Hivi ni kweli anavyosema kipanya?

534907_360404210732966_330362536_n.jpg
 
Mkuu MziziMkavu, nilisoma hii habari kwenye gazeti la Mwananchi la 09/04/2012, kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajui kusoma wala kuandika. Sasa hili ni janga la kitaifa na ni moja ya sababu Tanzania kufika hapa tulipo, miaka 50 ya Uhuru bado tunaogelea katika umaskini wa kutisha licha ya rasilimali lukuki zinazotuzunguka.

:coffee:
 
Last edited by a moderator:
MziziMkavu nakushukuru sana, inawezekana kabisa kuwa ni kweli kwani kuna wanafunzi ambao wanafaulu kwenda shule za kata lakini kusoma hawawezi vizuri sasa sijui inakuwaje wanafaulu, ni swali ambalo Wizara ya Elimu wanayo majibu sahihi
 
MziziMkavu, naomba msaada wako, hivi kile kipindi cha MaishaPlu kinachoendeswa na kipanya ratiba yake huwa ni mwezi wa ngapi?
 
Mkuu MziziMkavu, nilisoma hii habari kwenye gazeti la Mwananchi la 09/04/2012, kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajui kusoma wala kuandika. Sasa hili ni janga la kitaifa na ni moja ya sababu Tanzania kufika hapa tulipo, miaka 50 ya Uhuru bado tunaogelea katika umaskini wa kutisha licha ya rasilimali lukuki zinazotuzunguka.

:coffee:
@Fredrick Ishengoma Hiyo yote inatokana na hao Viongozi wetu wa Serikali Uongozi wao ni mbovu sana Serikali itakayo chukuwa Uongozi Mwaka 2015 itabidi ilishughulikie hili Suala la kushuka kwa elimu Tanzania ee Mungu isaidie nchi yetu ipate Viongozi bora wenye kuipenda nchi yetu ameen.
 
Mkuu MziziMkavu, nilisoma hii habari kwenye gazeti la Mwananchi la 09/04/2012, kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu hawajui kusoma wala kuandika. Sasa hili ni janga la kitaifa na ni moja ya sababu Tanzania kufika hapa tulipo, miaka 50 ya Uhuru bado tunaogelea katika umaskini wa kutisha licha ya rasilimali lukuki zinazotuzunguka.

:coffee:
Wakati wa Mwl. tuliambiwa tuna maadui watatu Ujinga, Malazi na Umasikini. Hawa tunatakiwa kuwashinda ili kuwa na maisha BORA na si BORA maisha.
Ukichunguza vizuri ni kuwa ukimuua mmoja (UJINGA) wengine wanatafuta njia ya kupita wenyewe.
Bahati mbaya tunatoa michango kumsaidia UJINGA aongeze ukubwa wa jeshi lake!.
Maisha BORA yatafikiwa lini?
 
Inasikitisha laikini ni ukweli uliowazi japo watawala wetu wanakataa bila ya kuchukua hatua zozote, kama vyuo vya ualimu haswa vya binafsi vinataka wanafunzi wenye Div 1V hata pointi 29 hata kama umezipata katika sitting tofauti unategemea huyo mwalimu ataweza kweli kumjenga kifikra mwanafunzi...sidhani!!!

Ni jukumu la serikali kuachana na vipaumbele visivyokuwa na Long-run direct impact kwa mwananchi.... kujikita zaidi katika kuboresha Elimu yetu haswa upande wa walimu bora iwe miongoni mwa vipaumbele...!
 
Back
Top Bottom