Hivi ni kweli kiswahili hatuna neno "future"?

Ginner

JF-Expert Member
May 8, 2011
1,459
1,832
Bahari za mihangaiko wanandugu....leo katika maongezi na baadhi ya wadau hapa mtandaoni..jamaa yangu akasema..."Tatizo la sisi waswahini ni kwamba hatunaga future katika mipango yetu...tuna zamani tu na ndomaana hatuna neno future kwenye lugha yetu..." Nikajaribu kutafakari nikaona kweli huyu mtu analogic...tuna neno zamani kuonesha wakati uliopita...tukawa na neno sasa kuonesa wakati uliopo ila nikashindwa kujua wakati ujao unaitwaje kwa neno moja tu la kiswahili....

Kama kuna mtaalam wa lugha humu ndani tafadhali atujuze future kwa kiswahili ni nini????
 
Boss naomba nitafsirie sentesi hii, I will see you in future days.

Nitakuona siku za usoni!
Nadhani kutumia Neno ''Tutaonana siku za usoni'' au (Mbeleni) kama imekaa fresh kwa upande wangu

???Nitakuona siku za Mustakabala? hii imekaaje!
 
Hapo tuliwapiku Waingereza. Hawana neno "pole".
Wanalo pengine kwa matumizi mengine Kuna North Pole na South Pole.. hahaha

Kwani Kumwambia Mtu Am Sorry!
Nadhani inaendana na meaning hiyo

Ugua Pole = Get well ??
 
Si lazima kuwa na tafsiri ya neno kwa neno ili kulinganisha Kiswahili na Kiingereza. Hebu wataalamu wa sarufi wa lugha zote waje hapa kutujuza
 
Mtaumia kwa kuhangaika na tafsiri sisisi, si kila dhana au neno limo kwenye kila tamaduni/ustaarabu.
 
Back
Top Bottom