Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,173
Nape azionya NGOs
Friday, 10 December 2010 20:58
Abdallah Bakari,
Masasi.
UONGOZI wa serikali katika Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara umesema hautasita kuyafuta mashirika yasiyo ya kiserikali yatakayobainika kuwa yanafuja fedha zinazotolewa na wafadhili, kusaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii wilayani humo.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa wilaya hiyo, Nape Mnauye, alipokuwa akifungua mafunzo ya siku kumi kwa wawezashaji wa Benki za Jamii Vijijini (Vicoba) ngazi ya kijiji.
Mafunzo hayo yalikuwa yameandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali ya Saidia Watoto (Sawa) na kufanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi cha mjini Masasi.
Mnauye alisema mashirika yasiyo ya kiserikli ni wadau muhimu katika kuharakisha maendeleo, lakini kama viongozi wake watatawaliwa na tamaa ya kujinufaisha, hayatakuwa na tija kwa jamii.
Alisema kwa msingi huo, uongozi wa serikali katika wilaya yake, hautasita kuyachukulia hatua kali mashiria hayo ikiwa pamoja na kuyafuta.
"Mashirika yasiyo ya kiserikali ni nyenzo na wadau muhimu hasa kama yatafanya kazi na kutumia fedha za wafadhili kama ilivyokusudiwa," alisema Mkuu wa wilaya.
wasiendelee kutoa fedha
Hata hivyo Mnauye, aliisifu Sawa kwa ubunifu na utekelezaji wa miradi inayolenga mahitaji ya jamii.
"Nimemsikia hapa Mkurugenzi wa Sawa amesema wanakusudia kuunda shirikisho la Vicoba la wilaya lakini wanashaka watapaje jengo kwa ajili ya ofisi serikali itatoa ofisi bure na kila aina ya msaada utakaohitajika," alisema.