Hivi ndiyo ccm kweli!!!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Katika gazeti la Mwananchi toleo la leo, kuna habari yenye kichwa kisemacho "CCM wafanya mkutano kanisani, washambulia". Katika habari hiyo mwandishi kutoka Biharamulo anasema kuwa kundi la wafuasi wa CCM walivamia Kigango cha Kanisa Katoliki Parokia ya Kaniha kwa lengo la kuchukua viti na Meza kwa ajili ya mkutano wao wa kampeni. Cha kushangaza, waliamua kufanya mkutano humo humo ndani huku wakitumia meza kubwa ya ibada kama meza kuu ya viongozi. Katibu wa kigango alipojaribu kuwasihi waondoke kwenye hiyo nyumba ya Ibada kwani si mahali sahihi kwa mikutano ya siasa, alipigwa na kuumizwa vibaya. Jeshi la polisi likaarifiwa na kutuma vijana wake ambao wamewakamata baadhi ya viongozi wa kanisa huku wakiwaachia wafuasi wa CCM.Viongozi wa Polisi wamekuwa wakitupiana mpira wa nani wa kutoa taarifa rasmi huku Mkuchika akisema atafuatilia. Wanajf, na hii imekaaje, nini maoni yenu?
 
usishangae wakaunganishwa kwenye sakata la DECI.
Zidumu fikira za mwenyekiti CCM.
 
Back
Top Bottom