Hivi ni kwanini maji ya mto Nile yanatoka ziwa Victoria(chini) na yanapandisha kwenda Egypt(juu)?

mfukunyunzi

Senior Member
Mar 4, 2011
142
26
Jamani wataalamu wa Jiografia na maumbile ya dunia naomba mnisaidie kutatua hili suala:
Ukitizama jinsi umbile la dunia (kama unaweza angalia hata kwenye lile umbile la dunia linalowekwa maofisini au majumbani) jinsi lilivyo inaonesha dhahiri kuwa eneo lilipo ziwa victoria lipo kwenye uwanda wa chini ukilinganisha na kule ilipo nchi ya Misri sasa chakushangaza ni kuwa maji ya mto Nile yanawezaje kumwagika kutoka ziwa Victoria na kuelekea kule Misri sehemu ambayo iko juu, na kwa uelewa wangu mimi ni kuwa maji huwa yanatiririka kutoka juu na kuelekea chini. Naomba wataalamu na magreat thinkers wenzangu mnisaidie kutatua/kunielewesha hili suala.

nile river.jpg
 
Mmmh! Ngoja tusubiri wataalamu!
 
Sina uhakika na kama Misri ipo juu au vipi...ila kitu ambacho nina uhakika ncho ni kuwa, ili kuufikia mto Nile popote ulipopita ni lazima ushuke, yaani umepita katika bonde, na kutoka na jiografia ya mahali ambapo mto huo unapopita ndiyo maana huwa linaitwa bonde la mto nile.
Tusubiri wataalam zaidi waendelee kuchangia, labda wanaweza kutusaidia zaidi
 
  • Thanks
Reactions: cmp

Mkuu unachangaya juu na kaskazini?....
 
As far as my my geography is......lake Victoria is situated where the imaginary line with 0 degree known as equator which divides the earth into two same hemispheres passes...! as you can see its like the childish riddle that asks....KAMA JOGOO AKITAGA YAI KATIKATI YA MLIMA KILIMANJARO YAI LITAANGUKIA UPANDE GANI?
Hivyo basi, kutokana na kuwa katikati...maji huweza ku-flow katika pande hizo kuu mbili zilizogawanywa....!
(wanajiografia wanikosoe)
 
Sina uhakika na kama Misri ipo juu au vipi...ila kitu ambacho nina uhakika ncho ni kuwa, ili kuufikia mto Nile popote ulipopita ni lazima ushuke, yaani umepita katika bonde, na kutoka na jiografia ya mahali ambapo mto huo unapopita ndiyo maana huwa linaitwa bonde la mto nile.
Tusubiri wataalam zaidi waendelee kuchangia, labda wanaweza kutusaidia zaidi

hapo kidogo naanza kupata mwanga flani.
 
Ngoja nikupe jawabu. Unapotazama ramani kitabuni ama iliyobandikwa ukutani ukaona nchi ya Misri ipo juu kama unavyoita wewe (ingawa ukweli ni kuwa ipo Kaskazini wala sii juu) unaweza kujiuliza mara alfu lela ulela hilo swali. Ukweli ni kuwa haipo juu.
Bara la Afrika, Wanajografia wanatuambia kuwa unapotokea Ethiopia kuelekea kusini unakuwa unaelekea uwanda wa juu. Ina maana kwamba maeneo mengi ya Kusini mwa Afrika yapo juu zaidi ya usawa wa bahari ukilinganisha na maeneo ya Kaskazini. Kwa mantiki hiyo, nchi za Sudani, Ethiopia na Misri zipo chini zaidi ukilinganisha na Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya ambako maji hayo ya mto Nile yanakotokea.

Jambo kama hilo hilo huwa lina wachanganya watu wengi kuhusiana na mito miwili mkoani Mbeya. Mito hiyo ni Songwe na Kiwira ambayo yote hupeleka maji yake kwenye Ziwa Nyasa (wenyewe wanaliita Ziwa Malawi kwa kuwa ni mali yao) Watu hudhani maji ya mito hiyo hupandisha milima. Lakini ukitazama vema na kukokotoa kiwango cha maeneo hayo kutoka kwenye usawa wa bahari, utagundua hakuna mto unaopandisha mlima.

Huo ndo mchango wangu.
 
soma google andika the source of river nile and how it flows to egypt utapata maelezo kibao.mm nipo north ya dunia naona kuna milima na mabonde pia ila jua ndio naliona linatoka south east linatua south west yaan kamma nusu duara kimzunguko kwa hivo saa 9 alfajiri limeshaanza kuonekana na kutua saa 3 usiku. sama to river nile limetoka uganda kule na kupita mabonde na sio kupanda milima.
 
Mimi sii mtaalam wa Jiografia,ila ninachofahamu ni kuwa bahari zote duniani ziko chini kwenye altitude moja,hivyo maeneo yote ya dunia(kwenye ardhi) ziko juu ya usawa wa bahari hivyo kupelekea maji toka pande tofauti kwenda baharini.
 
far as my my geography is......lake Victoria is situated where the imaginary line with 0 degree known as equator which divides the earth into two same hemispheres passes...! as you can see its like the childish riddle that asks....KAMA JOGOO AKITAGA YAI KATIKATI YA MLIMA KILIMANJARO YAI LITAANGUKIA UPANDE GANI?
Hivyo basi, kutokana na kuwa katikati...maji huweza ku-flow katika pande hizo kuu mbili zilizogawanywa....!
(wanajiografia wanikosoe)

Ninashwishika kusema jibu lako linaweza kuwa na hoja ya kuilinda, ila ngoja nijiridhishe kama hakuna mto unao flow toka kaskazini ya uganda kenya na kwingineko kuingia ziwa Victoria au kutoka kusini mwa Mwa ziwa victoria kuingia humo yaani toka Mwanza Shinyanga n.k
 
Ngoja nikupe jawabu. Unapotazama ramani kitabuni ama iliyobandikwa ukutani ukaona nchi ya Misri ipo juu kama unavyoita wewe (ingawa ukweli ni kuwa ipo Kaskazini wala sii juu) unaweza kujiuliza mara alfu lela ulela hilo swali. Ukweli ni kuwa haipo juu.
Bara la Afrika, Wanajografia wanatuambia kuwa unapotokea Ethiopia kuelekea kusini unakuwa unaelekea uwanda wa juu. Ina maana kwamba maeneo mengi ya Kusini mwa Afrika yapo juu zaidi ya usawa wa bahari ukilinganisha na maeneo ya Kaskazini. Kwa mantiki hiyo, nchi za Sudani, Ethiopia na Misri zipo chini zaidi ukilinganisha na Rwanda, Tanzania, Uganda na Kenya ambako maji hayo ya mto Nile yanakotokea.

Jambo kama hilo hilo huwa lina wachanganya watu wengi kuhusiana na mito miwili mkoani Mbeya. Mito hiyo ni Songwe na Kiwira ambayo yote hupeleka maji yake kwenye Ziwa Nyasa (wenyewe wanaliita Ziwa Malawi kwa kuwa ni mali yao) Watu hudhani maji ya mito hiyo hupandisha milima. Lakini ukitazama vema na kukokotoa kiwango cha maeneo hayo kutoka kwenye usawa wa bahari, utagundua hakuna mto unaopandisha mlima.

Huo ndo mchango wangu.
mkuu hapo kwenye red umechemka...ipo mito inayopandisha milima mfano mzuri ni mto Ruaha.
 
Back
Top Bottom