Hivi ndivyo Lowassa alishiriki Richmond

Ukiwa hujui taratibu za manunuzi na due deligence utajibu kama ulivyo jibu, lakini ukiwa unajua utapingana na majibu ya lowasa.
kwanza unatakiwa ujue kwanini kunafanyika due deligence, hii inafanyika ilikuepuka kupata mkandarasi asiye faa, iwe mkurugenzi wake au hiyo kampuni, na hivi vitu vipo, sio kwamba mimi ninatunga leo, pili mkandarasi kutakiwa kutoa mahesabu yalio kaguliwa, bank statement, wasifu wake kwa kazi alizokwisha fanya etc etc, sasa hili lilifanyika kwa ufanisi? nini yalikuwa mapendekezo ya wataalamu kuhusiana na hili?
Humu JF watu na kwenye magazeti yaliisha anza minongono, Gire nk wakatupa web site na kudai wameweka bomba la mafuta Costa rica etc etc, lakini licha ya huo uongo wao watu waliliona hilo, tena wasio kuwa na resource, je serikali inayo ongozwa na waziri mkuu walishindwa kuliona hilo?
Nini matumizi ya balozi zetu zilizo nje ya nchi? si ni kuisaidia serikali kwa shughuli zilizo nje ya nchi?
Nini matumizi ya AG office ikiwa mshauri mwenyewe wa sheria naye haisaidi serikali.
Jingine unatakiwa ujue wajibu wa kazi za waziri mkuu, nazo ni kumsaidia Raisi, sasa hapa nitakupa mfano aliotoa Warioba , kwamba nyerere alitaka kumchagua kiongozi aliyehukumiwa kwa sheria za uchaguzi, warioba akmwambia mzee utakuwa unavunja katiba, nyerere akawa mbishi kidogo, lakini warioba alikwenda kwa waziri mkuu Sokoinne akampiga shule akaelewa, kesho yake warioba na sokoinne walienda kwa mwalimu, mwalimu nae akasema unajua jana sikulala, nilikuwa nafikiria lile jambo, pia unatakiwa uelewe kwanini nyerere alimlaumu malecela waziri mkuu na makamu wa Raisi? na kolimba katibu wa ccm, raisi Alhaji Ali na mwenyekiti wa CCm, sababu alivyo taka kuingiza mchi OIC, hawa jamaa kwa sababu zao mwenyewe walishindwa kumwambia au kumshauri Raisi na Mwenyekiti wao kwamba hiyo itakuwa ni kinyume cha katiba yetu na Sera ya Chama.
Sasa kwa hili hata kama Raisi alitaka iwe hivyo waziri mkuu alikuwa anatakiwa kulisisitizia hayo mapungufu ambayo aliyaona kama mtu mwerevu angeamua hakubalina na hili kwa maandishi au kwa kujiuzulu, lakini kuonyesha kwamba ni kiongozi dhaifu, hakufanya hivyo , bali nae akashiriki kuingia mkataba tata.
Zaidi ya hapo richmond alianza kusua sua kuleta mitambo kwa kukosa mtaji, na minongono ilikuwepo, sasa hapa ilikuwa ni wakati muuafaka wa kuvunja mkataba for non delivery as per agreement, badala yake wakaridhia kuwauzia huo mkataba Dowans.

August,

Kama Due Dilligence ingekuwa inafanyika Tanzania, leo hii tusingekuwa na IPTL, Rada, GulfStream, ATCL, TRL-Rites, EPA, CIS, Kiwira, Vhalambia, Nolan au Richmond!
 
August,

Kama Due Dilligence ingekuwa inafanyika Tanzania, leo hii tusingekuwa na IPTL, Rada, GulfStream, ATCL, TRL-Rites, EPA, CIS, Kiwira, Vhalambia, Nolan au Richmond!
kwa kutokea hizo scandal ambazo zingine bado tunazifuatilia, hai-halalishi, lowasa kufanya alivyo fanya, na tena alivyo ........., ameanza kufanya madudu from day one, mkapa yeye madudu kafanya karibu ya second term , baada ya kuwadanganya watanzania kwa baadhi ya mazuri aliyo fanya, alhaji pia alifanya madudu second term, sasa wenzetu hawa, ili filimbi inalia kipute kianze , nao wanaanza na madudu. na zaidi ya hapo umeme ndio roho ya nchi, halafu mtu anasema we are right on time, katika ku-take off. etc etc
Pili ndugu yangu nikuulize sasa, kwa sababu watu hawa-heshimu hiyo due deligence ndio kuna halalisha uzuri wa EL. Sasa huo mshahara mnono, wa U-PM, na marupurupu mengine ni yanini. na pensheni ya kustaafu nayo unapewa, rejea warakawa mafao ya viongozi hasa hao wa juu ilikuwa ili wasiingie tamaa na ku-sign mikataba mibovu mibovu, infact hao akina mkapa ipo haja ya ku-reviewe pensheni zao ili kuona kama zinaendana na kazi waliotakiwa kuifanya.
Tatu uelewe hizo kesi zingine zinafuatiliwa , huwezi jua mwaka kesho tukawa na utawala tofauti, ambao utakuwa na uwezo wa kuzi shughulikia hizi tuhuma head on.
Nne ulipokuwa unasoma shule au tulipokuwa tuna soma shule kuna wengine walikuwa wanaiba mitihani, na kufanya juhudi tofauti ili wafaulu, lakini wewe ulikuwa hufanyi hivyo kwa sababu ya uadilifu wako na ulikuwa ukielewa kwamba muda utafika wata kwama, so to lowasa kama wenzie walikuwa wezi/ mafisadi haimanishi na yeye awe hivyo.
Nakuombea kwa Alah/ Mwenyezi Mungu/ Yehova/ God/Jah akupe nguvu na hekima zaidi ili utupe shule na waraka zako.
 
Aliyeandika makala hii akitegemea itaonesha ubaya wa EL kushiriki mchakato wa Rdc amechemsha. Makala inaonesha EL akiwa on top of his game. Ndiyo tatizo la kupigana vita wasiyojua adui ni nani. Oh well.

seemz u know the target of this battle......advice!!!!!!!!!.

i thot u r mature kumbe unajadili kama unafanya practice ya political science....try to be consrtuctive not destructive....

by the way your motive is doubting since you condemn wapiganaji......on the same issue i read in TAZAMA(untrusted paper).......... stop ujuaji...
 
akisafishwa mimi najinyonga au nakunywa sumu

....Duhhh!,tofauti iliyoje hii.Wengine humu wanamategemeo ya Kunyonga Tai na Kunywa Mivinyo??
**Mkuu, nafikiri naelewa machungu ya yanayopelekea mawazo yako hapo juu,This Guy had some weird dreams of making the RAIN, probably the rain that would have caused troublesome Waves, now imagine He wants all of us to think He is the only one who can SAVE the ship!!,C'mon now!!
 
- Naona kuna watu humu mmekamia sana kumsafisha Lowassa kwa udi na uvumba, lakini tunawaambieni kwamba we know better, kwamba Lowassa ndiye aliyekua kiongozi wa wizi wa Richimonduli. Ni Lowassa ndiye aliyevunja kanuni za serikali na zabuni kwa kuingilia kati utafutaji wa zabuni kwa kuwamuru wajumbe wa ile kamati kujadili kampuni moja tu ya Richimonduli, badala ya zingine zote zilizoomba tenda.

- Lowassa ndiye aliyemtuma bangusile, awazuie wanakamati ya zabuni wasiende Texas, kuangalia kwa macho yao Richimonduli na ofisi zake zilipo, mkuu ninazo documents zote nilizopewa na mshiriki mmoja wa kamati, ambaye nilimuonya mapema kwamba he was about to be taken down as a sacrifice ili akishikwa nimwage ukweli, na baadhi yake nilizimwaga kidogo hapa huko nyuma. Alipoitwa Takukuru, huyu mkuu aliwaabisha na ukweli mpaka wakaishia kumuacha kama alivyo

- Lowassa alijichukulia maamuzi yote on his own bila kum-consult Rais, ndio maana moto ulipowaka Rais naye alimuachia abebe msalaba wake, Yona na Mramba, walitimiza sheria ya serikali ya kuruhusu kusamehe kodi, lakini tatizo ni kwamba hawakuwahusisha kamati ya bunge na bunge zima kama sheria inavyosema, ndilo tatizo la wezi wote duniani huwa wanajaribu sana kufuata sheria, lakini wanapindisha kiufundi sana wasijulikane.

- Rais alijua kuhusu kuwepo kwa mchakato wa umeme, one thing hakujua kwamba kuna ujanja unatendeka, alipohisi alimuita Masha na kumtukana sana kwamba kwa nini hakumuarifu mapema, ndipo kwa mara ya kwanza alipopata the glimpse ya the deal ya Lowassa, Lowassa pekee yake ndiye mchawi wa Richimonduli, ndio maana alikimbia bila kufukuzwa, the hero alikuwa Rutabanzibwa peke yake ndiye hakuhusika na ule wizi, wengine wote wakiongozwa na Lowassa walihusika.

- Ya Lowassa kusitisha mkataba ni another myth, kama ni kweli kwa nini Lowassa alitumia Billioni mbili kujaribu kuizima hii ripoti isiende bungeni? Kwa nini Hosea aliudanganya umma kwamba hakuna makosa Richimonduli? alitumwa na nani? Na kwa nini Lowassa alikuwa anamlilia Rais kwamba ni jm ndiye anayeleta fujo za Richimonduli, lakini ishu haina tatizo lakini mwishoni akakimbia mwenyewe bila kufukuzwa? Kama Rais alihusika kwa nini aliruhusu ripoti kwenda bungeni bila kuisoma kwanza, pamoja na kwamba aliambiwa mapema inawahusu marafiki zake wengi wa karibu?

- Jamani kama mnataka kuongozwa na Lowassa, msaidieni na kampeni zenu kama tunavyoziona hapa, lakini msitudanganye kwamba hakuhusika na Richimonduli wakati wengine on the record ndio mliokuwa mstari wa mbele sana kwenye kumsaidia Mwakyembe na ripoti, inatia kinyaa sana!

Lowassa ni mwizi tu, hata mumsafishe vipi ni kazi ya bure, yeye ndiye chanzo cha Richimonduli, bila ya yeye kusingetokea ule wizi, kama hamuridhiki na uongozi wa Rais wa sasa, yasemeni mapungufu yake kama yalivyo, lakini sio kujaribu kumuhusisha na asiyohusika nayo! Kwamba mnaweza kulikomboa taifa kwa kuwagombanisha Rais na Lowassa, kwangu sounds very low kwa sababu hili taifa linapaswa kuwa bigger than hawa viongozi wawili, kama we are running out of ideas za kulikomboa taifa letu basi tusubiri watoto wetu!

Respect.

FMEs!

FMES,

Kama una huo ushahidi unaoutaja, mbona hujaupeleka mahakamani au kutoa nakala hapa ukumbini kama vile watu walivyofanya kwenye mkataba wa Buzwagi?

Mbona umebadilika sana na kuanza kumtetea Rais kwa kila kitu ambacho yeye kwa kauli zake mwenyewe zimekuwa zikimfunga? Je ulisikia alivojibu swali kuhusu Richmond siku alipohojiwa kwenye TV, Simu na Internet?

Unasema kuwa kuwagonganisha ni too low, unakumbuka uchaguzi 2005 walifanyiwa nini kina Mzee Malecela na Salim?
 
kwa kutokea hizo scandal ambazo zingine bado tunazifuatilia, hai-halalishi, lowasa kufanya alivyo fanya, na tena alivyo ........., ameanza kufanya madudu from day one, mkapa yeye madudu kafanya karibu ya second term , baada ya kuwadanganya watanzania kwa baadhi ya mazuri aliyo fanya, alhaji pia alifanya madudu second term, sasa wenzetu hawa, ili filimbi inalia kipute kianze , nao wanaanza na madudu. na zaidi ya hapo umeme ndio roho ya nchi, halafu mtu anasema we are right on time, katika ku-take off. etc etc
Pili ndugu yangu nikuulize sasa, kwa sababu watu hawa-heshimu hiyo due deligence ndio kuna halalisha uzuri wa EL. Sasa huo mshahara mnono, wa U-PM, na marupurupu mengine ni yanini. na pensheni ya kustaafu nayo unapewa, rejea warakawa mafao ya viongozi hasa hao wa juu ilikuwa ili wasiingie tamaa na ku-sign mikataba mibovu mibovu, infact hao akina mkapa ipo haja ya ku-reviewe pensheni zao ili kuona kama zinaendana na kazi waliotakiwa kuifanya.
Tatu uelewe hizo kesi zingine zinafuatiliwa , huwezi jua mwaka kesho tukawa na utawala tofauti, ambao utakuwa na uwezo wa kuzi shughulikia hizi tuhuma head on.
Nne ulipokuwa unasoma shule au tulipokuwa tuna soma shule kuna wengine walikuwa wanaiba mitihani, na kufanya juhudi tofauti ili wafaulu, lakini wewe ulikuwa hufanyi hivyo kwa sababu ya uadilifu wako na ulikuwa ukielewa kwamba muda utafika wata kwama, so to lowasa kama wenzie walikuwa wezi/ mafisadi haimanishi na yeye awe hivyo.
Nakuombea kwa Alah/ Mwenyezi Mungu/ Yehova/ God/Jah akupe nguvu na hekima zaidi ili utupe shule na waraka zako.

August,

Watu wengi humu kamwe hawatanielewa maana wameweka hisia zao (emotions) kwenye hili suala na hasa kuhusiana na Lowassa kiasi kwamba wanadhani namsafisha!

Suala la Richmond ni la Serikali nzima na Rais ambaye ndio msimamizi mkuu ndiye anayewajibika na si mwingine. Kwa kuwa Lowassa alifanya kazi hii kwa uzembe, ilimpasa Rais amfukuze kazi kama vile Nyerere alivyomuondoa Kawawa au Mwinyi alivyomuondoa Malecela.

Watu wanachokifumbia macho ni utamaduni mbovu na mfumo mbovu wa kiutawala na kiuongozi Tanzania!

Suala la kuingia mkataba mkubwa kama huu, halimhusu Waziri Mkuu pekee, ni mpaka Baraza la Mawaziri kwa kuwa tulikuwa kwenye crisis.

Ukisoma walichoandika Nipashe, unaona kuwa Waziri Mkuu alitaka upsates za kila kitu kila siku, which means alikiwakilisha kwa Rais wake kila siku.

Kuna watu ambao wanataka kuonyesha kuwa Kikwete hakuhusika, lakini nawaambia rejeeni interview ya Kikwete ya mwanzo mwa 2007 aliyofanya na NIpashe hao hao na uchangue alichokisema, ndipo utajua ni vipi mchakato mzima ulifanyika.

Lowassa alifanya makosa ya kiutendaji alipopewa jukumu la kuongoza mchalato huu wa kununua Umeme. Na hilo ndilo nililolisema awali kuwa ni makosa ya kiutendaji ambayo kila mtu anafanya.

Lakini watu wanafikiri aliiba, au kajitajirisha. Aliyetajirika na Richmond si Lowass ,bali ni Dowans na wote tunajua ni nani aliyeishikilia Dowans.

Mimi kusema kuwa Lowassa anatufaa, nimetoa sababu zangu za msingi, nikasema inabidi kuwa na sacrifice na compromise.

Ukisoma hii habari ya Nipashe, utaona kuwa kiuchapa kazi na ufuatiliaji, Lowassa was on top of his game! Na huyo ndiye Lowassa ninayempigia debe, uongozi wa namna hiyo wenye kufuatilia mambo.

Je Lowassa hana makosa? swali ni nani kati yetu hajafanya maamuzi mabovu au mabaya? Kawawa na vijiji vya ujamaa, Sokoine na Vita vya Ulanguzi, Malecela na G55 na OIC, na utitiri kibao.

KUna kitu tulimlaumu Mrema kuhusiana na kukataa kushiriki katika Collective Responsibility.

Suala la Richmond ni Collective Responsibility ya Serikali nzima, regardless ya nani alikuwa akiongoza task force. Kwenye task force alikuwepo Mwanasheria Mkuu, Katibu Mkuu Hazina na Katibu Mkuu NIshati. Hao ndio walikaa chini na kupitia makampuni yote yaliyoleta uzabuni kwa haraka haraka na ndio maana protocal za kawaida ziliachwa.

Je kazi hii ya kufanya uzabuni huu ilifanywa kwa kufuatia Sheria na Kanuni au tulikurupuka ili kujihami kutokana na hali ilivyokuwa mbaya?

Ikulu inatoa amri, wanaofuata wanatekeleza amri/agizo, ufinyu wa kufuata kuona kama tunaifanya kazi hii kwa kanuni unatokea, hujuma inafanyika kutokana na aliyepewa zabuni kuwa ni mbangaizji, mwishowe, mkataba unachukuliwa na yule aliyeutaka awali akapigwa panga na GNT kwa kuwa alihujumu kila kitu kwa makusudi ili aje aununue mkatana kwa bei nafuu.

Sasa kama aliyetuhujumu ni Shemeji ya Rais (inasemekana), alikuwa mweka fedha wa CCM na mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, halafu tunakimbilia kushupalia kuwa aliytetuibia na kutuhujumu ni timu ya Serikali iliyofanya uzembe, iweje tuanze kusema timu ya Serikali imeiba?

FMES kasema Yona na Mramba walikiuka kitu, swali ni hili, Yona na Mramba walipofanya waliyoyafanya na kuyachapa katika Gazeti la Serikali, Wabunge, Baraza la Mawaziri, AG na watchdogs wengine wote walikuwa wapi kusema hili lirekebishwe?

Je kwenye suala la Richmond, TISS walikuwa wapi wasimshauri Rais directly kuwa hili ni bomu hata kama Lowassa alikwenda kichwa kichwa?

Kama mtasema Rais aliliacha makusudi Lowassa ajitie kitanzi, ambacho ni kitu cha kipuuzi na ni unafiki kuhusu Urafiki wao, je ile hasara ya nchi kukosa umeme wa kutosha ambayo ni kubwa kuliko hata mkataba mzima wa Richmond ni msalaba wa nani? (The actual cost of shortage of power duting this saga was more than the cost of the damn contract with Richmond!)

Okay lets say mkataba wa Buzwagi for that case. Karamagi kaenda London, kunahitajika mabadiliko kwenye mkataba, anayafanya bila kuwasiliana na AG. Yeye yupo hapo Churchil hotel na Rais. Anakuja anadai alifanya hivyo kwa kuwa ana mamlaka kwa mujibu wa Sheria. Kaingia mkataba wa miaka 25! Zitto katoa siri, kwanza Serikali nzima kwa kuwa wanafanya mambo kisiasa, wakatumia turufu ya kichama na kumshushua Zitto.

Mambo yalipoanza kudoda baada ya watu wa JF kubandika mkataba hadharani, Rais anaundia Tume!

Hivyo basi, all fingers will still point back to Head of State, regardless of outcome. It means he is reckless and negligent.
 
Watch out what you say because the universe may think thats what you want and make sure it happens.....
 
Rev.Kishoka,

..Mwakyembe alidai kuna mambo ambayo yangeweza kuiabisha serikali aliamua yasitolewe ktk ripoti ya kamati yake.

..sasa ukisoma ripoti ile unaona kwamba ambaye hajatajwa ni Raisi tu, lakini kila aliyekuwepo kwenye mlolongo wa tender ile ametajwa.

NB:

..kusema eti Lowassa alijaribu kuuvunja mkataba lakini akawa-overuled ni kutafuta visingizio tu.

..ilibainika kwamba Richmond hawana hela za kutekeleza mkataba huu, sasa ni nani aliwatuma serikali wawapatie udhamini wa mkopo CRDB?

..kumbukeni Richmond walisaini mkataba wa kujenga bomba la mafuta na serikali ya Mkapa. serikali ya Mkapa ikawapa miezi 18 watafute hela za mradi. Richmond walishindwa kupata fedha na mradi ukafa.

..jambo la kujiuliza mbona Mkapa hakujaribu kuwadhamini huko CRDB ili wapate mkopo?

..JK na Lowassa wangewachunia tu Richmond kama alivyofanya Mkapa, tusingeingia hasara tuliyoingia. kwa maoni yangu mkataba ungekufa a natural death.
 
Rev.Kishoka,

..Mwakyembe alidai kuna mambo ambayo yangeweza kuiabisha serikali aliamua yasitolewe ktk ripoti ya kamati yake.

..sasa ukisoma ripoti ile unaona kwamba ambaye hajatajwa ni Raisi tu, lakini kila aliyekuwepo kwenye mlolongo wa tender ile ametajwa.

.

Sasa si unaona jinsi Wapiganaji walivyopigana vita feki? Wao wenyewe walifanya compromise wakaamua kumuacha mkuu kisa walipewa nafasi kulizungumzia suala la Richmond.

Infact kama ningekuwa mimi niko Bungeni wakati ule nikapewa option ya kuchunguza Richmond kama walivyofanya kina Mwakyembe au kupewa dhamana ya kusimamia Tume ya Bomani ya madini, ningechukua la Tume ya Madini!

Don't ask me why!
 
FMES,

Kama una huo ushahidi unaoutaja, mbona hujaupeleka mahakamani au kutoa nakala hapa ukumbini kama vile watu walivyofanya kwenye mkataba wa Buzwagi?

Mbona umebadilika sana na kuanza kumtetea Rais kwa kila kitu ambacho yeye kwa kauli zake mwenyewe zimekuwa zikimfunga? Je ulisikia alivojibu swali kuhusu Richmond siku alipohojiwa kwenye TV, Simu na Internet?

Unasema kuwa kuwagonganisha ni too low, unakumbuka uchaguzi 2005 walifanyiwa nini kina Mzee Malecela na Salim?

- Mkuu vipi hapa JF tuna ushahidi wa kesi ngapi mpaka za Meremeta mbona hatujapeleka mahakamani? Kwani kupelekwa kwa mkataba wa Buzwagi kumesaidia nini kama kina Zitto hao hao sasa wanashangilia Dowans? Unasema nini wewe, kwamba sasa madini yetu hayaibiwi tena kwa sababu mkataba wa Buzwagi ulitolewa?

- Rais hana kosa lolote na Richimonduli, ripoti ipo wazi kule bungeni na wote tunayo, kama ana makosa mengine na wewe unayajua kwa nini hujampeleka mahakamani?

- Halafu kwa nini huna hoja zaidi ya Malecela na Salim, I mean huwezi kuandika bila haya majina vipi bro? hivi ni lin utajifunza kusema solutions, badala ya kila siku kulaumu wengine tu, wakati misery yetu nationally ni ya miaka 47 sasa, almost your age lakini kazi kulilia wapiganaji tu na Malecela na Salim vipi mkuu, Lowassa na Idd Simba ni mafisadi tena original! Naona umepania sana kutuhadaa lakini tutaendelea kuweka record straight! fisadi ni fisadi tu hata asafishwe vipi!

Respect.

FMEs!
 
Huyu bwana EL kwa vigezo vyovyote vile anatakiwa awe mahabusu akingoja mashitaka ya kuhujumu uchumi wa nchi yetu; na kesi yake hatakiwi kupewa dhamana kwani hasara aliyoisababishia nchi yetu kwa kukosa umeme haihesabiki!! Wakati umefika hata hao wanaomlinda nao wawajibishwe bila kumuonea haya mtu!!
 
- Mkuu vipi hapa JF tuna ushahidi wa kesi ngapi mpaka za Meremeta mbona hatujapeleka mahakamani? Kwani kupelekwa kwa mkataba wa Buzwagi kumesaidia nini kama kina Zitto hao hao sasa wanashangilia Dowans? Unasema nini wewe, kwamba sasa madini yetu hayaibiwi tena kwa sababu mkataba wa Buzwagi ulitolewa?

- Rais hana kosa lolote na Richimonduli, ripoti ipo wazi kule bungeni na wote tunayo, kama ana makosa mengine na wewe unayajua kwa nini hujampeleka mahakamani?

- Halafu kwa nini huna hoja zaidi ya Malecela na Salim, I mean huwezi kuandika bila haya majina vipi bro? hivi ni lin utajifunza kusema solutions, badala ya kila siku kulaumu wengine tu, wakati misery yetu nationally ni ya miaka 47 sasa, almost your age lakini kazi kulilia wapiganaji tu na Malecela na Salim vipi mkuu, Lowassa na Idd Simba ni mafisadi tena original! Naona umepania sana kutuhadaa lakini tutaendelea kuweka record straight! fisadi ni fisadi tu hata asafishwe vipi!

Respect.

FMEs!

FMES,

Unajifanya umesahau uhuni waliofanyiwa Salim na Maelcela 2005 na chama chako cha CCM?was it that long that you can not remember kuwa kampeni chafu ndani ya chama chako iliyompa madaraka Kikwete ndiyo iliwapakazia kina Salim na Malecela unazi na tuhuma zisizo na msingi?

Ushahidi wa Meremeta, sisi tumeuweka hapa ndani wazi kwa kila mtu na tumeupeleka Serikalini ufanyiwe kazi, je wako huo wa Richmond umeshauweka wazi hadharani au uko mkobani?
 
Kama Lowasa kahusika 100% katka Richmond...na huyu bwana ni swahiba mkubwa wa mkuu wa nchi si hasha kuwa yeye Lowasa ameshawishi ikulu au ikulu imekula na Lowasa ndo maana linapokuja suala la kushitakiwa Lowasa panakuja uzito kama kwamba kuna kitu kinafichwa sasa mashaka yangu yanaweza kuwa ya kweli kuwa ikulu imehusika na dili la Richmond
 
Jokakuu,
Richmond wameingia Tanzania wakati Kikwete akiwa rais.. wakati wa Mkapa ujenzi wa bomba la mafuta ulikuwa chini ya mamlaka ya Songas wenyewe lakini baada ya kuingia Kikwete ndipo Richmond walipoingia ktk deal hilo na navyofahamu mimi Kikwete alitaka shirika moja toka Qatar wakishirikiana (ubia) na mkewe (Mpya) ndio wachukue ujenzi wa bomba hilo.. Hizi zilikuwa habari za mjini na zenye uhakika..

Kama kweli ulisoma vizuri report ya Mwakyembe utagundua kwamba kila sehemu alohusika Lowassa alijaza question marks na haya maelezo ya Msabah yanadhibitisha zaidi ni kiasi gani Lowassa alihusika. Ni vitu ambavyo hakutakiwa ku report na ukweli ni kwamba barua zote hizi walikuwa nazo tayaro isipokuwa kwa kuheshimu nafasi ya waziri mkuu ushahidi huu ulitakiwa kuwasilishwa bungeni kama bunge lingeamua kumsimamisha kizimbani.

Pengine mnasoma bila kuunganisha lakini ukweli ni kwamba maelezo hyaya ni maelezo ya Msabah waziri wa nishati ktk kujitetea nafasi yake na sidhani kama Msabah anashindwa kumtaja Kikwete ktk barua zote.. Wakuu zangu mara zote rais anapoingilia maswala kama haya kungekuwepo na ushahidi hata mdogo wa barua hata moja kwenda kwa Msabah, Tanesco, kiongozi wa juu au chombo chochote kumhusisha Kikwete au Ofisi yake..mifano mingi tumeiona kwa Mkapa, mbali na hapo Kikwete alikuwa akitalii nje za Ughaibuni, haya maswala ya ndani yote alimwachia Lowassa..Na sijui kama umesahau kwamba wengi wetu tulifikia wakati tukajiuliza hivi rais ni Kikwete au Lowassa!
Huu ndio ukweli ambao watanzania wote tunaukumbuka, kuvisha tai ndewfu hoja ya Richmond haipendezi hata kidogo..
 
TUsisahu kitu kimoja hapa...mwakyembe anasema kuna mambo walificha kulinda heshima ya serikali..wasiwasi wangu hili scandal ni la serikali nzima ya JK....mana kama kuna vitu vilifichwa kulinda heshima ya serikali, ni vitu gani hivyo wakati vilivyotolewa tu vilitosha waziri mkuu kujiuzulu? vingetolewa na hivyo vilivyofichwa? nadhani JK angejiuzulu...pole sana Lowasa, umetolewa kafala ilhali mlikuwa wengi hata na swaiba wako JK...we hukumbuki wakati wa mjadala mkali, JK alipotoka ziara ya marekani alithibitisha kukutana na wamiliki wa kampuni ya RICHMOND, lakini baadae akina mwakyembe wanasema Richmond ni kampuni hewa!..., Mbona Kamati ya Mwakyembe haikumuhoji Rais kujua hao aliokutana nao Marekani na kuzungumza nao ni akina nani?...Pole sana EL......mlikuwa wengi, lakini ilikuwa zamu yako.
 
Mkandara said:
Jokakuu,
Richmond wameingia Tanzania wakati Kikwete akiwa rais.. wakati wa Mkapa ujenzi wa bomba la mafuta ulikuwa chini ya mamlaka ya Songas wenyewe lakini baada ya kuingia Kikwete ndipo Richmond walipoingia ktk deal hilo na navyofahamu mimi Kikwete alitaka shirika moja toka Qatar wakishirikiana (ubia) na mkewe (Mpya) ndio wachukue ujenzi wa bomba hilo.. Hizi zilikuwa habari za mjini na zenye uhakika..

Mkandara,

..hapana. Richmond waliingia nchini wakati wa utawala wa Mkapa na walisaini Memorandum of Understang[MOU] na serikali kwamba watakusanya funds within 18 months kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta la Dar--Mwanza.

..sasa miezi 18 ilipita na hawa Richmond hawakuonekana kabisa. serikali ikaona kwamba jamaa ni wababaishaji kwa hiyo ikawaandikia barua ya kufuta MOU. barua ya serikali kufuta MOU iliandikwa na Bashir Mrindoko ambaye ni Kamishna wa Nishati ktk wizara ya Nishati na Madini. barua hiyo nadhani iko kama kiambatanisho ktk ripoti ya Dr.Mwakyembe.

..actually, Mwakyembe amependekeza Bashir Mrindoko achukuliwe hatua kwasababu hakumshauri vizuri Katibu Mkuu Arthur Mwakapugi kuhusu uwezo wa kifedha wa kampuni ya Richmond.

..baada ya serikali kufuta MOU kati yake na Richmond, sasa ndiyo Kikwete amepata hao wawekezaji toka Qatar kujenga hilo bomba la mafuta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom