Hivi ndivyo ilivokuwa kwenye maandamano ya ccm mbeya katika picha!

Sawa. wana haki ya kuandamana, lakini pia vyama vingine vya siasa vina haki hiyo. Haki sawa.
 
Mbona CHADEMA wakiandamana viongozi wa CHADEMA wanapelekwa polisi na kupigwa mabomu,again kila kitu kina mwanzo na mwisho.......CCM mkae mkijua kuna mwanzo na mwisho......
 
Sawa. wana haki ya kuandamana, lakini pia vyama vingine vya siasa vina haki hiyo. Haki sawa.

Mzee EDO!Nilikuwa namaanisha hivi kama wao wanaandamana kwanini mwanzo walikuwa wanabeza maandamano ya CDM!
Walifikia kusema maandamano ya CDM yanapoteza muda wa wananchi!
 
CHADEMA wakiandamana utasikia mara ooo wanawakosesha wananchi kufanya kazi; au maandamano hayana tija; au wanatishia amani; ...
Na haya maandamano yamagamba tunasemaje?
Juzi wamemtia ndani mbunge baada ya kuweka onyesho lililokaribia kuvunja fiesta yao; sasa wakaona wajaribishe na maandamano. Tutaona mengi kabla ya 2015
 
Jamani tukubali pia ukweli upande wa pili kuwa maandamano na mkutano wa akina 6 umekonga nyoyo.Matokeo mengine ni hapo 2015.Nadhani mkakati mkubwa wa CCM ni kwenda kimakundi kwa hoja ya kumsupport Nape.Wakubwa Msekwa,Mkama,Chiligati na wengineo bara na Zenji wametulia mpaka ngoma inoge.Kuna tetesi kuwa Mwenyekiti anaandaa ratiba ya kuzunguka nchi hivi karibuni hasa baada ya makali ya umeme kupungua ili kuwashukuru watz kwa kura.Hizi harakati za kina6 hazitokomea Mbeya,zitaingia sehemu nyingi kumsafishia njia Mkulu hasa baada ya Mfungo maake hatozunguka katika kipindi cha mwezi Mtukufu maake swaumu kali inaweza leta labsha.Mpango mkakati wale wasiofunga watangulie kuweka mambo sawa sasa.
 
Mwema hakupata taarifa za kiintellijensia kuhusu maandamano hayo?
 
Ni haki yao ya kikatiba jamani. Waache wafanye tu kama yanaweza kuwa saidia. Si waliona lile nyomi la Chadema? na wao wanadhani wanaweza. Wapeni uhuru wafanye ili mradi waombe kibali cha polisi na tuwe na hakika kuwa polisi walitoa kibali vinginevyo itachimbika sasa hivi kati ya polisi na waandamanaji wengine.
 
Kwa maandamano haya yaliyosheheni,CDM imekula kwenu.
Tusi mpendavyo lakini mradi hamna ch kuwaonyesha wana Mbeya kimaendeleo,CDM mkoani Mbeya itakufa tu.
Karibu na Nape ni Prof David Mwakyusa Mbunge wa Rungwe Magharibi.
Naona kuna mambumbu wengi sana wasioelewa siasa za Mbeya


 
Apo wote tukitafuta Body Mass Index,(BMI)=wako ktk catergory ya OBESITY!
 
Halafu tunalalamika madaktari hawatoshi ona huyu daktari mzima yuko majukwaani anapiga porojo iko wapi taaluma yake? They all deserve a standing oviation of the tallest finger!!!!!
 
Sasa hivi ni kupambana kwenye katiba mpya kupata mgombea binafsi
Tangia nimeanza kusoma posts zako leo for the first time nimeona constructive idea from you kumbe una akili timamu ukichaa unaigiza tu bravo kungekuwa na ka thank you ningekubofyea
 
Hivi walitoa notisi ya maandamano yao polisi au kwasababu polisi wengi wapo undercontrol yao? je walihutubia hadi saa ngapi maana Zitto alishawahi kukamatwa na polisi kisa kazidisha dakika 5 kwenye mkutano wa hadhara Singida?...magamba bwana wameona CDM wanafanikiwa kwenye maandamano wakaona ngoja na wao watesti zali..
 
Walikuwa wanaandamana ili iwe nini hasa? Wanatoa shinikizo kwa nani?
 
Wengi wametoka Ileje na Mbarali huko Rujewa na Wahanji wa Chimala. Kyela si rahisi kwenda kudanganywa, na huyo ndugu yao H 2015 mh!
 
Re: Hivi ndivyo ilivokuwa kwenye maandamano ya ccm mbeya katika picha!<!-- google_ad_section_end -->
<!-- google_ad_section_start -->Kwa maandamano haya yaliyosheheni,CDM imekula kwenu.
Tusi mpendavyo lakini mradi hamna ch kuwaonyesha wana Mbeya kimaendeleo,CDM mkoani Mbeya itakufa tu.
Karibu na Nape ni Prof David Mwakyusa Mbunge wa Rungwe Magharibi.
Naona kuna mambumbu wengi sana wasioelewa siasa za Mbeya


Wengi wametoka Ileje na Mbarali huko Rujewa na Wahanji wa Chimala. Kyela si rahisi kwenda kudanganywa, na huyo ndugu yao H 2015 mh!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom