUp!!!!!

.....Hapo mkurugenzi umenena,,,,tatizo ni sisi watanzania,
na mabadiliko tutayaleta sisi tukiachana na tabia ya unafiki
kama ya huyo jamaa!
 
Hujaelewa na Tatizo sio Mbowe kwani ni msimamo wa chama.Na mwenyekiti wa chamandivyo anatakiwa awe ,asiwe mtu wa kununulika kirahisi.Nawapongeza CDM kwa maamuzi magumu.Lakini la msingi la kujiuliza ni kwa nini hiyo tafsiri ya neno kambi rasmi linatolewa sasa hivi?

Jibu:

ni kwa sababu CCM wameshakiri kwamba Chadema ni Tishio na kwamba watawakataje makali ni kwa wanachokifanya sasa wakishirikiana na wapinzani ambao wananunulika.Wanaona kabisa kwamba wakiacha kanuni zibaki zilivyo zinaweza kufanya kamati kama ya PAC ( Public Accounting Commettee ) kuangukia mikononi mwa mtu kama Lissu na akawavua nguo serikali kama Slaa alivyowavua kwamba chai za maofisini tu ni mabilioni ya pesa.Hapa ndio ambapo Chadema wanahisi kuonewa.
 
Ni kipindi cha kuona rangi za wahusika tuombe salama Mungu ajalie wenye makosa wayaone makosa yao ili tuweze kufika kule tunakotaka kufika.
 
Sajenti naona unalichukulia hili suala juu juu...Kiuhalisia CCM wanajua vyema uwezo wa kiakili, kifikra na kiuongozi ambao wabunge wa CHADEMA wanao na ndio maana wanaunga mkono mapendekezo ya Hamad na Kafulila...hilo ni moja...
na pili CCM wana-play political game kwa kupitia mgongo wa CUF na vyama vingine vya upinzani, waliwapa kina Zitto, Slaa na Cheyo uenyeviti wa kamati ktk bunge lililopita wakijua kua mpinzani wao mkubwa bungeni ni CUF kwa wakati huo, bahati mbaya nafasi walizowapa zikawageuka na kuwashikisha adabu ktk ufuatiliaji wa mambo ndani ya kamati husika. leo wanajua CHADEMA ni nani na wanafanya vile vile..bahati mbaya ni kwetu sisi wananchi..si kweli CUF itaweza hata kidogo kuikosoa serikali ambayo katibu mkuu wake ni part ya serikali husika
Kiuhalisia tumepoteza uwakilishi wa muhimu sana katika kamati husika lakini wananchi wanajua vyema kua Upinzani bara ni CHADEMA pekee....

Siku zote tutawaunga mkono....

Umenena Mkuu. Kama una namba ya TiGO nipatie ili nikupunguzie salio.
 
Mimi naliona jambo hili kuja kwa wakati ambao sio mwafaka. CCM wamona loophole ni kupitia CUF kwahiyo wakaipitisha hoja ya kubadilisha kipengere hicho. Hiyo si sawa kabisa na Chadema walikuwa na haki ya ku walk out. Ikiwa mbinu kama hizi zitakuwa zinatumika hatutaweza kuona upinzani bungeni ila wananchi tuko gado kuona upinzani haudhoofishwi kwa mbinu chafu.
 
Seriously Chadema kuna tatizo. Ama wamelewa madaraka au kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo. Hawa jamaa baada ya mkutano wa kamati kuu waliwajibu kwa kejeli za ki-JF wenzao wa CUF ambao walichukua hatua mara nyingi kuwasihi Chadema waunganishe nguvu ya upinzani. Kwa makusudi au kulewa wakadhani CUF wasinge-react. ! Wenzao wakatumia ushawishi wa kibunge kuwatega na sasa wamevuna mabua!

Mimi sidhani kama Mbowe ndiye anayewaburuza, ukiangalia hoja za Mdee na Lisu ni hizi ambazo tunazozisoma kila siku humu JF! Hivi hawa jamaa wanachukua porojo za humu kupeleka bungeni?
JF is killing CDM! Kep it up JF!
Itakuwa ajabu kubwa basi! Ama kwa namna nyingine ni kwamba baadae huulizana "uliona nilivoandika JF?" naomba isiwe kuwa ndivyo hivyo! sipendi kabisa kuamini katika hilo.
 
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....

Kwa hiyo unashauri waungane na CCM "B"ndiyo utajisikia vizuri!!pole sana mkuu!!
 
MIMI nadhani ingekua poa kama mwenyekiti wa CDM angefanya mpango wa kuunda tume ya vyama vyote vya UPINZANI wawe lengo moja,ili
nguvu izidi zaidi ktk hoja mchanganyiko hivi mnajua CDM wako juuuuuu ile mbaya kinachotakiwa ni umoja tuuuu
 
kama wadau wengi wanavyosema kuna ajenda nyingi nyuma yake. udini, ukabila na kushindwa kutafsiri vyema kanuni za bunge. Bila kusahau uroho wa madaraka na Roho mbaya tu. lakini pia inaonekana kuna mawazo mburuzo. Mbowe anawaburuza wenzie.

Tukijikumbusha nyuma wenzao CUF waliwashirikisha chadema na ndio maana Dr. Slaa, Cheyo na Zito wakapata umaarufu.

iweje leo wao wawe kinyume chake?. Nafikiri wanazidi kujinyambulisha na kujulikana walivyo na hii sio nzuri katika kuleta utengamano wa kisiasa na mustakabali mwema wa nchi yetu.

sijui wengine wanaliona vipi hili.

Ndugu hongera kwa maoni yako,ningekuheshimu sana kama ungefanya uchunguzi yakinifu juu ya hili kabla hujaandika.

Labda unisaidie kunijibu je unaweza kutueleka ni mazingira gani yalipelekea CUF kuwahusisha Chadema na vyama vingine 2005 na si 2000.

Naomba unisaidie kunifungua ushirikiano uliopo sasa wa serikali ya kitaifa Zanzibar unaleta madhara gani katika Muungano ,katika swala la mipaka ya kiuongozi na maamuzi.

na mwisho kwanini wameona ni muhimu leo ndani ya Bunge wapinzani wengine wameona na si nje ya Bunge waliko wananchi toka mwanzo.

Baada ya majibu yako natakuwa nimekujifunza zaidi.
 
mie niliuza tangu jana nani alipeleka hilo suala la kambi ya upinzani kuunganishawa wakati huu cdm in majorty ya kuunda hiyo kambi? why now?
 
Seriously Chadema kuna tatizo. Ama wamelewa madaraka au kuna tatizo kubwa zaidi ya hilo. Hawa jamaa baada ya mkutano wa kamati kuu waliwajibu kwa kejeli za ki-JF wenzao wa CUF ambao walichukua hatua mara nyingi kuwasihi Chadema waunganishe nguvu ya upinzani. Kwa makusudi au kulewa wakadhani CUF wasinge-react. ! Wenzao wakatumia ushawishi wa kibunge kuwatega na sasa wamevuna mabua!

Mimi sidhani kama Mbowe ndiye anayewaburuza, ukiangalia hoja za Mdee na Lisu ni hizi ambazo tunazozisoma kila siku humu JF! Hivi hawa jamaa wanachukua porojo za humu kupeleka bungeni?
JF is killing CDM! Kep it up JF!

Ndugu Jesuit;
Tumia muda wako kusoma maoni yangu kama ifuatavyo:-
Mwaka 1995 NCCR-Mageuzi walikuwa na nguvu sana. Kulitolewa mwito vyama vya upinzani viungane ili kuiondoa CCM madarakani. Vyama vyote vilikubali isipokokuwa CUF iliyoamini itachukua Zanzibar hivyo kutohitaji ushirikiano! Matokeo yake wote tunayafahamu kwamba mwisho wa siku kila mmoja alienda njia yake!
Mwaka 2000 baada ya uchaguzi CUF walipata viti vingi vya ubunge hivo kuwa na haki ya kuunda kambi ya upinzani bungeni. Wakati huo hapakuwa na neno "Kambi rasmi ya upinzani" Katika chaguzi za kamati mbalimbali Hamad alishindwa na Bwana Mapesa. Aliposhindwa akaona hajatendewa haki hivo akaenda bungeni kushawishi wabunge wakubaliane na mabadiliko katika kanuni kwa kuongeza neno kambi rasmi ya upinzani Lengo hapa likiwa ni CUF kuwadhibiti wapinzani kutoka vyama vingine vya upinzani. Kimsingi CUF waliamini wao wataendelea kuwa na wabunge wengi katika Bunge la Jamhuri hivyo kuendelea kunufaika na ruzuku mbalimbali za kibunge. ANGALIZO; CUF wamekuwa sehemu ya CCM tangu mwaka 2002 baada ya huyo huyo hamad Kuchaguliwa na Mkapa kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais.
Mwaka 2005 baada ya uchaguzi mkuu CUF waliongoza kwa kuwa na wabunge wengi lakini hawakufikia idadi iliyotamkwa kwenye kanuni kwamba; ili waunde kambi rasmi ya upinzani lazima wawe na 12.5% mwanzoni walitaka kulazimisha kuunda kambi pasipo kutimiza hayo masharti. Hoja zao zilishindikana kwa kuwa CCM walitaka kuwavunja nguvu. Waliposhindwa ndipo wakawashawishi wapinzani wengine waungane ili kufikisha ile 12.5%. Wenzao Akina Cheyo na CHADEMA waliamua kuwapa masharti kazaa na kwa kuwa interest yao ilikuwa ni vyeo na si kuleta upinzani wa kweli walikubali haraka haraka. Katika makubaliano hayo walilazimika kutoa sehemu ya uongozi wa kamati kwa vyama vingine ndio sababu akina slaa, Cheyo na Zito waligombea peke yao kwenye hizo nafasi ingawa walitakiwa kutoa wagombea zaidi ya mmoja.
Haya ni machache ya mengi yaliyojili tangu mwaka 1995 yakiihusisha CUF.
Mwisho ni kwamba CCM imechaguliwa kutokana na Sera Zake ambazo zinaenda mpaka Zanzibar. CUF wameunda serikali ya umoja wa kitaifa na CCM ili kutekeleza sera za CCM hivyo kiufundi wao si wapinzani tena maana wamekubaliana na sera za chama tawala hivyo kuungana nacho. Sasa kulazimisha CHADEMA iungane na CUF ni kulazimisha hicho chama kikubaliane na sera za CCM. Je, unaona hiyo ni sawa sasa kuita huo bado ni upinzani?
 
kama wadau wengi wanavyosema kuna ajenda nyingi nyuma yake. udini, ukabila na kushindwa kutafsiri vyema kanuni za bunge. Bila kusahau uroho wa madaraka na Roho mbaya tu. lakini pia inaonekana kuna mawazo mburuzo. Mbowe anawaburuza wenzie.

Tukijikumbusha nyuma wenzao CUF waliwashirikisha chadema na ndio maana Dr. Slaa, Cheyo na Zito wakapata umaarufu.

iweje leo wao wawe kinyume chake?. Nafikiri wanazidi kujinyambulisha na kujulikana walivyo na hii sio nzuri katika kuleta utengamano wa kisiasa na mustakabali mwema wa nchi yetu.

sijui wengine wanaliona vipi hili.

Maneno yako swadaktaaah

Choyo na wivu umewajaa kwenye mioyo yao
 
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....

Tatizo ni Dogo tu mdogo wangu,
Miaka ya nyuma Chadema walikuwa wanaunda kambi ya upinzani kwa kushirikiana CUF na vyama vingine.

Lakini kwa hali iliyopo sasa ni kuwa CUF wameungana na mpinzani wao wa miaka yote yaani CCM.

MFANO:
Mimi na wewe tuungane kumpinga Mzee Mwanakijiji, then siku chache zijazo mimi niungane na Mzee mwanakijiji, kisha niwe nakulazimisha kuendeleza ule umoja wetu wa kumpinga Mzee Mwanakijiji...
Wewe hii itakuingia akilini na kunikubalia?

Sasa Chadema wanachokipinga kwa CUF ni kuwa CUF wao wameshakubali ndoa kwa CCM, sasa iweje wang'ang'anie na kulazimisha kujiunga ktk kambi ya upinzani?
 
Back
Top Bottom