Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Nimetatizwa na hali iliyojitokeza jana bungeni pale wabunge wa CHADEMA walipoamua kutoka nje ya ukumbi kususia hoja ya kufanyia marekebisho kipengele cha kanuni ya kambi ya upinzani bungeni. Kwa mtazamo wangu nadhani wabunge wa CHADEMA wanachofanya si haki na hasa kwa wapiga kura wao waliowapa idhini ya kuwawakilisha bungeni. Lakini pia napata hisia zaidi za kuona kama Mwenyekiti wao Freeman Mbowe kama mtu anayewaburuza zaidi wabunge wa chama hicho. Hivi kuna tatizo au ugumu gani CHADEMA kushindwa kuungana na wabunge wa vyama vingine vya upinzani kuunda kambi ya upinzani? Ni mtazamo wangu tu....