- Thread starter
- #21
Huulizwi vyeti au chochote kwa sababu wao wanajali "uungwana wako" na ni "watekelezaji wa sheria".
Unaweza usiulizwe vyeti na kazi ukapewa. Unaweza kusafiri kwenye usafiri wa umma usiulizwe tiketi.
Unaweza kudanganya chochote ukajiona wewe mjanja lakini....Siku wakikukamata, hakuna msalie mtume.
Mfano, ikiwa imeandikwa "Kupanda basi bila tiketi faini ni dola 10,000 au kifungo cha miaka 3, siku wakikukamata hakuna wa kumpa rushwa wala mjomba atakayekutetea.
Kweli Marekani inatumia sana uungwana lakini wanakua very selective maana hawatumii ungwana huo huko kwenye criminal backround, Drug test etc kuna vitu vingi tuu vingine visipokaa sawa hupati kazi
Ingekuwa rahisi kama walavyotumiama makampuni kwenye drug test na Criminnal wangeweza kutumia makampuni ya verify vyeti , wangeweza hata kusema leta copy wakae nazo ili kama wakija kukugundua wana kesi nzuri ya kugushi , lakini unaandika tuu Education:Master's Degree in Computer Science
Kazi ukiomba kwenye academic institution ndio wanauliza , maana huo ndio msingi wa kazi yenyewe au zile kazi zenye board exams ambazo unarenew baada ya muda fulani huko wanauliza board kama uko uptodate