Hivi, ni kupenda au kutamani?

malisak

JF-Expert Member
Mar 16, 2006
694
772
Jamani nina swali nataka kuuliza,utakuta mtu ana mke wake halafu anamtongoza mke wa mtu na kujinadi kwake kua ana mpenda mpaka hana amani hivi hapo anakua amempenda au ametamani kua naye?.
 
kutamani na kupenda sometimes ndio maana moja..

mtu kuwa na mke haina maana anampenda mkewe..

unaweza kuoa kwa sababu tofauti na mapenzi...
 
kutamani na kupenda sometimes ndio maana moja..

mtu kuwa na mke haina maana anampenda mkewe..

unaweza kuoa kwa sababu tofauti na mapenzi...

aisee cjawahi kuwaza hili, kama mtu anaweza kukuoa kumbe hakupendi ana sababu zake tu nyingine,
 
hapa ni kutamani sio kupenda

Kumbuka Wanaume wanatamani kwanza halafu ndio wanapenda na ndio maana inachukua muda sana mwanaume kukuweka kwa moyo na itakapotokea akakuweka kwa moyo ningumu sana kukutoa.

Wanawake wanakuwa rahisi sana kukuweka kwa moyo kwani akikubali tu haichukui muda kukuweka kwa moyo na ndivyo vivyo hivyo kukutoa

cha msingi ni vizuri kujua kuwa
LOVE IS A PROCESS AND NOT A DESTINATION.

Kama ni tamaa za mwili basi hapo hakuna mapenzi ya kuendelea kwani utakuwa unaangalia destination na utakapofika fika hapo unapoelekea na ndio basi kutamani ni sawa na kukubaliana na LoVE is a destination(Tamaa za mwili kwa kutamani ngono) na siyo Love is a process(ambayo ni mapenzi ya kweli na ya dhati)

Kwa hiyo hapo jamaa amemtamani na sio kumpenda
 
kutamani na kupenda sometimes ndio maana moja..

Mtu kuwa na mke haina maana anampenda mkewe..

Unaweza kuoa kwa sababu tofauti na mapenzi...

hii ndio kwanza nisikie leo mimi nijuavyo anaependa kuweka ndani na anayetamani hutumia kwa muda tu au?.
 
kutamani na kupenda sometimes ndio maana moja..

mtu kuwa na mke haina maana anampenda mkewe..

unaweza kuoa kwa sababu tofauti na mapenzi...
Umesema kweli, The Boss. kuna watu wanaishi na wake/waume zao wakati wanapenda watu wengine "God Forbid". Ingawa pia kuwa watu ambao wanawapenda wake/ waume zao lakini pia wanawapenda watu wengine nje. kuna rafiki yangu ameoa lakini ana girlfriend, nilipolijua hilo nilimuuliza inakuwaje ana GF? nikamuuliza kama hampendi tena mkewe, akanijibu kuwa anampenda; na GF akasema anampenda. sikuweza kumwamini kama kuna kupenda zaidi ya 1 kwa wakati mmoja, lakini aliniambia huo ndo ukweli wake.
 
kumbe bado mdogo eeh?

kweli mie bado mdogo naona mambo mengi siyafahamu,kama hili la kuolewa/kuoa mtu usiempenda, unaweza kutufafanulia sababu nyingine za kuoa/kuolewa zaidi ya upendo, kumbe ndo maana vioja haviishi kwenye ndoa, watu wanalala kitanda kimoja kumbe hawapendani
 
convenience........
 
aisee cjawahi kuwaza hili, kama mtu anaweza kukuoa kumbe hakupendi ana sababu zake tu nyingine,

Tafuta maana ya neno opportunist, ndio utajua. Kuna mtu namfahamu ameingia kwenye ndooa kwa kuwa mwanamke ana pesa, yeye hakufuata mapenzi alifuata pesa. Na mpaka sasa kazi yake ni kuhangaika na wanawake wengine kutafuta mapenzi. Kuna wanawake wengine pia huwa wanaolewa na pesa na sio mwanaume. This is the fact of life.
 
Kuoa au kuolewa hakufuta hulka ya kibinadamu ya kupenda au kupendwa. Na wala hakuweki ganzi au kuchora mstari wa mwisho wa kupenda au kupendwa. Kinachotokea ni kuwa umejiwekea mwenyewe limit katika kutafuta au kutafutwa ( availability). Pia umejiwekea mipaka katika kupenda au kupendwa.

Kupenda na kutamani huambatana. Kuna mstari mwembamba sana baina ya kupenda na kutamani. Kutamani yaweza kuwa temporary wakati kupenda kama alivyosema mzungumzaji mmoja hapo juu ni mchakato. Huwezi kumuona mtu na kumpenda hapo hapo.Utaanza na kutamani... kutamani kumjua mtu vizuri au zaidi, kutamani uwe karibu nae zaidi na baada ya hapo waweza kumpenda. Kama ulimtamani tu basi utakapokuwa karibu na kumfahamu zaidi huenda ukaishia hapohapo usimpende tena.
 
Mimi nadhani mtu huanza kumtamani mtu, kisha ukisha mjua vizuri unaanza kumpenda, then unafanya uamuzi wa kumuoa au kuolewa naye. Kwa hiyo watu huoana kwa kuwa walishatamaniana na kupendana. lakini hiyo haikuzuii kumtamani mtu mwingine na hata kumpenda mtu mwingine wakati umeoa au kuolewa na unampenda mwenzio. Suala la kuwa na uhusiano na huyu mtu mwigine uliyemtamani au uliyempenda ni uamuzi mwingine kama ulivyofanya uamuzi wa kuoa. Unaweza kuwapenda watu wengi lakini si lazima uwe na uhusiano nao wote.
 
Kuoa au kuolewa hakufuta hulka ya kibinadamu ya kupenda au kupendwa. Na wala hakuweki ganzi au kuchora mstari wa mwisho wa kupenda au kupendwa. Kinachotokea ni kuwa umejiwekea mwenyewe limit katika kutafuta au kutafutwa ( availability). Pia umejiwekea mipaka katika kupenda au kupendwa.

Kupenda na kutamani huambatana. Kuna mstari mwembamba sana baina ya kupenda na kutamani. Kutamani yaweza kuwa temporary wakati kupenda kama alivyosema mzungumzaji mmoja hapo juu ni mchakato. Huwezi kumuona mtu na kumpenda hapo hapo.Utaanza na kutamani... kutamani kumjua mtu vizuri au zaidi, kutamani uwe karibu nae zaidi na baada ya hapo waweza kumpenda. Kama ulimtamani tu basi utakapokuwa karibu na kumfahamu zaidi huenda ukaishia hapohapo usimpende tena.

are you suggesting there is no love at first sight??
 
Back
Top Bottom