Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

Kwetu Iringa

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
355
88
Wana JF, nimekuwa katika mawazo mazito sana toka Dr. Mwakyembe aanze kushughulikia sakata la ATCL. Hili jambo limejadiliwa sana hapa jamvini. Wengine wakisema Mwakyembe kakosea wakati wengine waki-support. Hoja yangu iko tofauti na hili. Siko upande wowote wa mjadala huu.

Mara nyingi sana tumeshuhudia au kusikia Pinda akichelea kuchukua hatua juu viongozi waiopatikana na makosa kwa kisingizio kuwa anayepaswa kuwachukulia hatua za nidhamu ni Rais!!

Sasa Mbona Dr. ameweza kuwachukulia hatua hawa vigogo wa ATCL? Pinda, ambaye ni boss wa Dr, anashindwaje kuwachukulia hatua vigogo wa aina hii?

Je hii inathibitisha ile imani ya kuwa Pinda ni mwoga au dhaifu? Au hawa vigogo wa ATCL waliochukuliwa hatua za nidhamu na Dr ni tofauti na wale ambao Pinda anawaogopa?? Au Dr ni jasiri zaidi ya Pinda? Au ni nini?

Nawasilisha!
 
Kuna watu huzaliwa wana confidence na wengine huzaliwa hawana confidence!
Haujawai kuta subordinate ana confidence kuliko bosi wake tena kwa kiwango ata cha kumpiga biti bosi tena akaufyata


Nimewahi!!
 
nampongeza Dr kwa ujasiri wake mi nakasirika sana viongozi wanaosema 'ngoja fulani aje'utadhani wenyewe pale waliwekwa kuziba nafasi tu wanafanana na wanawake fulani ambao mtoto akikosea anamwambia ngoja baba'ko arudi anafikiri anatibu kumbe anaharibu,naomba hao viongozi wajifunze na wabadilike
 
Unashindwa kujua hata weledi wa kiongozi wako?ni mara ngapi umesikia mzee mapinda kuwa ni spring? Tabu yeye kawekwa kama pambo,wenzake wanajitolea maisha yao
 
Mtizamo wangu ni tofauti kidogo! Isingekuwa busara kwa Waziri Mkuu kuingilia kati jambo kama lile wakati kuna Baraza la Mawaziri lanalokaa na kila mmoja kuwajibika. Pili ikumbukwe Lowasa ukiherehere wake wa kuingilia kila kitu ulimponza na hatimae ikamlazimu kujiuzulu. So Pinda amekuwa ni mtu wa kuzingatia sana utawala wa kisheria, kwa mfano hili la ATCL lilikuwa chini ya bodi ambayo ikishindwa anafuatia Waziri husika. Na kama Pinda hajapokea malalamiko yoyote toka kwa Waziri husika au taarifa yoyote yenye utata juu ya aliyetimuliwa hawezi kukurupuka kama alivyofanya Mwakyembe kwa kuamini taarifa za mdomoni (eti nasikia baadhi yenu mkawapigia simu kuwa hela imetoka) na kutengua uteuzi wake. So nadhani sometimes hawa mawaziri pamoja na uzuri wao pia wana mapungufu ambayo huwa ni vigumu kuyaona kwa mtu wa kawaida.
 
Kwetu Iringa,
Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote yale toka awe PM, zaidi ya Kulia na kuahidi ahid tu, na amekuwa PM wa kwanza TZ kutaka kung`olewa na Bunge. yupo buze na Sumry bus service,
 
Bosi Chizi ATCL ampinga Mwakyembe
Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi ambaye hivi karibuni alitenguliwa katika cheo hicho na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wiki jana, amefikisha ramsi malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Uchunguzi wa gazeti la Habari Leo umebaini kuwa Chizi amewasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu akipinga tuhuma zilizoelekezwa kwake na Waziri, Mwakyembe akidai si za kweli na kwamba zimelenga kumshushia hadhi kwa jamii.

Pamoja na barua hiyo, Chizi amewasilisha lundo la vielelezo vikifafanua tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Dkt. Mwakyembe dhidi yake, ili kuthibitisha kutokubaliana na tuhuma hizo kwake. Kaimu Mkurugenzi huyo wa zamani wa ATCL alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo alikiri suala hilo kuwasilishwa ofisi ya Waziri Mkuu, ingawa hakuwa tayari kulizungumzia zaidi kwa madai kuwa liko kwenye mamlaka za juu sasa.

Tuhuma ya sare za milioni 80/-

Maelezo ya Chizi kwa Pinda, yanafafanua kwamba ATCL ilinunua loti 30 za vifaa mbalimbali vya wafanyakazi zikiwamo sare zilizotajwa na Dk Mwakyembe kwa thamani ya dola za Marekani 18, 920 na si dola za Marekani 50,000 kama alivyodai Waziri Mwakyembe, hatua ambayo ilifanya ATCL kuokoa zaidi ya Sh milioni 44 kama ingenunua sare hizo nchini kulingana na bei ya ununuzi iliyowasilishwa ATCL.

Tuhuma ya ukodishaji wa ndege

Anapinga pia kuhusishwa na ukodishaji wa ndege aina ya Airbus ambayo Waziri Mwakyembe alisema haikuwa na sababu ya kukodishwa, akisema ndege hiyo ilikodishwa mwaka 2007 na kufanya kazi hadi mwaka 2008, wakati yeye aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Agosti 2011. Dk Mwakyembe akizungumzia mkataba huo tata wa Airbus, alisema umeifanya nchi kudaiwa Sh bilioni 69 na kusisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yanayoendelea katika shirika hilo.

"Kuhusu ukodishaji wa ndege aina ya Boeing 737 – 500 kutoka Kampuni ya Aerovisto, utaratibu wa kawaida wa ukodishaji wa ndege kwa njia ya wetlease ulifanyika, taratibu zote kama zinavyotakiwa kisheria zilifuatwa.

"Ilikuwa ni suala la kushitua sana kwangu pale nilipopata maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu (Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo) kwamba taratibu hazikufuatwa, na hivyo ndege tuliyoikodi haikutakiwa kuruka kinyume na barua ya Waziri Mwakyembe mwenyewe ya Mei 12, akieleza kuridhishwa na hatua tulizochukua katika ukodishaji ndege na kuturuhusu kuendelea na mchakato," ilisema barua hiyo.

"Suala la kupeleka mkataba wa ACMI kwa AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) ambao si utaratibu wa kawaida, lilikuja wakati mchakato wa kuleta ndege uko katika hatua za juu kabisa. Hata hivyo, maagizo yalizingatiwa; mkataba ulikwenda kwa AG hata baada ya Waziri kutoa maoni yake kuwa ni mzuri. Waziri alitoa kauli kama hiyo pia kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilipokaa Ofisi Ndogo za Bunge hivi karibuni," ilisema barua hiyo.

Tuhuma za fedha na akaunti

Barua hiyo kwa Waziri Mkuu ikifafanua kuhusu suala la sare za ATCL ilisema lilishafanyiwa uchunguzi baada ya Chambo kuunda Tume kuchunguza ubadhirifu huo ikiongozwa na DAP wa Sekretarieti ya Utumishi wa Umma Shekiondo Magesa na Tume kubaini hakukuwa na ubadhirifu wowote na kumpongeza Chizi kwa kuokoa fedha za Kampuni.

"Madai ya Waziri Mwakyembe kuhusu fedha za bima ni kwamba kampuni ya Alexander Forbes ilitoa taarifa, kuwa fedha za bima zingetumwa kwenye akaunti yetu wiki ya nne ya Mei 2012.

Menejimenti ya ATCL ilikaa na kutafakari agizo la Wizara kutaka fedha hizo zipelekwe CHC (Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma).

"Tulisubiri kupata akaunti ya CHC ili tutoe maagizo hayo. Hata hivyo, akaunti hiyo tulichelewa kuipata, ndipo tulipokwenda benki kutaka kupata njia mbadala ya kuhakikisha usalama wa fedha zetu. Mei 28 dola za Marekani milioni 3 zililipwa kwenye akaunti yetu ya Stanbic na Menejimenti ya ATCL ikaagiza benki ihamishe fedha hizo ili zishikiliwe kama dhamana ya ATCL kupata mtaji wa kujiendesha.

"Maagizo ya kuhamishwa pesa hiyo ili zihifadhiwe na benki yalitolewa kwa benki siku hiyo hiyo Mei 28. Asubuhi ya Mei 29 wakati mchakato wa kuzihifadhi haujakamilika, tulitaarifiwa kuwa dola milioni moja zimezuiwa na amri ya mahakama kutoka Kampuni ya Ultimate Security yenye thamani ya dola 993,000.

"Hapo hapo tulielekeza wanasheria wetu wazuie utekelezaji wa amri hiyo na jambo hilo lilifanyika na pesa hiyo ipo kwenye akaunti salama hadi leo, hakuna aliyelipwa kama alivyosema Waziri Mwakyembe. Shauri hilo litatolewa uamuzi Juni 18," ilisema barua hiyo.

Kulingana na vielelezo vilivyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu, gazeti la Habari Leo limebaini kuwa wakati Wizara ya Uchukuzi ikiwasilisha barua ya maagizo ya fedha hizo za bima kuwekwa kwenye akaunti ya CHC, malipo hayo ya bima yalikuwa yamelipwa kupitia akaunti ya Stanbic na kampuni ya Alexander Forbes asubuhi siku hiyo.

Gazeti la Habari Leo lilipowasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo jana, alithibitisha kupokewa kwa malalamiko hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa ATCL na kusema ofisi yake ilikuwa bado inayafanyia kazi ili kufahamu mwenendo mzima wa suala hilo kabla ya kulizungumzia.



Source: Chizi awasilisha barua kwa Waziri Mkuu kupinga 'tuhuma' za Dkt. Mwakyembe dhidi yake - wavuti
 
Wana JF, nimekuwa katika mawazo mazito sana toka Dr. Mwakyembe aanze kushughulikia sakata la ATCL. Hili jambo limejadiliwa sana hapa jamvini. Wengine wakisema Mwakyembe kakosea wakati wengine waki-support. Hoja yangu iko tofauti na hili. Siko upande wowote wa mjadala huu.


Pi
Mara nyingi sana tumeshuhudia au kusikia Pinda akichelea kuchukua hatua juu viongozi waiopatikana na makosa kwa kisingizio kuwa anayepaswa kuwachukulia hatua za nidhamu ni Rais!!

Sasa Mbona Dr. ameweza kuwachukulia hatua hawa vigogo wa ATCL? Pinda, ambaye ni boss wa Dr, anashindwaje kuwachukulia hatua vigogo wa aina hii?

Je hii inathibitisha ile imani ya kuwa Pinda ni mwoga au dhaifu? Au hawa vigogo wa ATCL waliochukuliwa hatua za nidhamu na Dr ni tofauti na wale ambao Pinda anawaogopa?? Au Dr ni jasiri zaidi ya Pinda? Au ni nini?

Nawasilisha!

Pnda amkanza lini kuwa na madaraka. Yupo yupo tu kwenye cabinet
 
Chizi utalalamika sana ila suala la wewe kurudi pale halipo!
Maana nimjuavyo Mwakyembe anaweza ata Kujiuzulu kwa ilo suala!
Kama hauna ukweli kwenye izo tuhuma si usubiri kamati ya uchunguzi waje na report yao!
 
Wakati mwingine inategemea unamwajibisha nani.Pinda si dhaifu ila ni waziri mkuu aliyenyimwa mamlaka.
 
Simply ni kuwa Mh. Pinda hana confidence, ingawa ni mwadilifu na ni mtu ambaye yuko honest, kuhusu Dr. Mwakyembe ni kuwa yeye ni jasiri wala sio mwoga.
 
Back
Top Bottom