HIvi Mwanaume bila ya Mwanamke ni Mchafu?

Uchafu ni tabia ya mtu. Kuna wanaume wachafu kadhalika wanawake wachafu. Unaweza kwenda kwenye nyumba ya mwanaume aliyeoa ukashindwa kunywa hata maji. Hivyo huo uchafu ulioona si matokeo ya mwanamme kuwa singo bali tabia yake. Mbona baba yenu mie kabla ya kuoa nilikuwa msafi sana? Nakumbuka shuleni na jeshini tukifundishwa kutandika vitanda na kuwa mardadi ukiachia mbali kufundishwa nyumbani.

Nakubaliana nawe asilimia zote kuna baadhi ya wanawake ni wachafu hawsaa unaweza kukuta viombo vya jana usiku vimeshinda kutwa havijaoshwa vimefula kwa uchafu
 
inawezekana kweli ukaingia chumbani kwa mwanaume ambae ni rafiki yako wa kawaida tu?unafuata nini wakati kuna sebule,study room n.k!

Andishile kisa remote na soski hajuhi ameweka wapi sababu vitu havijakaa kimpangilio, sasa ile tafuta tafuta ndio mpaka kwa chumba
 
ila mtoa mada, kama umetoa picha halisi za nyumba ya huyo mtu utakuwa hujamtendea haki.

Ndio maana mie sipendi anakuja kwangu na kupiga piga picha, yaani nakugaya for good.

sorrrrrrry Kongosho kwa kutoa picha yako bila radhaa yako.
 
sikukuaribisha uje upige picha nyumba yangu, kwanza ulikuja kwa shida zako bhana ila dah mshkaji umeniumbua sana

Hahahaaaa nilienda Abla kumtembelea mtu flani hivi, yaani nilikuta mende hadi mlangoni
 
ni rafiki yako wa mda mrefu?

ni mara ya ngapi wewe unakwenda hapo?..mara zote nyumba iko katika hali hiyo?

mkewe /mchumba anajua una access ya chumbani?

hhuwa hafiki humu jf? ..
 
Kwahili kunamwanamke nimeishi nae kama miezi mitatu leo nimeamua mtimua ni mvivu na kila kitu anaona sawa hadi kufanya usafi anataka nifanye mm. Hilo gheto lipo pouwa sana sema huyo binti itakuwa ni nyumba ndogo ya mwenye gheto
 
Mmmmmmh uliingia mpakaa bedroom? Ulienda kutafuta nini


anyway huyo mwanaume ni mchafu tu jamani, mwanamke sio maid, kutokuwa nae hakukupi tiketi ya kuwa mchafu...

Ukiona mwanaume mchafu eti kisa mkewe hayupo ujue ana silika ya uchafu tu.... Ndo hao hata kuoga mpaka wasimamiwe na wake zao , na huyo mkewe namhurumia...kuishi na janaume chafu uwiiiiiii
 
..........
Kisa cha kuingia hadi chumbani ni utafutaji wa remote hakujua ameiwaka wapi kwa jinsi vitu vilivyokuwa shaghala bagala

kutafuta remoti hakukupi tiketi ya kuingia kwenye chumba cha wanandoa.....au ulienda kutafuta remote na remonnnnntiiiiii?
 
I see truth in your lies..umefika mpaka kwa room then hizi picha zinaonyesha taa zilikuwa ziko on kwahiyo giza lilikuwemo humo ndani..naextrapolate tu..!!
 
Wanaume wengi hubadilika na kuanza kujiendekeza baada ya kuanza kuishi na wachumba ama wake ambao huwa wanafanya usafi na shughuli nyingine za nyumban

ila ni tabia mbaya kiukweli na inaboa, unakuta ulimkuta mwanaume anatandika kitanda, anadeki room anafua, kupika na kuosha vyombo, lakin baada ya kuanza kuishi na mwanamke anabadilika kabisa mpaka inafikia hatua mwenzi wake anasafiri au anaumwa, mwanaume hata kitanda tu kinamshinda kutandika.............BADILIKENI
 
Hilo nalo neno na mim nina ndg yngu mwanaume anavaa nguo za ,viatu,perfume za bei lakin mashuka yake yanaweza kutandikwa miez3 bila kufuliwa chumba kinajaa makolokoro kibao huku akiambiwa anasema mbona ni kusafi tu wkt hata harufu ndan ni nzito anatumia airfresher.
 
Andishile kisa remote na soski hajuhi ameweka wapi sababu vitu havijakaa kimpangilio, sasa ile tafuta tafuta ndio mpaka kwa chumba

Nakshi we mtundu sana, yaani remote uliitafuta mpaka ukaikuta chumbani! Na hapa ni soksi zipi ulizokuwa unamtafutia?
 
Last edited by a moderator:
ila mtoa mada, kama umetoa picha halisi za nyumba ya huyo mtu utakuwa hujamtendea haki.

Ndio maana mie sipendi anakuja kwangu na kupiga piga picha, yaani nakugaya for good.
to be frank hata mi sijapenda unless anajua utaipost nyumba yake humu!halafu inakuwaje huyo rafiki yako ambaye ana mke anakuruhusu uingie mpka chumbani kwake?sidhani kama ni sahihi.
 
Andishile kisa remote na soski hajuhi ameweka wapi sababu vitu havijakaa kimpangilio, sasa ile tafuta tafuta ndio mpaka kwa chumba
unapata wapi guts za kuingia mwenye chumba cha mwanamke mwenzio aliye na mume wake ilhali yeye mke hayupo?
 
Back
Top Bottom