Hivi ni maswali kwa waziri mkuu au maswali kwa Mizengo Pinda?

Ptz

JF-Expert Member
Aug 23, 2011
541
384
Shaloom wakuu! Kila siku ya Alhamis wakati vikao vya bunge la Tanzania vikiendelea huwa mida ya saa 3 kamili kuwepo na kipindi cha dakika 30 za wabunge kumuuliza waziri mkuu maswali ya papo kwa papo. kwa mujibu wa kanuni za Bunge la Tanzania toleo la 2007 kanuni ya 38:1 "waziri mkuu anaweza kuulizwa maswali na mbunge yoyote ambayo yatazingatia masharti kuhusu Bunge pamoja na mwongozo uliowekwa na nyongeza ya sita ya kanuni hii" hoja yangu ni kuwa ni maswali kwa waziri mkuu kama taasisi au ni maswali kwa Mizengo Pinda kwa jina? maana kwa uelewa wangu waziri mkuu ni taasisi na kwa maneno mengine mtu yeyote anayekalia kiti hicho iwe ni kwa kukaimu au kwa kudumu lazima kipindi hicho kiwepo maswali kwa waziri mkuu kwani hata kanuni haijatamka jina la mtu. Imekuwa ni kawaida kwa bunge letu Mh Pinda asipokuwepo kipindi hiki hukosekana mfano ni siku ya leo. Naomba Magreat Thinker mchangie.
 
Back
Top Bottom