Hivi ni kweli? kujadili suala la pamba ni kutumia vibaya muda wa bunge?

KIMBURU

JF-Expert Member
Jan 12, 2011
210
189
Kuna mbunge katoa hoja binafsi ya kutaka bunge lijadili suala la kushuka bei ya pamba, kitu cha kushangaza ni kwamba baada ya spika kutoa muongozo wa kueleweka, kwanza amecheka cheka, pili kamlaumu mbunge kwa kusoma kanuni nusu nusu na tatu kasema kulijadili suala hilo ni kutumia vibaya muda wa bunge. Suala hili limeniuma sana nikilingalinisha hasara tunayoipata wakulima wa pamba na kauli anazozitoa huyu fisadi wa kike.
Nadhani muda wa CCM kukaa madarakani unahesabika kwa sababu hakuna inachoweza kusimamia; wafanyakazi wanalalamika, wakulima wanalalamika, wananchi wanalalamika; na kubwa kuliko yote hata rais mwenyewe analalamika.
 
Huo ndio mtazamo wa spika, kwamba kujadili bungeni uchumi wa kanda ya ziwa ni kupoteza muda.
 
Huo ndio mtazamo wa spika, kwamba kujadili bungeni uchumi wa kanda ya ziwa ni kupoteza muda.

Inauma sana. Ukweli ni kuwa, bila CCM kuondolewa madarakani tusitegemee jema kwa wakulima wa pamba. Wengi wa wanunuzi wa pamba ni makada wa CCM (kuanzia SHIRECU)
 
Halafu slogan ya Taifa "kilimo ni uti wa mgongo". huyu Bi mkubwa kwake yy vijembe na maneno ya shombo bungeni, kwake yy ndio ya muhimu zaidi kuliko kujadili mustakabali wa wakulima
 
CCM wameamua kuwakomoa wakazi wa mikoa ya pamba kwani wengi wao wamekihama chama na kukimbilia M4C majimbo ya Musoma mjini, Ilelema, Nyamagana, ukerewe, Biharamulo, Bukombe, Maswa Magharibi, Maswa mashariki, Meatu Bariadi Mashariki.Majimbo haya yote yanawakulima wa pamba kwa hiyo CCM hawana cha kupoteza.Nashauri CDM wafanye yafuatayo ili kuwasaidia wapiga kura wao;
  1. Wafanye utafiti wa haraka kuangalia trend ya bei ya pamba kwenye soko la dunia ili kujua ni muda gani pamba huwa inapanda kwenye soko la dunia;kwa kawaida bei hupanda kuanzia september wakati huo wakulima tayari wameuza pamba yao kwa bei ya kutupa
  2. Wawashauri wakulima na serikali ili kubadilisha muda wa kuanza msimu, inapendekezwa wawashauri wauze kuanzia september.
  3. CDM waangalie uwezekano wa kuwashauri wakulima kwa muda huu wavumilie wakati wanajiandaa kuiondoa CCM madarakani na kuiweka CDM ambayo kwa sasa iko mioyoni mwa wana-lake zone.
  4. CDM wawaandae wakulima kisaikolojia kuwa kuanzia 2013-2015 wakubali hasara lakini waelekeze nguvu kujiandaa kuiweka madarakani CDM hapo 2015
  5. Baada ya kuisha bunge M4C ikaanzia lake zone lengo ni kuelezea hoja za upinzani zilivyozimwa ikiwemo kutozungumziwa kwa hali tete ya zao la pamba
Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom