Hivi ni kwa nini tunakuwa na maneno ya kashfa namna hii!!!!

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,701
Siku hizi imekuwa ni kawaida kwa watu wanaoenda kuwapongeza akina mama waliojifungua kutoa SIFA ambazo mimi naona ni KASHFA. Kwa mfano kama ni mtoto wa kiume eti wanasema "umetuletea jambazi" na kama wa kike "umetuletea changudoa, house girl...nk" Hata kama ni utani huu umezidi, inaweza kutokea kweli mtoto akawa hivyo. Hii tabia mimi siipendi, mbona zamani ilikuwa safi maneno ya umetuletea "mchumba, mkwe, mama, bibi dada, nk" yalitawala na yalikuwa mazuri.
 
hee! mie akitokea mtu aknambia hivyo namtimua .......haijahusu hata kidogo!

anambie umetuletea 'engineer' .........:D
 
Aisee kuna watu wanakupongeza umeleta jambazi? haki nitapigana na mtu mm! na urafiki kwishnei simhitaji ndio nimesikia hapa leo
 
Halafu unashangaa after sometime mtoto anakuwa Jambazi kweli halafu unaanza ku refer kwa mtu aliyetoa hiyo comment
 
teheeee kwa nini asiseme umetuletea rais tena mwenye PhD ya heshima toka Nairobi kwa Kalonzo
 
Wanaongea hayo ukiangalia vizuri wana upungufu wa hekima kwa mtu na kili zake timamu hawezi kufanya hivyo
 
Mimi nadhani inategemea na wewe ni mtu wa namna gani, labda unaendekeza utani wa kijinga, mimi nimezaa watoto wawili miaka hii mitano iliyopita na sijawahi kusikia mtu aniambie hivyo, na atakae jaribu atanijua vizuri.:A S angry::nono::nono:
 
hee! mie akitokea mtu aknambia hivyo namtimua .......haijahusu hata kidogo!

anambie umetuletea 'engineer' .........:D
......wengine kwa kujua mdomo huumba, hawasemi maneno mazuri...........
 
Mimi nadhani inategemea na wewe ni mtu wa namna gani, labda unaendekeza utani wa kijinga, mimi nimezaa watoto wawili miaka hii mitano iliyopita na sijawahi kusikia mtu aniambie hivyo, na atakae jaribu atanijua vizuri.:A S angry::nono::nono:
Unaweza ukaua mtu!!!
 
Ni utani tu jamani!...Mbona kuna watu humu ndani wanaitana"KICHAA WANGU". are they serious?
Kuna wakati inabidi tuelewe kwamba wazazi wanataniana!
Maana hata mtu akimwita binti yangu MCHUMBA, atakuwa anamvuruga ati, kwanini amwanzishie mambo ya uchumba wakati anatakiwa akikua aanze shule!
 
Wengine nilisikia wakisema kaleta barmaid!! muhimu mtu unapotamkiwa unakanusha saa hiyo hiyo na kumpa onyo aliyetamka,vinginevyo kweli kinywa huumba.
 
Ni utani tu jamani!...Mbona kuna watu humu ndani wanaitana"KICHAA WANGU". are they serious?
Kuna wakati inabidi tuelewe kwamba wazazi wanataniana!
Maana hata mtu akimwita binti yangu MCHUMBA, atakuwa anamvuruga ati, kwanini amwanzishie mambo ya uchumba wakati anatakiwa akikua aanze shule!

Unajua PJ bora useme hayo maneno kwa mtu ambaye ameishakuwa mtu mzima he/she wont mind sasa mtoto kazaliwa leo halafu unasema naona umetuletea Jambazi aftersomtime mtoto anakuwa jambazi kweli halafu ukikumbuka maneno ya huyo mtu wakati alipokuwa amekuja kukupa pongezi unaweza kuhisi ndio mchawi wako
 
Ni utani tu jamani!...Mbona kuna watu humu ndani wanaitana"KICHAA WANGU". are they serious?
Kuna wakati inabidi tuelewe kwamba wazazi wanataniana!
Maana hata mtu akimwita binti yangu MCHUMBA, atakuwa anamvuruga ati, kwanini amwanzishie mambo ya uchumba wakati anatakiwa akikua aanze shule!

Pls PJ utani mwingine haufai hata kidogo,,,,jambazi,changu,et.... no plz
 
kwli mtu akitoa comment za aqina hiyo kwa kichanga changu namtoa spidi, mambo gani ya ku label mtoto hivyo?
 
Back
Top Bottom