Hivi ni kweli Dallas wa Wolper kafilisika kifedha au ni story tu za mjini?

Kama ni kweli ametapanya mil 700 basi jamaa ni bonge la panzi! wajanja wanatengeneza asset alafu wanaendelea kula bata, huyu alitakiwa anunue kirikuu nne, ajenge nyumba nzuri ya kukaa yeye na nyumba za kupangisha fedha nyingine angetuliza kwa ajili ya kusukumia dili za fasta mjini na bado hao watoto angewararua leo, kesho keshokutwa mpaka apate ngoma
Big up kaka,kwenye mia saba alikuwa mdg mdg tu kama ulivyoshauri,tungemzika na chenji yake
 
Kama chizi fresh dallas. .akipata pesa ya chips kuku tu full kelele. ..kiukweli jamaa anatilisha huruma kwani kakojoa mbaya. ..halafu yule pimbi hajawahi kuwa mzungu wa unga. .aliwekwa bond na wazungu wa unga akabahatika kuchomoka na mzigo so peak ile ya kifedha ataisikia bombani
 
Kama chizi fresh dallas. .akipata pesa ya chips kuku tu full kelele. ..kiukweli jamaa anatilisha huruma kwani kakojoa mbaya. ..halafu yule pimbi hajawahi kuwa mzungu wa unga. .aliwekwa bond na wazungu wa unga akabahatika kuchomoka na mzigo so peak ile ya kifedha ataisikia bombani

Duu kweli mkuu unamjua vzr ndg yake ndio alimuweka bond ila wakati yupo shamba nae alikuwa anapiga shunting shamba kuleta mjini wakamuamini wale jamaa ndio akawaumiza na kurudi tena kusafiri hawezi ni wanted ngoja tuache ni mipango ya watu hii ila huyo jamaa ni ----- tu hao bongo muvi kwa laki hadi 50 elfu hawakatai wana njaa hatari
 
MFANYABIASHARA ‘mjanjamjanja’, Abdallah Mtoro ‘Dallas’, amefilisika na amechoka vibaya kiasi cha kuanza kuombaomba bia.
Mwanasiasa aliyeshinda ujumbe wa Nec (CCM) hivi karibuni, William Malecela ‘Le Mutuz’, aliandika wiki iliyopita kwenye ukurasa wake, mtandao wa kijamii Facebook: “Ok I have this friend, Super Dallas anatokea sana kwenye magazeti. I feel sorry for him aliwahi kuwa na utajiri wa ajabu alikuwa akihonga Mabebs wa mjini mpaka USD 10000 (karibu shilingi milioni 16).

Abdallah Mtoro ‘Dallas’.

“Then akawa mchumba wa Wolper! Poor guy now amechacha watu wote hawamtaki wanamkimbia waziwazi na kumcheka, I feel so bad for him siwezi kumkimbia I know him, so I accommodate him like I know nothing people get upset with me that kwa nini ninam support na kumpa vinywaji?”
William ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, John Samuel Malecela, alichanganya Kiswahili na Kiingereza lakini alichomaanisha ni kuwa Dallas amefilisika kiasi ambacho yeye ndiye amekuwa akimlinda kwa kumnunulia vinywaji.
Jitihada za kumpata Dallas azungumzie madai hayo ya William hazikufanikiwa lakini baada ya mwanasiasa huyo kuandika hivyo, watu wengi walinakili ujumbe huo na kuusambaza kwenye mitandao mbalimbali.

Jacqueline Wolper.

Bloga mmoja wa kike, aliweka kwenye blogu yake huku akisindikiza kwa kichwa cha habari: “Maskini Dallas wa Wolper kutoka kwenye utajiri wa madola mpaka zero ground.” Akimaanisha kwamba mfanyabiashara huyo alikuwa tajiri akimiliki noti za dola mpaka kufilisika hadi sifuri.
Wolper alipoulizwa kuhusu hali ya Dallas kama anaweza kumsaidia, alijibu: “Nisingependa kumzungumzia huyo mtu.”
 
Hii ingeletwa na warumi ingependeza, hii imewatokea wengi hata le muntuz asingeshutuka akajenga banda angekuwa kama jack mpemba au jack unguja
 
Back
Top Bottom