Hivi naibu Spika anadhani Bunge la TZ ni CCM lipo kushindana na upinzani

Wakwetu

Senior Member
Sep 14, 2008
156
16
Nimeshangazwa sana na kauli ya naibu spika bwana Job Ndugai wakati wa kufunga bunge mchana tarehe 15/7/2011kutangaza kuwa kwa kuwa mtoa hoja wa kambi ya upinzani alipomaliza kutoa hoja hakuuliza wanaounga mkono hoja hivyo hoja yake imepotelea hewani. Mimi najua kwa kuwa bunge linatetea maslahi ya taifa na kwa kuwa hoja yake ilikuwa ni muhimu basi angewaambia aulize wanaounga mkono hoja maana hoja yennyewe ni kwa ajili ya kutetea maslahi ya watanzania na sio chadema kama anavyofikiria ndugai. Kwake yeye ndugai alifurahi Mnyika alivyosahau kusema wanaounga mkono hoja, ni kama alikuwa anategea asahau hilo jambo. Umeme ni jambo la muhimu na limekuwa kero kubwa hapa Tz hivyo kufanya mambo ya kutegeana (unamtega mwenzako asahu ili upande mwingine ufaidi) kwa swala la kitaifa ni ujinga. KUna kukosea na kama kiongozi alipaswa kumkumbusha. Sina imani na Bunge la Tz kwani ni la CCM zaidi na sio kwa manufaa ya watanzania.
 
jamani hakuna mwanaccm alietimamu, hakuna hata mmoja, hakuna mwanaccm anaeweza kufikiri kwa kina matatizo ya taifa hili, kama yupo nitajieni humu jamvini
 
analipa fadhila kwa kupewa safari ya london kutumbua kodi yako...anatia aibu..alitakiwa yeye ndo aulize wanaounga mkono hoja,.mafisadi hawataisha ndani ya ccm,..
 
Kaka tuombe Mungu ifike 2015 nikamtie adabu kupitia Cdm huyu bwana, kwanza huyu bwana huku jimboni kupo taabani sana hakuna maendeleo yanayoonekana,pia dhana ya Uccm imemkaa kichwani vibaya kana kwamba hata issue zina tija ambazo Cdm wamekuazungumza bungeni yeye amekua na mikwara ati kwamba wabunge wazingatie kanuni wakat kanuni hizohizo wana Magamba wanazivunja,pia amekua ni mbinafsi sana katika kuendeleza jimbo la Kongwa kwa ujmla hana manufaa yoyote kwani ameshindwa kulisemea jimbo letu hata akiwa kwani nafasi ya Unaibu Spika inamfanya awe hvyo la msingi hapa tuombe uzima tufike 2015 salama
 
Kwa ujumla huyu bwana anapwaya sana kwenye kiti kile na bahati mbaya huyo bosi wake hawezi kumrekebisha kwani nae ni walewale. Nasikitika sana kuona bunge hili limekusa viongozi
 
jamani hakuna mwanaccm alietimamu, hakuna hata mmoja, hakuna mwanaccm anaeweza kufikiri kwa kina matatizo ya taifa hili, kama yupo nitajieni humu jamvini

Wapo wengi ila wamekaa pembeni na wengine wamekufa hao ni Salimu Ahmed Salimu, Joseph Warioba, Mwalimu JK Nyerere na Edward M Sokoine
 
Back
Top Bottom