Hivi ni kwanini maji ya mto Nile yanatoka ziwa Victoria(chini) na yanapandisha kwenda Egypt(juu)?

Tumezoea kuona kwa ramani yya kwenye karatasi kua afrika tuko chini wenzetu wako juu. Ndio neno la majuu linakuja hapa! Kihalisia misri iko chini kuliko mwanza ndio maana maji yanakwenda. Maji hayawezi kupanda mlima
 
Na nitafiti zipi zilisha wahi kusema kaskazini ni juu!? Au TWAWEZA ndio wamefanya huo utafiti
 
Maji huwa hayapandi juu kwa namna yoyote ile labda kuwe na nguvu ya ziada iyasaidie kufanya hivyo kama vile pampu na nyingine. Kingineni kuwa siku zote maji ya mto hutiririka kwenda kwenye bahari, ziwa, bwawa, au mkondo wa mto mwingine ambao uko eneo la chini ukilinganisha na kule unakotokea mto. Ndio maana hata bahari inasemekana kuwa na chumvi nyingi kwa sababu mito mamilioni inaingiza maji yaliyo na madini mengi yenye chumvichumvi kwa miaka mamilioni. Hii ni kwa sababu bahari siku zote iko katika eneo la chini kabisa kuliko sehemu zote na hivyo mito inaifuata kutoka sehemu zote za juu. Ukitaka kuelewa hilo, hata muinuko wa mahali hupimwa kwa kuuwianisha kutokana na usawa wa bahari. Na ndio maana utasiki sehemu Y iko mita kadhaa kutoka usawa wa bahari. Kwa hiyo ni vigumu kusema mto Nile unapanda juu kwa sababu palipo na bahari siku zote ni bondeni.
 
are u serious!?.. Nadhan hii ilitakiwa ikae katika jukwaa la jokes.
Hii kitu hata mtoto wa darasa la sita analijibu... Its a shame to call urself a great thinker ukiwa hujui hata ramani ni nini!...

Kama na huyu alotoa swali hili ni great thinker mimi najitoa kuanzia leo sitaki ugreat thinker..eboo!!
 
Usiku sana kama mida ya saa nane ziwa Victoria huwa linainuka juu then linashuka na kutumia kusubiri vivuko vya Kamanga na Busisi.
 
Asante kwa jibu lako.Maana mimi nilifikiri kwa kuwa dunia ni duara ukiikata ulipopita mstari wa ikweta utapata vipande viwili vyenye slop.Slop ya kwanza ikielekea kaskazini unakoelekea mto Nile na slop ya pili ikielekea kusini

Umenifikilisha
 
Maji huwa hayapandi juu kwa namna yoyote ile labda kuwe na nguvu ya ziada iyasaidie kufanya hivyo kama vile pampu na nyingine. Kingineni kuwa siku zote maji ya mto hutiririka kwenda kwenye bahari, ziwa, bwawa, au mkondo wa mto mwingine ambao uko eneo la chini ukilinganisha na kule unakotokea mto. Ndio maana hata bahari inasemekana kuwa na chumvi nyingi kwa sababu mito mamilioni inaingiza maji yaliyo na madini mengi yenye chumvichumvi kwa miaka mamilioni. Hii ni kwa sababu bahari siku zote iko katika eneo la chini kabisa kuliko sehemu zote na hivyo mito inaifuata kutoka sehemu zote za juu. Ukitaka kuelewa hilo, hata muinuko wa mahali hupimwa kwa kuuwianisha kutokana na usawa wa bahari. Na ndio maana utasiki sehemu Y iko mita kadhaa kutoka usawa wa bahari. Kwa hiyo ni vigumu kusema mto Nile unapanda juu kwa sababu palipo na bahari siku zote ni bondeni.

Vipi kwa Bahari ambazo hazina maji ya chumvi?
 
Eh, nna mashaka sana ufahamu wako, yani hujui kaskazini ni juu
Acha ku coment kwa hisia wewe, juu sio kaskazini juu ni mlimani kama kusini ingekuwa ni chini basi mito yote duniani ingekuwa inaelekea kusini. Lakini ukweli ni kuwa maji hutiririka kutoka uwanda wa juu(milimani) na kuelekea uwanda wa chini acha kukariri.
 
Hapa ndo tunapojua jua kwamba ulikuwa unakariri ama unaelewa? Nyingine ni hii :

Ukichora shape ya dunia ambayo ni spherical, je sisi tuko juu ama ndani ya huo mchoro?
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom