Hivi ndivyo ambavyo gari lako linaweza kukupa hasara

usalama kwanza

JF-Expert Member
Oct 3, 2012
386
157
Inawezekana wewe ni mfanyabiashara, mjasiriamali, meneja usafirishaji, au ni mmiliki wa gari/magari. Leo nataka nikuonyeshe ni jinsi gani gari iwe ni yako ya binafsi au ya kiofisi linavyoweza kukupa hasara kubwa bila wewe kutambua. Nitakupa matukio mbalimbali ya mambo ambayo yamewahi kutokea na athari unazoweza kuzipata Hii inatokana na uzoefu tuliona kama wataalamu wa mitambo ya kisasa ya kiusalama.

Tukio la kwanza:

Hili lilimkuta mmoja wa mteja wetu ambaye aliweka kifaa cha tracking katika gari yake. Kifaa hiki kilimpa uwezo wa kujua eneo gari lililopo, speed inayotembea, kuweza kuzima gari kupitia simu yake, Mteja wetu ni mjasiriamali. Yeye aliwapatia gari vijana wake ili waweze kufanya promotion za bidhaa. Lakini cha ajabu kwa siku nzima ya kwanza hawakuweza kuuza bidhaa yoyote hivyo ilimlazimu kuwalipa vijana posho ya siku nzima iliyofika kiasi cha 30,000/- na pia kuweka gari mafuta ya Ths 20,000/- . Siku ya pili pia waliendelea na promotion lakini nusu saa baada ya kuchukua gari walionekana wakiwa eneo ambalo hawakupaswa kuwepo kwa ajili ya kazi, lakini hata baada ya masaa mawili pia walionekana wakiwa eneo hilo hilo na walipokuwa wakipigiwa simu walitaja kuwapo katika eneo la kazi jambo ambalo lilipingana na kifaa cha tracking ndipo muhusika alipoamua kuzima gari muda huo huo. Mara baada ya kulizima akalifuatilia na kugundua kuwa ni kweli halikuwa eneo la kazi, lakini na kwa siku hiyo pia ilibidi awapatie posho vijana wale 30,000/- na gharama za mafuta 20,000/- . Mara baada ya tukio hilo alianzisha uchunguzi kwa kufanya mahojiano na vijana wale na ndipo ilipogundulika kwa siku mbili zote hawakuwa wakifanya kazi kama inavyotakiwa badala yake walitumia gari la ofisi kwa shughuli zao binafsi .

Mteja huyu kwa siku mbili tu alipoteza kiasi cha Tsh 100,000/- . Jaribu kutafakari ni vipi asingekuwa na kifaa hiki je angeweza kugundua kuwa vijana wake hawafanyi kazi , lakini pia kama angeendelea nao katiaka kazi hii tuseme siku kumi au mwezi angeweza kupata hasara ya mpaka million tatu.

Tukio la pili:

Hili lilitokea kwa kampuni inayojihusisha na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ya kwa ajili ya wateja wake. Kampuni hii iliweka kifaa chenye uwezo kama cha mteja wa kwanza na chenye uwezo wa kujua matumizi ya mafuta. Mara baada ya kuweka kifaa hiki katika magari yote ya kampuni aligundua yakuwa magari yalikuwa hayajazwi mafuta kwa kiwango kinachotakiwa mfano ripoti inakuja inasema gari limejazwa lita arobaini lakini tracking device inasema imejazwa lita thelathini na tano na mida nyingine magari yalionekana kupungua mafuta ghafla kwa kiasi kikubwa. Ndipo kampuni ilipohitaji mtaalamu wetu kwa ajili ya kusaidia kufanya uchunguzi , wakati uchunguzi ukiendelea iligundulika ya kuwa moja ya gari ambalo lilikuwa halitumiki kwa siku za karibuni report ilionyesha kuwa limejazwa mafuta ilihali kifaa kilionyesha kuwa gari halikuwa halijajazwa mafuta na halikuwa limetoka katika siku husika. Na tofauti kati ya mafuta yaliyopo kwenye ripoti na kifaa ni kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa

Hebu fikiria kampuni hii ina magari zaidi ya ishirini tufanye kila gari likienda kuongezwa mafuta lita tano zilikuwa zinaibwa .kwahiyo magari 20 * 5litres * 2000 bei kwa lita= 200,000 kwa hiyo kila wakati magari yalipokuwa yanajazwa mafuta kiasi cha laki mbili kilikuwa kinapotea hapo ni ukiacha yale mafuta ambayo huibwa kwa kunyonywa na ripoti nyingine za uongo. Sasa hebu fikiri wizi huu umekuwa ukifanyika kwa miaka mingi sana.

Pia kuna matukio ya watu ambao kabla ya kuwa wateja wetu walikumbwa na mikasa ifuatayo.

Mteja mmoja ambaye alikuwa anamiliki pikipiki alikuja kuazimwa pikipiki na rafiki yake wa karibu, basi tangia siku amemwazima hajawahi kupata pikipiki yake tena na yule rafiki hapatikani kwenye simu, uzuri ni kuwa mteja alikuwa anawafahamu ndugu zake basi walikubaliana tu kulipa ile pikipiki baada ya vikao kadhaa.

Najua pia na wewe unamikasa mbalimbali ambayo imewahi kukukumba au kuwapata majirani na marafiki .

Isecure technologies, wataalamu wa vifaa vya kiusalama vya kielectroniki inakukaribisha kujipatia kifaa hiki cha kutrack magari na vyombo vingine vya usafiri . gharama zetu ni nafuu sana hazina malipo ya mwisho wa mwezi na gharama ya chini kabisa ni kuanzia Tsh 120,000/- kutegemeana na ufanyaji kazi wa kifaa husika. Kifaa kinafanya kazi kama alarm ya gari ya kawaida na tracking device

N.B inawezekana hujawahi kufikiria umuhimu wa kifaa hiki lakini ipo siku utatamani kujua gari/usafiri wako upo wapi , unafanya nini , matumizi yake ni sahihi, je halihatarishi usalama wa mali zako na bidhaa.

Tupigie kwa mawasiliano zaidi : 0714890018
email; justine@isecuretec.com
 
Asante ndugu ,nitajitahidi rekebisha
Kichwa cha habari kingebadilika. Dereva kukuibia mafuta huwezi kusema kwamba "Gari linakutia hasara", bali hapo ni "dereva anakutia hasara". Vivyo hivyo kwa wale watu wako wa promotion ambao hawakufika eneo la kazi, huwezi kusema hapo kwamba "Gari linakutia hasara". Sijui, labda mimi naelewa tofauti na wengi
 
Ila kweli. Kuna jamaa juz jirani yangu mwenye bodaboda alimpata mteja akawa anampeleka asubuhi na kumrudisha jioni jamaa akajizoesha kwa boda boda kwa kumwachia chenji bila kuuliza, cku nyingne anamwambie nipeleke nikapate supu afu anampa bodaboda ofa ya supu, mbaya zaidi jamaa hakuwa kufika na boda anakolala anaishia maeneo tu ambayo cyo kwake. Cku ya cku akukutana na boda ameshika mfuko wa matunda akamwambia bodaboda naomba pikpik nipeleke haya matunda then uje unipeleke mahali dak 0. Si akapewa pikpik ikawa ndo nitolee mpaka leo pikpik haijapatikana. Laiti angekuwa na hiyo device angepata pikpik yake bila hata jasho.
Wakuu huu ndiyo mwisho wa wizi wa vyombo vya moto
 
unaweza kuwa sahihi ila nimejaribu tu kufanya kichwa cha habari kiwe kifupi cha kueleweka v
 
Ila kweli. Kuna jamaa juz jirani yangu mwenye bodaboda alimpata mteja akawa anampeleka asubuhi na kumrudisha jioni jamaa akajizoesha kwa boda boda kwa kumwachia chenji bila kuuliza, cku nyingne anamwambie nipeleke nikapate supu afu anampa bodaboda ofa ya supu, mbaya zaidi jamaa hakuwa kufika na boda anakolala anaishia maeneo tu ambayo cyo kwake. Cku ya cku akukutana na boda ameshika mfuko wa matunda akamwambia bodaboda naomba pikpik nipeleke haya matunda then uje unipeleke mahali dak 0. Si akapewa pikpik ikawa ndo nitolee mpaka leo pikpik haijapatikana. Laiti angekuwa na hiyo device angepata pikpik yake bila hata jasho.
Wakuu huu ndiyo mwisho wa wizi wa vyombo vya moto
Matukio ya bodaboda kuibiwa ni mengi sana bado wale wanaoporwa baada ya kukabwa. Kifaa kama hiki kwa ajili ya pikipiki unaweza kukipata kwa bei nafuu kuanzia 120,000/-.
 
Nimeona nilete ufafanuzi zaidi ya jinsi kifaa hiki kinavyofanya kazi.

1. Kifaa kinafanya kazi kama alarm.

i) Hii inamaana italiza king’ora ikiwa ghali lako litagushwa au kupata mshtuko

ii) Iwapo alarm italia utapata pia taarifa kwenye simu yako ya mkononi.

iii) Milango ya gari itakuwa imefunguliwa.

2. Kifaa kinafanya kazi ya kutrack.

i) Hapa itakupa taarifa ya kuwashwa kwa gari yako ,

ii) Itakupa taarifa ya kuzimwa kwa gari yako

iii) Utapata taarifa ya utumiaji wa mafuta katika gari yako

iv) Itakupatia taarifa kuhusu mwendo kasi wa gari lako na kama gari lako limezidishwa mwendo.

v) Inayo uwezo wa kukupa taarifa ya gari yako kila baada ya muda utakaochagua , mfano kila baada ya nusu saa , hapa itakuletea mwendokasi wa gari ,mahali lilipo, na muda.

vi) Inao uwezo wa kukupa taarifa ya gari lako kutokana na umbali uliotembea , mfano kila baada ya kilomita 3 itakuletea taarifa gari lilipo, mwendokasi, na muda.

vii) Inao uwezo wa kulizima gari lako popote lilipo na lisiweze kuwaka mpaka pale utakapoamua kuliwasha kwa kupitia simu yako ya mkononi.

viii) Pia lina geofencing function, SOS button , online tracking.
 
Mleta mada sijaelewa ni kwa jinsi gani hiki kifaa kinaweza kumwondolea mfanyabiashara hasara, Mfano umeongelea upande wa promosheni kuwa wahusika hawakufika eneo la tukio, vipi ikiwa wamefika eneo la tukio na wasifanye kilichowapeleka kifaa chako kinasaidiaje?

Nakubalia nawe kuwa unweza kuminize risk lakini huwezi kulimit, Kama wadau walivotangulia kusema kichwa cha habari hakikupaswa kuapia kama kilivo kuwa awali.
Kwa kifupi ni kweli unaweza kupunguza hasara kwa kuhakikisha dereva hazidishi mwendo (Overspeeding) ambayo inapelekea hash brake pia ajali kwa chombo.

Ikiwa mimi ni mteja wako ambaye ninatumia hiyo tracking system nitawezeje kujua kama wakati huu sasa kuna mtu anajaribu ku temper na system?

Pia nitajuaje kuwa kuna lita kadhaa za mafuta zimeibwa wakati siphoning?
 
Matukio ambayo nimeyatolea mifano ni baadhi tu , nimeyatumia kutaka kukutolea mfano uliohai kuwa ni jinsi gani utaweza kujua matumizi mabaya ya chombo chako ambayao mwisho wa siku yataleta athari katika biashara yako .Kuhusu wafanyakazi kwenda na kutokufanya kazi ipasavyo hilo ni jambo lingine . Hata hivyo the device inaweza kuwekewa mic na camera hapo mambo mengi lakini hilo hufanyika kwa gharama za ziada.

sio rahisi kutemper na system kwanza inawekwa sehemu iliyofichwa na si rahisi kujua gari hili lina kifaa hiko mpaka pale utakapoambiwa na pili pale utakapo anza kuichezea itaanza kukataa baadhi ya functions hivyo unaweza kugundua hilo.

Kuhusu mafuta ni kuwa kifaa huwa kinaonyesha utumiaji wa mafuta kwa kutumia chart na percentage , sasa katika hali ya kawaida mafuta tunategemea yatapungua taratibu , haitawezekana ghafla tu ndani ya dakika chache mafuta yashuke kwa lita tano au chart ishuke haraka na kwasababu hatutegemei pia mafuta yashuke wakati gari limesimama au limezimwa .

karibu
 
Inawezekana wewe ni mfanyabiashara, mjasiriamali, meneja usafirishaji, au ni mmiliki wa gari/magari. Leo nataka nikuonyeshe ni jinsi gani gari iwe ni yako ya binafsi au ya kiofisi linavyoweza kukupa hasara kubwa bila wewe kutambua. Nitakupa matukio mbalimbali ya mambo ambayo yamewahi kutokea na athari unazoweza kuzipata Hii inatokana na uzoefu tuliona kama wataalamu wa mitambo ya kisasa ya kiusalama.

Tukio la kwanza:

Hili lilimkuta mmoja wa mteja wetu ambaye aliweka kifaa cha tracking katika gari yake. Kifaa hiki kilimpa uwezo wa kujua eneo gari lililopo, speed inayotembea, kuweza kuzima gari kupitia simu yake, Mteja wetu ni mjasiriamali. Yeye aliwapatia gari vijana wake ili waweze kufanya promotion za bidhaa. Lakini cha ajabu kwa siku nzima ya kwanza hawakuweza kuuza bidhaa yoyote hivyo ilimlazimu kuwalipa vijana posho ya siku nzima iliyofika kiasi cha 30,000/- na pia kuweka gari mafuta ya Ths 20,000/- . Siku ya pili pia waliendelea na promotion lakini nusu saa baada ya kuchukua gari walionekana wakiwa eneo ambalo hawakupaswa kuwepo kwa ajili ya kazi, lakini hata baada ya masaa mawili pia walionekana wakiwa eneo hilo hilo na walipokuwa wakipigiwa simu walitaja kuwapo katika eneo la kazi jambo ambalo lilipingana na kifaa cha tracking ndipo muhusika alipoamua kuzima gari muda huo huo. Mara baada ya kulizima akalifuatilia na kugundua kuwa ni kweli halikuwa eneo la kazi, lakini na kwa siku hiyo pia ilibidi awapatie posho vijana wale 30,000/- na gharama za mafuta 20,000/- . Mara baada ya tukio hilo alianzisha uchunguzi kwa kufanya mahojiano na vijana wale na ndipo ilipogundulika kwa siku mbili zote hawakuwa wakifanya kazi kama inavyotakiwa badala yake walitumia gari la ofisi kwa shughuli zao binafsi .

Mteja huyu kwa siku mbili tu alipoteza kiasi cha Tsh 100,000/- . Jaribu kutafakari ni vipi asingekuwa na kifaa hiki je angeweza kugundua kuwa vijana wake hawafanyi kazi , lakini pia kama angeendelea nao katiaka kazi hii tuseme siku kumi au mwezi angeweza kupata hasara ya mpaka million tatu.

Tukio la pili:

Hili lilitokea kwa kampuni inayojihusisha na usafirishaji wa bidhaa mbalimbali ya kwa ajili ya wateja wake. Kampuni hii iliweka kifaa chenye uwezo kama cha mteja wa kwanza na chenye uwezo wa kujua matumizi ya mafuta. Mara baada ya kuweka kifaa hiki katika magari yote ya kampuni aligundua yakuwa magari yalikuwa hayajazwi mafuta kwa kiwango kinachotakiwa mfano ripoti inakuja inasema gari limejazwa lita arobaini lakini tracking device inasema imejazwa lita thelathini na tano na mida nyingine magari yalionekana kupungua mafuta ghafla kwa kiasi kikubwa. Ndipo kampuni ilipohitaji mtaalamu wetu kwa ajili ya kusaidia kufanya uchunguzi , wakati uchunguzi ukiendelea iligundulika ya kuwa moja ya gari ambalo lilikuwa halitumiki kwa siku za karibuni report ilionyesha kuwa limejazwa mafuta ilihali kifaa kilionyesha kuwa gari halikuwa halijajazwa mafuta na halikuwa limetoka katika siku husika. Na tofauti kati ya mafuta yaliyopo kwenye ripoti na kifaa ni kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa

Hebu fikiria kampuni hii ina magari zaidi ya ishirini tufanye kila gari likienda kuongezwa mafuta lita tano zilikuwa zinaibwa .kwahiyo magari 20 * 5litres * 2000 bei kwa lita= 200,000 kwa hiyo kila wakati magari yalipokuwa yanajazwa mafuta kiasi cha laki mbili kilikuwa kinapotea hapo ni ukiacha yale mafuta ambayo huibwa kwa kunyonywa na ripoti nyingine za uongo. Sasa hebu fikiri wizi huu umekuwa ukifanyika kwa miaka mingi sana.

Pia kuna matukio ya watu ambao kabla ya kuwa wateja wetu walikumbwa na mikasa ifuatayo.

Mteja mmoja ambaye alikuwa anamiliki pikipiki alikuja kuazimwa pikipiki na rafiki yake wa karibu, basi tangia siku amemwazima hajawahi kupata pikipiki yake tena na yule rafiki hapatikani kwenye simu, uzuri ni kuwa mteja alikuwa anawafahamu ndugu zake basi walikubaliana tu kulipa ile pikipiki baada ya vikao kadhaa.

Najua pia na wewe unamikasa mbalimbali ambayo imewahi kukukumba au kuwapata majirani na marafiki .

Isecure technologies, wataalamu wa vifaa vya kiusalama vya kielectroniki inakukaribisha kujipatia kifaa hiki cha kutrack magari na vyombo vingine vya usafiri . gharama zetu ni nafuu sana hazina malipo ya mwisho wa mwezi na gharama ya chini kabisa ni kuanzia Tsh 120,000/- kutegemeana na ufanyaji kazi wa kifaa husika. Kifaa kinafanya kazi kama alarm ya gari ya kawaida na tracking device

N.B inawezekana hujawahi kufikiria umuhimu wa kifaa hiki lakini ipo siku utatamani kujua gari/usafiri wako upo wapi , unafanya nini , matumizi yake ni sahihi, je halihatarishi usalama wa mali zako na bidhaa.

Tupigie kwa mawasiliano zaidi : 0714890018
email; justine@isecuretec.com
Yaani mtu kujua gari iliko hadi awapigie simu walio na gari..?!?! ina maana hiyo system haikuwa inaweza kusoma latitude na longitide za eneo ilipo gari?!
 
Itakuwa haujasoma maelezo vizuri , Kifaa kinauwezo wa kuonyesha vizuri eneo gari lilipo bila tatizo lolote . Hebu pitia tena maelezo
 
Ni kweli sojasoma habaro yote.... Kwani uliposema jamaa aliyeliwa laki si aliuliza..?
labda nikutoe shaka kifaa kinacho uwezo wa kujua sehemu gari lilipo, kwa mteja kuuliza gari lilipo si tatizo inawezekana kabisa wangewea kuwa eneo hilo wakiwa na sababu inayokubalika lakini kwa wao kudanganya eneo lililopo inaonyesha kuwa hawakuwa na nia nzuri, na ndio maana uchunguzi ulifanyika.
 
Back
Top Bottom