Hivi ni kweli kwamba CHADEMA imefilisika kisera?

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Baada ya kuwatumainisha Watanzania wengi wenye hamu ya mabadiliko katika Nchi hii pendwa ya Tanzania, inashangaza kuona kamba CDM haisikiki tena iwe kwenye vyombo vya Habari vinginevyo. Katibu Mkuu sijui kaenda kusoma au likizo haifahamiki. Hatuambiwi List of Shame wala Kupigania Rasilimali za Umma! CDM imebaki kwenye mdororo unaotia huruma!

Swali dogo la kujiuliza ni kwamba ni kweli Katibu Mkuu aliyepo viatu vinampwelepweta kiasi hicho hadi CDM inapumulia mashine au umaarufu wa Chama hiki haukuwa ni Sera bali maandamano na Vurugu? Ni nani Afisa Habari wa CDM hivi sasa na anafanya nini? Ni lini ule ushahidi mliosema mnao kwa miaka 8 utatumika kumfikisha mliomtuhumu Mahakamani? Au mliwandanganya Watanzania na kwamba hamna lengo la kushika dola? Nauliza tu. Swali dogo!!
 
Media zote zimepigwa marufuku kuweka issues za wapinzani.Pole kama hujui hilo
 
Waliofilisika ni wale waliojipa ushindi bandia na kusambaza mitandaoni, eti wanapongezana kwa ushindi bandia
 
mbona ile TV yao iko bize kutangaza udhaifu wa Serikali si wangeitumia hiyo kujitangaza?

TV yao ipi?Hivi CDM wana TV station siku hizi??Akili zako kama wale Mahakimu waliowapa dhamana watuhumiwa wa pembe za ndovu wakati sheria hairuhusu.
 
Mnakataza mikutano, mnaleta sheria ya habari halafu mnabambika watu kesi ambazo hazieleweki na mnaikataza mahakama kufanya kazi yake ikiwa huru kisha mnapata courage ya kuuliza maswali kama haya ambayo hayana hata vichwa jamani?
 
Si mnayo TV yenu? katangazeni mambo yenu huko!
 
Baada ya kuwatumainisha Watanzania wengi wenye hamu ya mabadiliko katika Nchi hii pendwa ya Tanzania, inashangaza kuona kamba CDM haisikiki tena iwe kwenye vyombo vya Habari vinginevyo. Katibu Mkuu sijui kaenda kusoma au likizo haifahamiki. Hatuambiwi List of Shame wala Kupigania Rasilimali za Umma! CDM imebaki kwenye mdororo unaotia huruma!

Swali dogo la kujiuliza ni kwamba ni kweli Katibu Mkuu aliyepo viatu vinampwelepweta kiasi hicho hadi CDM inapumulia mashine au umaarufu wa Chama hiki haukuwa ni Sera bali maandamano na Vurugu? Ni nani Afisa Habari wa CDM hivi sasa na anafanya nini? Ni lini ule ushahidi mliosema mnao kwa miaka 8 utatumika kumfikisha mliomtuhumu Mahakamani? Au mliwandanganya Watanzania na kwamba hamna lengo la kushika dola? Nauliza tu. Swali dogo!!
Imefirisika mubashara
 
WALIKURUPUKA SANA KUJAZA NAFASI YA KATIBU MKUU, KATIBU MKUU NI NAFASI YA MAKADA, (WAFIA CHAMA) SASA HUYU KATIBU WAO HANA UZOEFU HATA WACHAMA, CHADEMA HAWAJUI KUWA KATIKA SIASA KOSA MOJA LINAKUONDOA ULINGONI, KOSA WALILOFANYA NI KUFIKIRI KUISHIKA KANDA YA ZIWA NI KUMTEUA MASHINJI, LABDA WANGEKUWA NA AKILI WANGEFIKIRIA HATA KUMTEUA ALIEKUWA MBUNGE WAO WA NYAMAGANA JINA SILIKUMBUKI, TAYARI ANAJINA KUBWA NA NI MPAMBANAJI INGELETA LADHA KISIASA, ILA KWA KUWA WANABAHATI MBAYA YA VIONGOZI WASIO TUMIA KICHWA KUFIKIRI, HILI HAWAKULIONA, NA LITAWATESA MAISHA YAO YOTE. SWALI DOGO MNAMJUA KATIBU MWENEZI WA CHADEMA? MNAMJUA MSEMAJI WA CHADEMA? MAJUKUMU YAO NI YAPI? HIVI HATA WAO WANA OFISI KWELI?
 
Et mikutano imezuiliwa halafu watu wanajisifu.
Na EU imeagiza siasa ziendelee kama kawaida.Subirini mtaona
 
Et mikutano imezuiliwa halafu watu wanajisifu.
Na EU imeagiza siasa ziendelee kama kawaida.Subirini mtaona
Ni upuuzi na ujinga kutegemea EU kukuendeshea Siasa za Nchi yako! Ni sawa na kumkodi Baba toka kwa jirani kwa malipo na kujitangaza una baba wakati huna!!
 
Waliofilisika kisera ni wale wanaotumia mitutu ya bunduki kutunyima haki yetu ya kikatiba kutangaza Sera zetu.
 
Jamani nyie ni wachokozi. Mmefikia shughuli za kisiasa na funguo mmetupa sijui wapi mpk 2020. Mnataka wasikike vipi na wapi? Kama hata wale wanaotoa tu mnawakamata na kuwanyima dhamana ili wasiote utadhani kule lupango ni marufuku kuota. What do you want from these guys?
 
Back
Top Bottom