Hivi ni kwanini Gharama za Wakili ni kubwa hapa Tanzania?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,960
544
Kwa sasa hapa Tanzania Uwakili ni dili,ukiwa na Kesi inayohitaji Wakili unafikiria mara mbili maana gharama za Wakili ni kubwa sana.

Na hata hali ya kifedha ya Mawakili ni si haba hapa Tanzania. Vilevile kuna tetesi kuwa Mawakili wa pande mbili hukubaliana na hivyo kula fedha pande mbili.

Sasa si ni wakati wa kuweka mazingira mazuri ili msaada wa Wakili katika kesi iwe na gharama nafuu ili wananchi waweze kusaidiwa kisheria.

Wana JF wanasheria kwanini Gharama za mawakili hapa Tanzania ni za gharama kubwa?
 
Unaposema kubwa unalinganisha na nini? Unamaanisha kazi wanayofanya haiendani na malipo au kwa kuwa simply wananchi hawana kipato cha kutosha? Kama wananchi walio wengi hawana kipato cha kutosha basi hilo sio kosa la wakili ni la wananchi wenyewe na serikali yao. Hilo suala la kula dili la mtu mmoja moja kama lipo na ni utovu mkubwa wa kiapo cha utumishi katika uwakili!
 
gharama za wakili tanzania ni za kawaida sana, Anyway hujasema ni ghali kwa vipi, kuliganisha na nchi gani kwa aina gani ya kesi labda ufafanue.
 
Gharama za wakili bongo bado ni za kawaida tuu, nchi zilizoendelea hata kupangisha nyumba tuu lazima wakili fungu nene.

Gharama za wakili Tanzania zinadhibitiwa na sheria ya mawakili, hawalipwi zaidi ya asilimia 4 ya gharama halisi.
Kuna vituo kibao vya misaada ya kisheria kwa wasio na fedha, hivyo unapatiwa wakili bure.

Kesi zote za capital punishment, ambazo hukumu zake ni kifo, kama kesi za mauaji na uhaini, serikali inakuwekea wakili wa kukutetea ambaye analipwa na serikali yenyewe.

Mambo ya mawakili ndio kwanza wameongezewa ulaji tangu leo, Waziri wa Katiba na Sheria ameliambia Bunge, mahakimu wote wa mahakama za mwanzo sasa ni wahitimu wa degree ya sheria, hivyo mambo ya mawakili sasa ni toka mahakama ya mwanzo!.
 

Gharama za wakili Tanzania zinadhibitiwa na sheria ya mawakili, hawalipwi zaidi ya asilimia 4 ya gharama halisi.

"Gharama halisi" za nini, una maana damages zitakazo kuwa awarded kwenye kesi ya madai?

Mkuu, Pasco, tutajie, tafadhali, kipengele cha hiyo sheria inayosema mawakili wasilipwe zaidi ya "asilimia 4 ..."
 
Last edited:
"Gharama halisi za nini," una maana damages zitakazo kuwa awarded kwenye kesi ya madai?

Mkuu, Pasco, tutajie, tafadhali, kipengele cha hiyo sheria inayosema mawakili wasilipwe zaidi ya "asilimia 4 ..."

Kweli! Ukitaka mjadala unoge ni kuleta data toka reliable sources. Ukileta hisia hutaeleweka!
 
Pascal Mayalla ulipopotea kaka niliwaza mengi kikubwa nilihisi maana awamu hii ni kanda ya Balimi nikajua msukuma ameshakuteua msukuma mwenzio unakula kipupwe kwenye Ma Vx umetutupa humu
 
Nina swali.

Iwapo ulifungua kesi na bahati mbaya mkashindwa kesi hiyo.Je kuna sheria inayosema wewe uliyeshindwa umlipe mwana sheria aliyeshinda kiasi gani cha pesa kama gharama ya kesi?
 
Back
Top Bottom