Hivi ndio ndoa zilivyo?

manuu

JF-Expert Member
Apr 23, 2009
4,064
10,723
Habarini wandugu,
Wife kaniambia anataka achukue mkopo kazini kwao kama 1.5mil nikamuuliza kwa ajili ya nini akaniambia nataka kuongeza baadhi ya vitu hapa ndani nikamwambia sawa lakini hiyo 1.5m mbona tunaweza kupata kwa mwezi 1 bila we kuchukua huo mkopo kazin?Nikamwabia tuweke bajeti ya pesa kwa ajili ya hivyo vitu unavyotaka then tutavinunua tu.Nikamwambia ipo siku tutajakwama na hapo ndo utachukua mkopo ila kwa sasa sababu hatuna shida ya haraka hivyo haina haja ya kuchukua huo mkopo japo huo mkopo hauna riba ila nikamwambia unaweza chukua leo hiyo 1.5m then baada ya mwezi ikatokea issue ambayo ni urgent inataka pesa tutafanyaje na kama kwa upande wangu mi nikiwa nimekwama kpesa?Kwa sababu mi sikuona umuhimu wa kuchukua hiyo pesa sana nikamwambia aache.Ghafla akabadilika akanza kununa huwa tunakula pamoja nikaona anatenga chakula kila mtu na sahani yake,usiku hataki hata nimsogelee.

Basi asubuhi nikamwambia isiwe tabu sababu mshahara ni wako fanya vile unataka sintokuuliza wala kukuambia chchote kuhusu mshahara wako.Ila toka juzi hatuko vizuri nikitoka kazin nikimsalimia anaitika kama hataki ki ukweli inanikera sana.

Na shida ni kwamba hii ndio tabia yake yaani mkitofautiana maneno kidigo atanuna hapo hadi mi nijifanye mjinga kumwambia mama acha kununa na ile na ile basi ndo uhusiano unarudi tena.Ila nataka nijaribu kuona trip hii nione mwisho utakuwaje coz najua anasubiria nimwambie mama acha kununa.
Naomba munishauri sasa nifayeje wanandoa wenzangu?
 
Kha mie mtu anayenuna simpendi sana kwa sababu anakuwa na kinyongo mno na huwezi kujua anawaza nini.

Jaribu kumchunia na wewe kutoombwa acha kununa uone kama ataweza kununa mwezi mzima anakutega tu huyo na anajua utambembeleza.

Pole mwaya
 
Kha mie mtu anayenuna simpendi sana kwa sababu anakuwa na kinyongo mno na huwezi kujua anawaza nini.

Jaribu kumchunia na wewe kutombwa acha kununa uone kama ataweza kununa mwezi mzima anakutega tu huyo na anajua utambembeleza.

Pole mwaya
KUTO...BWA tena!, hebu edit hapo DA!
 
Manuu!
Inaonekana shemeji si muelewa. Kama mwenyezi Mungu amekujalia unauwezo wa kupata hiyo pesa anayotaka kukopa tena ndani ya mwezi mmoja tu mkopo huo ni wa nini na ananuna nini baada ya kumueleza mambo ya msingi kama hayo?
Inawezekana wife akawa ni mtu wa vinyongo na labda anataka nyumba iwe na vitu vyake kama yeye alivyonunua kwa pesa yake ambavyo ki msingi si kitu kibaya kama tayari katika mipango yenu mlisha panga kufanya mambo mliyopanga.
Kama baba ndio kichwa cha nyumba na umeshauri kwa nafasi yako hataki kusikia wewe mkazia hadi mwisho maana ukiendelea kuruhusu hiyo hali atakuwa anafanya mambo kwa kulazimisha. Matokeo yake ndoa ikizidi mivutano mwishowe huwa mbaya. Endelea kumuelimisha na simamia msimamo wako.
 
Oohh jamani
nimeipenda story
yako kweli..
THIS IS REALY LOVE
mmbeleze mama bwana
Rahaa kweli kama mwanaume wako
akiwa anakudekeza

Borea hata huyu
Anataka kubembelez wa
tu..mmmhhh ungempata
Yule mpaka BM ndo mtapatana..

Kesho rudi home
Mapema mpikie,weka
wine juu yA meza
A bunch of Rosess ,
Mishumaa mmmhhh..

Yes u do have teenager love..
Look after her..

Ps. .sijaolewa natarajia..
Samahani maana ulisema kwa walio olewa tu..
 
huyo anatingisha kibiriti,kwa kuwa anajua akinuna maneno gani aambiwe ili aache kununa.kwa kuwa hiyo tabia ya kununa ovyo inakuchosha,wee jifanye ngangari,na wewe kaa kimya mpaka mwenyewe atapoacha kununa.maana kama ugomvi wenyewe ndio huo,mbona ni mdogo sana wa kumfanya anune.si ashukuru anae mtu wa kumshauri
 
Mbona ushauri uliompa ni mzuri tu, kilichomnunisha ni hicho hicho au anakingine? Haya bwana kweli kwenye miti hakuna wajenzi
 
mna muda gani wapendwa wkenye hii ndoa? coz naona mdada bado hajapata purukushani za ndoa huyu acdhani vitu viogo kama hivi vitakuwa na nafac huko mbeleni, ni jambo dogo sana hili kweny hii game...ana kasumba zake huyo zitakuja kumuisha tu cku zinaposonga mbele mwenyewe atakuw anajibembelezesha.
 
Anaona aibu ofcini kasema atachukua mkopo sasa wewe unamkataza!!
Anyway, ni mambo madogo sana, wala usitie shaka, we mbembeleze msikilize tu, ila kama huwezi kujishusha ndo inakuwa mwanzo wa mambo mengine.
Labda kama alikuwa hakupendi, anatafuta upenyo, ila kama anakupenda, fanya kitu makusudi cha kumuonyesha kuwa unampenda na seriously hupendi hali ilivyo. nenda hata kafanye mazoezi ya kuact. Vinyongo vya kike havina akili kaka yangu. Sidhani kama ungependa kuwa shuhuda
 
Mh,huyo kuna jamaa anamlisha huko na kahitaji hela ndo mbinu ya kuzipata hiyo!
Ukimruhusu tu utasikia anakwambia kaibiwa
 
Kha mie mtu anayenuna simpendi sana kwa sababu anakuwa na kinyongo mno na huwezi kujua anawaza nini.

Jaribu kumchunia na wewe kutoombwa acha kununa uone kama ataweza kununa mwezi mzima anakutega tu huyo na anajua utambembeleza.

Pole mwaya
Nimejaribu kumchunia hadi sasa nahisi kama vile naanza kumchukia
 
Ni vizuri kama ushajua kuwa akinuna anahitaji kubembelezwa ili awe sawa.
Mbembeleze.
Kwani kumbembeleza inakugarimu nin?
Katika mapenzi wote mkitaka kujifanya mpo juu kama kikombe cha babu hamtafika popote.
 
Back
Top Bottom